TRA yotoa ufafanuzi wa madai ya kutengeneza mfumo wa kuingiza mizigo nchini usio halali

Sasa wahusika ndio wamekanusha hilo halipo, Kwahiyo mlalamikaji na athibitishe
Hilo sio swala la kukanusha ni swala la kuchunguza.Kwasababu mhusika kawapa taarifa ya wazi kua kuna magendo yanafanywa kwenye ofisi yenu walichotakiwa kufanya ni kuchukua hatua kufwatilia sio kukanusha.Au nini maana ya magendo?.Magendo maana yake jambo limefanywa kwa siri nje ya utaratibu.kupata ukweli wake lazima ulifwatilie nje ya mfumo ulionao ndo utalipata.Walitakiwa waombe ushirikiano kwa huyo mfanyabiasha vinginevyo yatakua nimambo yao wao kwa wao wanaficha ficha tu.
 
Wamnase alipe Kodi huyo hakuna blaa blaa
 
Saw Sawa nimekupata vyema, ila si angeripoti kwa vyombo vyenye mamlaka ya kuchunguza? Hivi unawaambia tra wajichunguze kweli watafanya? Nadhani ameripoti sehemu isiyo sahihi
 
Means TRA maofisa bandarini wameusajili huo mzigo katika mfumo mwingine wa kipigaji walioutengeneza ili pesa ziende kwenye mifuko yao ndio maana kwenye mfumo wa TANCIS hauonekani...HUYO JAMAA SIO MJINGA KUSEMA KUNA MFUMO MWINGINE.....RIP Magufuli ulipaweza sana pale bandarini na watu walishika adabu maana saiv TRA na wafanyabiashara huko wanaingiza makontena na hayalipiwi ushuru.
 
Hili ni bomu ambalo inatakiwa kitu cha kwanza Wazziri wa Fedha, Makamishnana, manaibu Kamishna, vyombo vya usalama vyote waliopo TRA wanaohusiana na bandarin, wote wasimamishwe kazi wawekwe wengine haraka sana, uchunguzi wa kina ufanyike.


Hawa ndiyo wanaochelewessha maendeleo.

Huyo Mfanyabiashara apewe ulinzi wa saa 24, watamfinya.

Wameshaonesha wanataka kumgeuzia kibao. Barua ya kujibiwa ndani ya muda mchache kwanini ikae miezi kujibiwa?

Tena inaonesha imejibiwa ile "ficha kombe mwanaharamu apite).


Mama aSamia, nnauhakika hili limeshafika mezani kwako.
 
TRA ni mtuhumiwa halafu amejipa mamlaka ya kushughulikia kosa. Hapo ndo unaona kuna mifumo ya kihuni mingi kwenye serikali hii. TRA wachunguzwe siyo wao ndo wachunguze.
 
Wakati mwingine ndiomana nina support bandari apewe mwarabu.

Mtanzania hajawahi kuacha rushwa hata moto wa milele uwe unawaka live hapa duniani watu hawataacha kula rushwa.
Bandari, Mahakama, Ardhi, Police huko kote mlungula unatembea vibaya sana.
Siyo wakati mwingine, si watu kama hawa waliopo sasa ndiyo wanazuwia yasifanyike.

Unafikiri kina nani, wote wanaopinga wana malahi yao andarini kwa namna moja au nyingine.

Hata kina Mwigulu mimi sina imani nao kabisa, vipi wewe waziri wa fedha usiyajuwe haya madudu wanayofanyiwa walipa kodi wako siku zote?

Ndiyo maana Mwigulu saakata la wafanyabiashara wa kariakoo alikuwa ana wasiwasi mpaka anajilamba ulimi, mate yalimkauka mdomini. Huyu aende tu.
 
TRA na Police hawana tofauti, wewe umetuhumiwa halafu wenyewe unajichunguza na kukanusha, why kusiwe na kamati huru ya kuchunguza?
 
Waziri wa uchukuzi ni Mzanzibar, KM wa uchukuzi ni Mzanzibar, CEO wa bandari ni mzanzibar(wote dini moja), Mwigulu anahusikaje kwenye bandari? upigaji ni mfumo ovu wa serikali nzima, kuna kuwaje na wizi na wakati hapo bandarini kuna polisi na TISS?
 
Tanzania kuna tatizo kubwa la kimfumo kutoka juu, serikalini kumejaa majangili ambayo yanafunga tai kila siku na kubebwa na V8
 
Ngoja nichanganue hili sakata kwa nilivyoelewa mimi.

Mfanyabiashara Ameingiza bidhaa zake nchini kupitia kampuni ya tosh cargo

Tosh cargo amesafirisha na kukamilisha taratibu zote za forodha na kukabishi mzigo kwa mteja wake.

Shida inaanzia hapo kwenye (Amesafirisha na kukamilisha taratibu zote za forodha)

Wakati mfanyabiashara anapelekea mzigo wake huko unapotakiwa kwenda gari ikapata ajali na kusababisha uharibifu na upotevu wa mali.

Kwakua mfanyabiashara alikua na bima, akaanza mchakato kufatilia ili apate fidia ya mali yake iliyoharibiwa na tukio la ajali.

Kampuni ya bima inawajibika kumlipa mteja wake, lakini kabla hawajamlipa lazima wapate nyaraka zote muhimu kuhusu mali zilizopotea, ikiwa ni pamoja na nyaraka zote halali za kikodi na mengineyo ili wapate uhakika wa thamani na uhalali wa wanachoenda kulipa.

Sakata linaanzia hapa kwenye nyaraka.

TRA hawatambui mali ya mlalamikaji, kwanini hawaitambui na hawajaiona kwenye mfumo?

Kuna mawili hapa;

1. Tosh cargo wameingiza mzigo kama mali yao, hivyo mteja mwenye mzigo hatambuliki na mfumo mzima wa TRA.

2. Rejea namba moja 😂, kama mfumo haukusomi basi unamsoma aliekamilisha clearance ya mzigo.


Kama Nyaraka za TRA hazikutambui kampuni ya Bima itakufidia vipi na umeshindwa kutoa vielelezo vya uhalali wa mali iliyoharibika, vipi kama umekula njama na mtu baki utumie mgongo wa mali yake iliyoharibika kujipatia bima kwa njia ya udanganyifu?


Swali jingine la msingi kwa mfanyabiashara.
Asijekua anataka huruma ilhali nayeye anajua fika changamoto ambazo zingejitokeza.

Je kabla ya kupata matatizo yote ya ajali n.k, aliridhika na nyaraka zote alizokabidhiwa baada ya kupewa mizigo yake, au akili imekuja kukaa sawa baada ya matatizo?
 
Hahaa good analysis mkuu.
Sababu unaponunua bidhaa nje lazima BL(documents) zitangulie kwanza kabla ya mzigo means unajua mnunuzi na gharama. Sasa kama itakuwa kama ilivyosema hapo juu maana yake alijua tangu awali.

Au basi mzigo umetoka kwa arrangements za " nje ya uwanja" japo documents ni za kwake kweli ndomana TRA hawatambui. Hapo kuna mengi mkuu.
 
Huenda waliokuwa wakichunguza ndio hao waliotengeneza huo mfumo.
Nyie TRA kuaminika ni ngumu sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…