TRA yazindua kodi ya kitanda kutoka kwa Watalii

TRA yazindua kodi ya kitanda kutoka kwa Watalii

Hiyo kodi ya kitanda itakuwa kwa watalii peke yao? Loji, Gesti hazitalipa? Mwenyeji akilala kwenye hoteli ya kitalii hatalipa? Au ni kodi inayoendana na vitanda ambavyo vipo kwenye hoteli na sio watu waliolalia vitanda hivyo?

Amandla...
Watalii wa nje na wa ndani
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi dhana ya kudhani watalii wana hela nyingi sana tutaacha lini?? Wengine wanapenda kutembea na kujifunza au kupumzika na sio kua wana hela sana......serekani inaturudisha kwenye fikra kua mzungu yeyote ana hela sana
Mm naona kuna shida kubwa ndani ya serikali,siku watalii wakikimbia asilaumiwe mtu kuwa ndo anaichafua taswira ya nchi huko nje,maana kama kodi hiyo itatolewa na wenye mahoteli ,hapo tutegemee wamiliki wa hoteli pia kupandisha entry fee katika hoteli na pia na gharama nyingine kuwa juu lengo likiwa kufidia hiyo kodi,na hilo ikifanyika tutegemee watalii kupungua na kukimbilia nchi jirani kuliko na unafuu
 
Hizo kodi zote tunashindwaje kuipita sarafu ya Kenya?

Uchumi wa Kati wa kubambikiwa ndio uliopo 🇹🇿
 
Nahisi Kenya wanatupita mbali sana kwa mambo na sera ya utaliii,na ndo mana idadi ya wageni kule kwao kabla ya korona walikuwa wanatupiga fimbo,hivi vijikodi visivyokuwa na mbele wala nyuma vitapeperusha wageni.
Subiri uone
Hizo kodi zote tunashindwaje kuipita sarafu ya Kenya?

Uchumi wa Kati wa kubambikiwa ndio uliopo 🇹🇿
 
Pesa hakuna tutalipa hadi kodi ya kichwa awamu hii, ngoja tuisome figure
Juzi niliskia ya viwanja wadaiwa sugu vitauzwa
 
Imekaa poa sana hii!! Napendekeza watutengenezee kodi na sisi watalii wa ndani tunao talii kwenye maguest house!! Itasaidia sana kuongeza mapato ili tusitoke kwenye uchumi wa kati!! kati patamu jamani!! Wabuni mbwinu tusitoke hapo katikati!! Mitano tena ni shiiida!!
 
Wakianzisha na za magesti hakika tutaanza rasmi kuwa dona kantre!
 
Nahisi Kenya wanatupita mbali sana kwa mambo na sera ya utaliii,na ndo mana idadi ya wageni kule kwao kabla ya korona walikuwa wanatupiga fimbo,hivi vijikodi visivyokuwa na mbele wala nyuma vitapeperusha wageni.
Subiri uone
Hivi na wewe ulimpigia kura ya ndiyo anko Magu?

Soon mtaanza kulipa kodi ya makalio maana nayo ni kivutio kwa wanaume wakware 😁
 
Usishangae sana mkuu. Watu wana chuki, tena wana chuki hadi kwa wanaowapa ulinzi wanapokua wamelala.

Kuna dada wa bongomovie aliwahi sema kwenye media hana mama, akadadavua mamake alishakufa ilihali mamake mzazi yuko hai na anamsikiliza sembuse huyu

Dunia inaenda kasi sana hii
kumbe kuna wanaotoa ulinzi tunapolala?!

nilijua ni Mungu pekee
 
Wahenga walisema "Jogoo La Shamba Haliwiki Mjini " - mtu wa kijijini aletwapo mjini shida kubwa sana hutokea !

- Just imagine ndege 11 cash money ?? Kama ni Utalii, kwa nini hoteli zinageuzwa Hostel ?

- Ushamba ni Shida Ya Zama Zote Ndugu Watanzania !
 
Binafsi nafikiri tatizo sio kodi ya Kitanda, tatizo ni kuchukulia Tanzania kama kisiwa kuwa lazima watalii watakuja Tanzania bila kujua huko Duniani kuna vivutio gani
Kuna moja ya Kozi Nzuri sana inatolewa na chuo kimoja cha UK inaitwa World Tourism Geography. Kwa kusoma hiyo Kozi unapata fursa ya kujua vivutio vingi tena Unique vilivyopo kwenye Nchi tofauti tofauti Duniani hivyo kujua kuwa, sio kweli kuwa lazima mtalii aje hapa kwa gharama yoyote. Huu utaratibu wa kuongeza tozo za kila aina huku tukifikiri watalii wataongezeka nafikiri ifike wakati ufikiriwe upya
Soko linakoelekea ni kwa Watalii kufuata vivutio vizuri lakini vilivyo affordable; wale wenye uwezo wa kulipa gharama za juu sio wengi hivyo ifike mahali tu target medium market & high marketi kwani tukiishia ku target high market pekee hatutafika mbali kwa kuwa ni wachache
Ifike mahali tufikiria faida za Utalii kwa upana yaani "Trickle down Effect" yaani tangu mgini afike uwanja wa ndege hadi siku anapanda ndege na kurudi kwao
 
Mm naona kuna shida kubwa ndani ya serikali,siku watalii wakikimbia asilaumiwe mtu kuwa ndo anaichafua taswira ya nchi huko nje,maana kama kodi hiyo itatolewa na wenye mahoteli ,hapo tutegemee wamiliki wa hoteli pia kupandisha entry fee katika hoteli na pia na gharama nyingine kuwa juu lengo likiwa kufidia hiyo kodi,na hilo ikifanyika tutegemee watalii kupungua na kukimbilia nchi jirani kuliko na unafuu
Umenena vyema mkuu unaweza kupunguza kodi ukasababisha kuongeza idadi ya watalii hivyo mapato ya serekali kupanda maradufu
 
Binafsi nafikiri tatizo sio kodi ya Kitanda, tatizo ni kuchukulia Tanzania kama kisiwa kuwa lazima watalii watakuja Tanzania bila kujua huko Duniani kuna vivutio gani
Kuna moja ya Kozi Nzuri sana inatolewa na chuo kimoja cha UK inaitwa World Tourism Geography. Kwa kusoma hiyo Kozi unapata fursa ya kujua vivutio vingi tena Unique vilivyopo kwenye Nchi tofauti tofauti Duniani hivyo kujua kuwa, sio kweli kuwa lazima mtalii aje hapa kwa gharama yoyote. Huu utaratibu wa kuongeza tozo za kila aina huku tukifikiri watalii wataongezeka nafikiri ifike wakati ufikiriwe upya
Soko linakoelekea ni kwa Watalii kufuata vivutio vizuri lakini vilivyo affordable; wale wenye uwezo wa kulipa gharama za juu sio wengi hivyo ifike mahali tu target medium market & high marketi kwani tukiishia ku target high market pekee hatutafika mbali kwa kuwa ni wachache
Ifike mahali tufikiria faida za Utalii kwa upana yaani "Trickle down Effect",
Faida anazo acha tangu afike uwanja wa ndege hadi siku anapanda ndege na kurudi kwao
meongea point ila wahusika sizan kama wanakijua ulicho kisema.
 
Kamishna Mkuu wa TRA Dkt. Edwin Mhede amepokea orodha ya huduma za malazi iliyoboreshwa 2020 kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki ili kuiwezesha TRA kukusanya tozo ya Kitanda Siku kutoka kwa Watalii wanaotumia huduma za malazi.

View attachment 1641829

Hii ni katika harakati za kuongeza mapato
Kuna kitu kinaitwa 'customer perception of value' is it competitively harmonized ?
 
Kodi huwa zina malengo yake mfano kuongeza kodi kwa bidhaa toka nje ni kuizuia au kupunguza idadi ya kuingia, mnaonaje kama tukiweka kodi ya kukata gogo kwanza tutaongeza mapato na pia atapunguza uchafuzi wa mazingira
 
Back
Top Bottom