Twende pamoja nami kwenye uzi huu.
Niseme tu kwamba Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John P. Magufuli ni Shujaa wetu.
Kwa maana tukifuatilia kwa umakini tulipokuwa, tulipo sasa na tunapokwenda hakika tuna kila sababu ya kumpongeza Shujaa wetu Dkt.John P. Magufuli
☆Kwa Mujibu wa Taarifa ya ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, ni kuwa Mamlaka hiyo imefanikiwa kukusanya kiasi cha Tzs Trilioni 2.088 katika kipindi cha mwezi Desemba 2020, ukilinganisha na lengo la kukusanya kiasi cha Tzs Trilioni 2.072, ambayo ni sawa na ufanisi wa 101.00%, kiwango hiki cha makusanyo kwa mwezi hakijawahi kufikiwa katika historia ya mamlaka.
☆Hii imefanya jumla ya makusanyo kuwa ni Tzs Trilioni 9.983 kwa kipindi cha nusu ya mwaka wa fedha 2020/21, ambapo huu ni ufanisi wa wastani wa Tzs Trilioni 1.664 kwa mwezi ikilinganishwa na wastani wa makusanyo ya Tzs Trilioni 1.500 kwa kipindi kama hiki kwa Mwaka wa Fedha 2019/20, Ifahamike hii ni sawa na ongezeko la 11.00%.
☆Hii inatuonyesha kuwa ni dhahiri shahiri kuwa watanzania kwa ujumla wamekuwa ni wazalendo wa hali ya juu kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari, liacha ya changamoto mbalimbali.
☆Jambo la kuzingatia ili tuendelee kuhakikisha nchi yetu inaendelea kusimama imara na kuimarika kiuchumi ni kila mtanzania kuendelea kuonyesha uzalendo kwa kuwajibika kudai risiti, kutoa taarifa ya upotevu wa mapato na kutoa mrejesho wa kuwezesha mamlaka ya mapato kutekeleza majukumu kwaa ufanisi, hata hivyo ikumbukwe kudai risiti yenye taarifa sahihi, siyo suala la hiari, ni takwa la kisheria.
》Nachelea kusema PAMOJA TUIJENGE TANZANIA
#PamojaTuijengeTanzania