TRA yavunja rekodi ya makusanyo ya mwezi Desemba 2020

Twende pamoja nami kwenye uzi huu.

Niseme tu kwamba Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John P. Magufuli ni Shujaa wetu.

Kwa maana tukifuatilia kwa umakini tulipokuwa, tulipo sasa na tunapokwenda hakika tuna kila sababu ya kumpongeza Shujaa wetu Dkt.John P. Magufuli

β˜†Kwa Mujibu wa Taarifa ya ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, ni kuwa Mamlaka hiyo imefanikiwa kukusanya kiasi cha Tzs Trilioni 2.088 katika kipindi cha mwezi Desemba 2020, ukilinganisha na lengo la kukusanya kiasi cha Tzs Trilioni 2.072, ambayo ni sawa na ufanisi wa 101.00%, kiwango hiki cha makusanyo kwa mwezi hakijawahi kufikiwa katika historia ya mamlaka.

β˜†Hii imefanya jumla ya makusanyo kuwa ni Tzs Trilioni 9.983 kwa kipindi cha nusu ya mwaka wa fedha 2020/21, ambapo huu ni ufanisi wa wastani wa Tzs Trilioni 1.664 kwa mwezi ikilinganishwa na wastani wa makusanyo ya Tzs Trilioni 1.500 kwa kipindi kama hiki kwa Mwaka wa Fedha 2019/20, Ifahamike hii ni sawa na ongezeko la 11.00%.

β˜†Hii inatuonyesha kuwa ni dhahiri shahiri kuwa watanzania kwa ujumla wamekuwa ni wazalendo wa hali ya juu kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari, liacha ya changamoto mbalimbali.

β˜†Jambo la kuzingatia ili tuendelee kuhakikisha nchi yetu inaendelea kusimama imara na kuimarika kiuchumi ni kila mtanzania kuendelea kuonyesha uzalendo kwa kuwajibika kudai risiti, kutoa taarifa ya upotevu wa mapato na kutoa mrejesho wa kuwezesha mamlaka ya mapato kutekeleza majukumu kwaa ufanisi, hata hivyo ikumbukwe kudai risiti yenye taarifa sahihi, siyo suala la hiari, ni takwa la kisheria.

》Nachelea kusema PAMOJA TUIJENGE TANZANIA
#PamojaTuijengeTanzania
 
Watumishi wanatunyonya Sana, yaani karibia nusu ya pato kwa mwezi wanachukua wao, na bado wanadai nyongeza,

Sioni kama Taifa namna tunaweza fanya maendeleo kama kipato almost chote tunalipana mishahara tu.
Umesahau hao watumishi wa umma wanaolipa kodi kibao.
PAYEE, wakinunua vitu wanalipa VAT, ..... mtiririko unaendelea namna hiyo.
 
Mishahara iendane na kipato,

Kwahiyo unaona sawa wengine wakamuliwe ili wakanufaike wengine,

Kama unaona mshahara ni mdogo si unaacha tu wengine watafanya.
Wengine wapi wasiostahili nyongeza za mishahahra,wala kupandishwa vyeo kwa mujibu wa sheria,ilhali tunatangaziwa makusanyo TRA ya kusadikika.
 
 
Twende pamoja nami kwenye uzi huu.

Niseme tu kwamba Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John P. Magufuli ni Shujaa wetu....
Mwanzoni modality ya ukusanyaji mapato ulikuwaje ukifananisha na sasa. Maana kwa sasa TRA ndio inakusanya vyanzo vyote hata vilivyokuwa vikikusanywa na halmashauri. Tukianzia hapo ndio tutajua hizi ni sifa za kijinga ama vipi.
 
Haileti maana kuwa fedha yote iishie kwenye mishahara tu,

Litakua taifa la ajabu Sana lisilo na vision yeyote,

Ni sawa na kuwa na familia ambayo kipato chake chote ni kwaajili ya chakula tu.
Unataka kusema mishahahra ni kitu kinachozuka ghafla bila kuwa NM kwenye bajeti?.
Mbona kuna matumizi mengi ya matrilioni yanayotekelezwa nje ya bajeti.
 
Hizo trioni mbili wamezikusanya vipi jamani mbona serikali ya Jiwe imetufanya kama mazwazwa
Yawezekana wamepata hizo 2t kwa mwezi wa 12 lkn january haiwezi kuwa hiyo lazima itakuwa chini sana na wataipata tena 2t mwishoni mwa mwezi 3. wafanyabiashara wanajua kwann nasema hivyo
 
Ukweli isiopingika mkuu
 
Na hapo bado ktk kada nyingi Serikalini kuna upungufu mkubwa sana wa watumishi,mfano kada ya elimu na afya kuna upungufu sana,kama wangeajiriwa kiukweli kweli wote,wage bill ingepaa sana
 
Aongeze basi mishahara hata kwa hao TRA wanaingia lawama kila kona kutimiza lengo la makusanyo walilopewa na Rais.
TUWE NA SHUKRANI NA WATU WANAOUMIA KWA AJILI YETU.
 
Bado upigaji upo sana TRA.Tukidhibiti kisawa sawa Trillioni 3 is a possibility.
Watumishi TRA wasio waaminifu wana-tuangusha sana,wadhibitiwe.
 
Mkuu ulitaka ukusanye wewe?

Ficha upumbavu wako kabla kukimbilia keyboard.

Kipindi cha nyumba fain za police na makusanyo mengine yote tofauti na kodi yalikuwa yakikusanywa na idara mbali mbali.Leo hata mtoto mwanafunzi anayejiunga na kozi ya uuguzi mbulu fedha zinakwenda mfuko Mkuu halafu tunakuja kujidai tumekusanya zaidi.

Hii ndio hoja kuu,kujimwambafai kwa sifa za uongo.
 
Itakuwa imefikiwa kwa sababu ya matangazo na maangalizo ya TRA na mamlaka mbalimbali kutaka watu wote walipe kabla ya mwisho wa mwaka.

November 2020 na January 2021 kutakuwa na picha tofauti na December 2020. Badala ya kushangalia December 2020, wajiandae kuelezea picha ya January 2020!!

Shida yetu kubwa na kupenda mihemuko!!
 
As a matter of fact you have never appreciated this Government, although you enjoy the tangibles. We are not going to allow few individuals like you to think that you own this country. There are free countries out there to be explored. The choice is yours.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…