TRA yavunja rekodi ya makusanyo ya mwezi Desemba 2020

Ahaaaa. Hongera kamanda. Sio kwamba sijui bei ya vitu. Mimi niliweka bei ya darasa kama bei elekezi ya halmashauri nyingi zinavyotangaza kandarasi. Madarasa mengi yana bei ya 40 mil. Kama wewe ulijeng kwa mil 6 inakuwaje kunakuwa na upungufu wa madarasa? Inabidi tufanye utafiti juu ya hili.
 

Kwa bei elekezi ni sawa maana wana vigezo vyao, na michakato yao ya kisheria kwani ni pesa za umma ambazo huenda zinafikisha bei hiyo. Lakini mimi nilijenga darasa kama darasa. Kumbuka darasa ni chumba kutupu kisicho na chochote ndani. Bati unapaua mgongo wa tembo. Mlango na madirisha basi. Na ujue kwenye ujenzi wangu mimi, hakukuwa na kikao cha maamuzi ya pesa yangu, zaidi ya kumtaarifu mwalimu Mkuu, na yeye kutoa taarifa kwa mamlaka husika kuhusu nia yangu njema. Uzuri nina maelewano mazuri na viongozi wa huko anakotoka baba yangu, maana wengi tuna undugu na kufahamiana nao, hasa ukizingatia babu yangu alikuwa mtu maarufu na vijisenti vya hapa na pale, na ukoo wetu ni mkubwa maeneo hayo. Hilo water tank mbona umesema ni 2m, nenda dukani hata sasa uona kama linafika hata laki 8. Labda hiyo bei ni ya kwenye hiyo michakato. Lakini ukiwa na laki 750, hata sasa hivi niambie uko wapi hapa Dar nakuletea ulipo bila hata kukudai nauli ya usafirishaji.
 
Hizo trioni mbili wamezikusanya vipi jamani mbona serikali ya Jiwe imetufanya kama mazwazwa
Asante kwa kuliona hilo. Halafu DENI LA SERIKALI LIMEFIKA Tsh 55 Trillion. Hii ni dalili mbaya kiuchumi na kiserikali. Nchi hii inadanganya kila siku kuwa makusanyo ya TRA yamepanda, na uchumi unakuwa. Najiuliza kama Uchumi unakuwa na makusanyo yako juu kwa nini DENI la Serikali likue?
Njia ya mwongo ni fupi! Mumedanganya miaka 5 kuwa mnakusanya kodi kuliko Serikali za Awamu tangulizi kumbe ni takwimu za UWONGO.

Halafu Serikali inakurupuka kuwekeza kwenye miradi inayoitwa TEMBO MWEUPE ambayo kwanza inakula fedha nyingi, haizalishi, ni inachukua muda mrefu kukamilika.

Watu wakiwashauri au kuwakosoa mnawapiga RISASI au mnawafungulia KESI ZA KUTAKATISHA FEDHA.

You can Rig Elections But You can't Rig Economic Growth.
 
Deni kufikikia tril 55 sio jambo baya kama linalipika,ndio maana kila mwezi **** bilions 300+ zinatumika kulipa deni la taifa. Maana ni deni la muda mrefu.

Deni kuwa kubwa ni sababu ya miradi mikubwa inayoendelea nchini hii sio sababu ya kuashiria kuwa uchumi haukui.

Napinga unapoinanga serikali inapiga risasi wanaoikosoa,unatakiwa ukosoe kwa lugha ya staa. Wewe unaesema takwimu za Tra ni za uongo tupatie za ukweli.
 

Kwahiyo usipoikosoa serikali kwa staha adhabu yake ni kupigwa risasi?
 
Ahaaa,hapana bosi. Mahakama zipo na watu wanaotumia lugha isiyofaa umeshuhudia wakipelekwa huko

Tumeona wakosoaji wakipigwa risasi na hata kuuwawa. Na wanaopelekwa mahakamani wanabambikiwa kesi tofauti ili kukomolewa.
 
Tumeona wakosoaji wakipigwa risasi na hata kuuwawa. Na wanaopelekwa mahakamani wanabambikiwa kesi tofauti ili kukomolewa.
Unaweza ukawa sawa ila unayosema yanahitaji kuthibitisha,maana kama mtu anakosoa juu ya sera mbaya za serikali atapigwa risasi? Mahakamani utambambikia kesi kiulaini?
 
Unaweza ukawa sawa ila unayosema yanahitaji kuthibitisha,maana kama mtu anakosoa juu ya sera mbaya za serikali atapigwa risasi? Mahakamani utambambikia kesi kiulaini?

Mahakama ingekuwa huru ukweli ungeweza kuwa wazi zaidi. Ila mahakama hazina nguvu kwenye nchi za madictator.
 
Mtasikia mengi taarifa sahihi na zisizo sahihi kwa sababu wakosoaji hawapo tuipokee tu kwa mikono miwili lakini awamu ya tano kampeni haziishi.
 
Siyo imevunja rekodi hata thamani ya pesa haionekani,, wenyewe ni kukusanya tu hawajui jinsi tunapata tabu sisi wafanya biashara
Wao kazi yao kufunga biashara kufunga Account kuwabambikia kodi kubwa wafanyabiashara kwa njia haramu za kishetani
 
Makonda aliwabambikia tuhuma feki kwa njia za kishetani ndiyo maana laana ikamkuta na kutupwa nje , hata maofisa wa TRA wanaoshiriki vitendo vya kuwabambikia kodi kubwa kufunga Account biashara za watu kwa nia ya kutengeneza mazingira ya Rushwa watambue kuwa laana zinawaandama mda si mrefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…