TRA yazindua kodi ya kitanda kutoka kwa Watalii

Tii shuruti.
 
Hata hao mnaowatetea ukienda kwao kulipa bed time levy ni utaratibu, sio swali wala ombi
Erythrocyte kuna vitu watanzania tunaongeaga na kufanya hadi hao Mabeberu wenyewe wanatuhurumia. Tofauti ZA kiitikadi zisfanye tukakosa uzalendo
Hebu nenda kwenye taarifa yangu pale juu kabisa halafu niambie kosa nililofanya , kwamba taarifa hii ulitaka iwe siri ?
 
Nani aliyempa leseni kama si kuikwapua kwa msaada wa tume na vyombo vya dola.
 
Tunataka habari kama izi zisizo pambwa kwa mbwembwe tuone uozo na uzuri bayana

Leta nyingine dada yetu ..
Serikali haihamasishi watalii bali inawafukuza kwenye hoteli na vivutio kwa utitili wa kodi bila kuzingatia haki za mlipa kodi
 
watanzania tunapenda kulalamika, kwanza hii kodi haikatwi wa mtalii wanaokuwa wame booking kwenye makampuni ya utalii, mfano mtalii akitumia zara tours hachajiwi hii kodi, mara nyingi price za makampuni huwa wina tax inclusive kwenye final price zao mtalii akilipia tour amemaliza except otherwise . Hii kodi ni kwa wale wanaotoa huduma ya bed & breakfast. mfano https://www.airbnb.com/ mtu ukifanya booking kwa hii njia lazima alipie hiyo kodi mara nyingi anakatwa host au client kulingana na sheria ya huo mtandao, hii sheria ipo nchi nyingi tu hamna cha kushangaza
 
Ni jambo la kheri kama wamepunguza PAYE kwenye mishahara ya wafanyakazi, na ikepelekwa sehemu nyingine. Ni kweli serikali inahitaji pesa kwa ajili ya maendeleo. Sasa wapunguze PAYE halafu wasiwachaji wageni?
Tumeshawazoea lazima mazumbukuku muwepo,kuna mambo mengine sio ubunifu ni wendawazimu,umeona wapi duniani wakawa na kodi yakitanda alicholala mtu?
 
Haya mambo na huko kwa wenzetu yapo kweli
 
Mkuu erthrocyte yani unaongoza kwa kutafta habari zenye mlengo hasa wa kuonyesha taswira mbaya kwa serikali kuwa eti " hali ni mbaya"
Hongera kwa hilo[emoji23][emoji23][emoji23]
yani huyu dada hajawahi post eti "magufuli awanyoosha mabeberu...." mwikoooo yeye yale mabaya tu ,daah kuna watu wanaroho ngumu aisee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mzee baba endelea kusifu na kuabudu,wenye mamlaka watakuona aisee.
 
Hali tete sasa watabuni kodi za kila aina.
Kiashiria hali ngumu huku covid-19 huku misaada ya mabeberu imepunguzwa kuchangia bajeti ya serikali ya CCM Mpya na pia hoteli kama ya nyota tano Ngurdoto Mountain 5 star kugeuzwa hosteli n.k ni kiashiria fuko kuu la hazina ya serikali linapungua lazima sasa vyanzo kutafutwa vya ndani bila kuathiri biashara ya hoteli za kitalii n.k

Naona TRA imeanza kufuata mtindo wa kodi za mabeberu ambao kwa muda mrefu sekta ya mahoteli kodi hulipwa kwa kitanda kwa kumaanisha wasipokuwepo wageni na mwenye hoteli atalipa kodi kidogo tofauti na ilivyokuwa TRA wao walipiga mahesabu kwa makadirio bila kutaka kujua wageni wangapi walilala na kipindi hiki cha COVID ndiyo TRA akili zimewarudi kuhusu uendeshaji halisi wa sekta ya hoteli za kitalii ikiwemo high season na low season.

Mabeberu pia hutoza mbali ya kodi ya kitanda pia kodi ya maji taka na halmashauri kufuatana na siku ulizolala mgeni. Hii pia TRA naamini wataiigiza ili kuongeza mapato kwa serikali na halmashauri kwa wageni hotelini wanaotumia mifumo ya majitaka na safi ya miji.
 
Mbona hii ilikuwepo toka mwaka 2013 ? tatizo watu mnakwepa kodi mpaka mnasahau kama zilikuwepo, safari hii hakuna janja janja.
Source: https://www.maliasili.go.tz/highlig...of-the-collection-of-tourism-development-levy
View attachment 1641818
JF imekuwa sehemu ya propaganda za kwenye migahawa. Wabunge wa 2013 wanahusika huo ulikuwa wakati wa Vasco Da Gama aliyekuwa anavumbua dunia, lakini lawama zote kwa mtekelezaji. Safi sana JPM sheria ni msumeno wasiotaka wahame nchi. Uzuri moja wanaolipa wala hawalalamiki lakini vibaka wanaolamba peremende haweshi kutapatapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…