TRA yazindua kodi ya kitanda kutoka kwa Watalii

Kwani hili baya, kupeana taarifa kuwa kuna kodi ya Kitanda Siku nayo nongwa au ni wakala wa mabeberu? Jamani kuweni na akili hata kidogo basi.
unamfuatilia erthrocyte lakni au umejisikia kuropoka tu??
Eti kuweni na akili ata kidogo; wewe unaakili??, yani darasa la saba halafu unavimba eti unauelewa😐
 
Kati ya watu wanaoishi kwa hasira kutokana na siasa za chadema, ni mleta mada
 
Nukuu ya uongo mkubwa.
 
Hii kodi ilikuwepo tunaita Government Leavy na kila Mtalii akilala usiku mmoja analipia USDollar 1.5 sasa sijui hawa viumbe wamepandisha tena au wameshusha kwa ajili ya kuvutia Watalii?
 
Hivi dhana ya kudhani watalii wana hela nyingi sana tutaacha lini?? Wengine wanapenda kutembea na kujifunza au kupumzika na sio kua wana hela sana......serekani inaturudisha kwenye fikra kua mzungu yeyote ana hela sana
 
Kwa mwendo huo,tutegemee hata na wananchi kuja kulipia kile kitanda anachokilalia nyumbani kwake,kama kodi ya ardhi tunalipia kama wenye mahoteli,kama wao watalipia kitanda kwa nini mwananchi wa kawaida naye asilipie?
 
Ushawastua na itakuwa kubwa sana ili wapunguze watumiaji wa mitandao wanaomtusi na kumkejeli huyo anayejiita mwendawazimu πŸ˜‚πŸ˜‚
Nchi inaendeshwa tuu kama gari bovu, hakuna sheria wala taratibu
 
Reactions: BAK
Hiyo kodi ya kitanda itakuwa kwa watalii peke yao? Loji, Gesti hazitalipa? Mwenyeji akilala kwenye hoteli ya kitalii hatalipa? Au ni kodi inayoendana na vitanda ambavyo vipo kwenye hoteli na sio watu waliolalia vitanda hivyo?

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…