TRA yampiga faini ya 3,500,000 dereva kisa kapakia tenga 27 za nyanya

TRA yampiga faini ya 3,500,000 dereva kisa kapakia tenga 27 za nyanya

Thubutu!
Wakulia nani? [emoji2369]

Acha mikwala yako mbuzi hapa!

Kuwa Officer wa TRA ni mgawanyo wa majukumu tu na hao ni watumishi wetu sisi wananchi na wanalipwa kodi zetu!

Tusitishane wala nini!
Kila la Heri mkuu
 
Haha...
Msemo huu unaanza kushika kasi.
Kaka yangu kaniambia kitu kama hicho siku 7 zilizopita.
Tulikuwa tunajadiri biashara flani kwa ajiri ya kupata pesa ya mboga nyumbani.
nadhani watu wengi wameogopa TRA
 
Upo sahihi kabisa. Na haya usemayo nimeyaona kwa upande wa wamikiki wa magari.

Hiki wanachofanya sasa TRA kinawasaidia wamikiki kudhibiti udanganyifu wa madereva.
Mlalamikaji anatetea hii njaa na janja janja ya madereva.

Lakini pia wamikiki wa magari wajali maslahi ya madereva.

Wanaweza kufuata ushauri wangu kwa njia ile ya kwanza au ya pili lakini mmiliki anaweza kupata taarifa zote kupitia rekodi za EFD iliyopo TRA. Ina maana EFD ichukue na namba za usajili za gari. Pamoja na TIN namba ya Dereva au ya kampuni mmiliki wa gari.

Maoni yako mazuri.
Ila utachukiwa na watanzania watetea kupita madili haramu.
Mkuu ukifanya hivyo magari yatapukutika barabarani. Madereva hawahusiki kwa lolote linalohusiana na matengenezo/tozo au malipo mbalimbali ya gari bali yanamhusu Mmiliki wake.

Sasa unapowaruhusu madereva kupakia mizigo mbali mbali bila idhini ya mmiliki wa gari hilo litawapelekea baadhi ya madereva kuwa waongo. Mf kuna aina mbili za usafirishaji kwa magari ya mizigo
1. Transit Goods
2. Local Goods
Nizungumzie hiyo ya kwanza dereva anaweza kupakia mzigo toka Bandarini Dar kwenda Rwanda. Wakati wa kurudi atarudi tupu. Sasa basi dereva anaweza kupata mzigo kutoka mpakani kuja Njia Panda ya Nyakanazi lkn mzigo huo utamaliza taratibu za malipo baada ya siku mbili. Dereva anaweza kumdanganya mmiliki wa gari kuwa gari lile limepata hitilafu mpakani wakati wa kurudi kumbe ni uongo.
Dereva yule atapoteza siku kadhaa njiani kwakuwa ameshapata chochote bila kujali kuwa gari lile lilitakiwa lifike mapema na kufanyiwa service kisha kupakia mzigo mwingine wa kwenda DRC.

Hapa mmiliki atalazimika kukodi gari lingine la kubeba ule mzigo ili asipoteze tender yake ile. Sasa basi kwanini TRA wambane dereva anapopakia mzigo wa njiani?? TRA ndiyo wanaokuwa walinzi na wasimamizi wa gari lile linapokuwa mbali na mmiliki. Hivyo basi dereva mara apatapo mzigo wa njiani anapaswa kumtaarifu mmiliki kisha mmiliki akamtengenezea hati ya malipo kisha akamfowardia control no na dereva kufanya malipo halali ya Serikali.

Hapo wote wawili Dereva na Mmiliki watakuwa salama.

Kwa hizi Local Goods ni rahisi kuzi monitor kwani hayana tofauti na mabasi. Kuna mawakala sehemu mbali mbali ndani ya Nchi kulingana na routes zako.
 
Lile ni tamko tu, ila halibadilishi nguvu ya sheria waliyonayo hao jamaa
Raisi alizungumzia ushauri wa mazao na siyo kodi ya biashara ya kusafirisha vitu.

Hiyo aliyozungumzia raisi inahusu mwenye mzigo au mkulima na hii ya usafirishaji inahusu mwenye gari au kampuni ya usafirishaji.

Jamaa kachanganya hizo tozo aina mbili tofauti. Hiyo anayolalamikia mdau ni ya usafirishaji siyo ya mazao.
 
Tenga 27 kwa bei ya juu kabisa ya mwezi uliopita ni 675,000 Tsh.

Faini inapigwa 3,500,000. Mfano angelipa kodi ilitakiwa iwe shilingi ngapi?

Kuna miongozo ya faini? Mfano thamani ya kipi inaangaliwa mpaka kuamua mzigo wa 675,000 faini iwe 3,500,000?
Mkuu faini ni adhabu. Mara nyingi inakuwa kubwa kuliko pesa uliyokwepa kulipa ili usirudie tena kukwepa kodi.

Uone ni bora kulipa kuliko kuja kukutana na hiyo adhabu.
 
Wao wanajilipa mamilioni meengii wengine 9, wengine 12, wengine 15 huyu dereva wa watu pengine salary ni laki 5 au 6
Mwenye nguvu mpishe, usipompisha unaumia. Mifumo ya dunia iko hivyo na kamwe dunia haitakaa iwe na haki wala usawa.
 
Mkuu faini ni adhabu. Mara nyingi inakuwa kubwa kuliko pesa uliyokwepa kulipa ili usirudie tena kukwepa kodi.

Uone ni bora kulipa kuliko kuja kukutana na hiyo adhabu.
Ni kweli lakini nini kinatathmini ukubwa upi unatosha?

Thamani ya matenga yote yakija sokoni na kuuzwa haizidi 700,000 hii inamaanisha hata 700,0500 ni kubwa.

Sasa kitathmini cha ukubwa wa adhabu ifike 3,500,000 ni kipi?
 
Tenga 27 kwa bei ya juu kabisa ya mwezi uliopita ni 675,000 Tsh.

Faini inapigwa 3,500,000. Mfano angelipa kodi ilitakiwa iwe shilingi ngapi?

Kuna miongozo ya faini? Mfano thamani ya kipi inaangaliwa mpaka kuamua mzigo wa 675,000 faini iwe 3,500,000?

Hapo umehama topic: Kesi iliyopo siyo kodi ya mzigo au mazao, bali kesi ni kwa dvr kupakia mzigo na kupokea gharama za usafirishaji bila kutoa risiti ya EFD ama nyaraka ya Kampuni ya kibali cha kusafirisha mzigo wa aina hiyo.

I believe sheria hizi zilikuwepo toka zamani lakini kulikuwa hakuna usimamizi serious kama sasa..
 
Hapo umehama topic: Kesi iliyopo siyo kodi ya mzigo au mazao, bali kesi ni kwa dvr kupakia mzigo na kupokea gharama za usafirishaji bila kutoa risiti ya EFD ama nyaraka ya Kampuni ya kibali cha kusafirisha mzigo wa aina hiyo.

I believe sheria hizi zilikuwepo toka zamani lakini kulikuwa hakuna usimamizi serious kama sasa..
Kwahiyo kutotoa risiti haijalishi ni ya shilingi 5000, laki saba au laki nane faini ni milioni tatu na nusu?
 
Kwahiyo kutotoa risiti haijalishi ni ya shilingi 5000, laki saba au laki nane faini ni milioni tatu na nusu?

Hiyo ndiyo adhabu iliyowekwa dhidi ya kosa la kukika sheria ya kodi Mkuu..!
 
Sijakataa hyo faini.
Suala mzigo ulikuwa unatoka SHAMBA.
Na huyo derev kwa maelezo ya mleta mada.
Dereva alimsaidia tu huyo mwenye mazao yake..
Hata pale mkata Kuna watu ukaa na msgunia yao ya machungwa n.k wanasubiri malori ya kurudi nayo dar.kosa la dereva lipo wapi?
Mkuu inatakiwa msafirishaji atoe risiti kwa huduma ya usafiri ,
Hapo mwenye mzigo hajaguswa kabisa naye anatakiwa awe na risiti yake , maswala ya kusema nilikuwa namsaidia mtu hayapo kwenye sheria in fact kutokujua tu sheria ni kosa kisheria.
Unaweza kusema nawatetea Tra ,in fact mimi binafsi ni muhanga mkubwa wa hizi sheria za Kodi amabazo zilitungwa kimhemko tu bila kuzingatia Hali halisi.
Hizi sheria zikisimamiwa kikamilifu zitaleta mfumuko mkubwa wa Bei hasa kwa items perishable masokoni ,
 
Hapa tunamzungumzia transporter lazima awe na efd machine kwa ajiri ya kuwapa risiti hao anaowabebea mazao eg tenga moja elfu 2 basi ampe na risiti.
Not a chance , transporter hahusiki na mizigo midogo midogo Kama hiyo , yeye keshaandika ristii yake ya mzigo kwenda kongo anajua gari lake linarudi empty , hawezi kuandika risrit za namna hiyo ni hasara kwake , dereva akijiongeza ndo inatokea mlipuko Kama huo
 
Back
Top Bottom