TRA yotoa ufafanuzi wa madai ya kutengeneza mfumo wa kuingiza mizigo nchini usio halali

TRA yotoa ufafanuzi wa madai ya kutengeneza mfumo wa kuingiza mizigo nchini usio halali

Hili ni bomu ambalo inatakiwa kitu cha kwanza Wazziri wa Fedha, Makamishnana, manaibu Kamishna, vyombo vya usalama vyote waliopo TRA wanaohusiana na bandarin, wote wasimamishwe kazi wawekwe wengine haraka sana, uchunguzi wa kina ufanyike.

Hawa ndiyo wanaochelewessha maendeleo.

Huyo Mfanyabiashara apewe ulinzi wa saa 24, watamfinya.

Wameshaonesha wanataka kumgeuzia kibao. Barua ya kujibiwa ndani ya muda mchache kwanini ikae miezi kujibiwa?

Tena inaonesha imejibiwa ile "ficha kombe mwanaharamu apite).

Mama aSamia, nnauhakika hili limeshafika mezani kwako.
Kama siyo wewe vile 😄😄😄
 
Jambazi anakubali kiurahisi?wewe unadhani kule Polisi kwanini kuna vyumba vya kubananishia Majambazi ikiwemo kubanwa korodani!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Sasa badala ya kwenda kulalamikia kwenye sehemu husika, yeye ameenda kulalamikia kwa hao hao tra?
Yaani jambazi ajichunguze mwenyewe?
Ilitakiwa aende takukuru au polisi kushatakia sio tra
Nadhani umeelewa
 
Tatizo lipo kwa mfanyabiashra (kutaka mtereremko kwenye kodi) na hiyo logistic company pamoja na ignorance.
 
Ngoja nichanganue hili sakata kwa nilivyoelewa mimi.

Mfanyabiashara Ameingiza bidhaa zake nchini kupitia kampuni ya tosh cargo

Tosh cargo amesafirisha na kukamilisha taratibu zote za forodha na kukabishi mzigo kwa mteja wake.

Shida inaanzia hapo kwenye (Amesafirisha na kukamilisha taratibu zote za forodha)

Wakati mfanyabiashara anapelekea mzigo wake huko unapotakiwa kwenda gari ikapata ajali na kusababisha uharibifu na upotevu wa mali.

Kwakua mfanyabiashara alikua na bima, akaanza mchakato kufatilia ili apate fidia ya mali yake iliyoharibiwa na tukio la ajali.

Kampuni ya bima inawajibika kumlipa mteja wake, lakini kabla hawajamlipa lazima wapate nyaraka zote muhimu kuhusu mali zilizopotea, ikiwa ni pamoja na nyaraka zote halali za kikodi na mengineyo ili wapate uhakika wa thamani na uhalali wa wanachoenda kulipa.

Sakata linaanzia hapa kwenye nyaraka.

TRA hawatambui mali ya mlalamikaji, kwanini hawaitambui na hawajaiona kwenye mfumo?

Kuna mawili hapa;

1. Tosh cargo wameingiza mzigo kama mali yao, hivyo mteja mwenye mzigo hatambuliki na mfumo mzima wa TRA.

2. Rejea namba moja [emoji23], kama mfumo haukusomi basi unamsoma aliekamilisha clearance ya mzigo.

Kama Nyaraka za TRA hazikutambui kampuni ya Bima itakufidia vipi na umeshindwa kutoa vielelezo vya uhalali wa mali iliyoharibika, vipi kama umekula njama na mtu baki utumie mgongo wa mali yake iliyoharibika kujipatia bima kwa njia ya udanganyifu?

Swali jingine la msingi kwa mfanyabiashara.
Asijekua anataka huruma ilhali nayeye anajua fika changamoto ambazo zingejitokeza.

Je kabla ya kupata matatizo yote ya ajali n.k, aliridhika na nyaraka zote alizokabidhiwa baada ya kupewa mizigo yake, au akili imekuja kukaa sawa baada ya matatizo?

Mizigo ya loose cargo nikuwa mizigo ya watu tofauti inakusanywa kwenye kontena moja na kampuni ya usafirishaji inasafirisha kama mali yao.Ndiyo maana unachajiwa kwa CBM na unalipa kwenye kampuni ya usafirishaji bila kwenda mwenyewe forodha.

I think baada ya TRA kupata hili zengwe la huyu jamaa wakaja na mfumo wa kila mtu alipie forodha,ambapo kwenye mgomo wa Kkoo kipindi kile watu waliupinga huu utaratibu.Maana ilikuwa let’s say kontena ina mizigo ya watu 100,kila mmoja inatakiwa akalipie ushuru forodha.

Kitu ambacho hawakujua ndio kama sasa hivi inakuwa ngumu bima kulipa bila nyaraka za uingizaji mzigo.TRA walilijua hili ila kwa kuwa walikuwa wananeemeka bila kesi wakapuuzia.
Kuna mtu atatolewa mbuzi wa kafara kwenye hili.
 
Hilo sio swala la kukanusha ni swala la kuchunguza.Kwasababu mhusika kawapa taarifa ya wazi kua kuna magendo yanafanywa kwenye ofisi yenu walichotakiwa kufanya ni kuchukua hatua kufwatilia sio kukanusha.Au nini maana ya magendo?.Magendo maana yake jambo limefanywa kwa siri nje ya utaratibu.kupata ukweli wake lazima ulifwatilie nje ya mfumo ulionao ndo utalipata.Walitakiwa waombe ushirikiano kwa huyo mfanyabiasha vinginevyo yatakua nimambo yao wao kwa wao wanaficha ficha tu.
Naimani pasi na shaka kuwa hilo genge la wezi linaongozwa na huyo kamishna. Je, anaweza kujichunguza? Je mtu wa chini yake anaweza kumchunguza? Jibu ni hapana. Ndio maana katoa hiyo barua ya vitisho vya wazi kwa muhanga.
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu malalamiko ya Bw. Emmanuel Gadi kuwa, TRA imetengeneza mfumo wa kuingiza mizigo nchini nje ya mfumo halali wa Serikali kinyume na Sheria ya Forodha.

Tunapenda kuufahamisha umma na jamii kwa ujumla kuwa, Mamlaka haina mfumo wowote mwingine inaouendesha wa kuingiza mizigo nchini nje ya mfumo wa Forodha wa TANCIS ambao unatumika kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACCMA).

Bw. Emmanuel Gadi alifikisha malalamiko yake kwa njia ya barua tarehe 27 Februari, 2023 akidai kupewa uthibitisho na TRA wa kuingiza mzigo wa vifurushi 471 vya “Toner Cartridges’’ kupitia kampuni ya Tosh Logistics Ltd. TRA ilifanya uchunguzi wa kutosha na kuthibitisha kwamba, hapakuwa na mzigo wowote ulioingizwa nchini kwa jina la Wintech Tanzania Ltd wa vifurushi 471 vya “Toner Cartridges” kupitia kadhia yenye namba TZDL-22-1382193 ya tarehe 18 Agosti 2022 kama anavyodai.

Hivyo, TRA ilimjibu mhusika kupitia barua yenye kumbukumbu namba CF 8/92/01 ya tarehe 25 Julai 2023 ikimjulisha kuwa, kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa “House Bill of Lading” na kutoonekana kwa mzigo huo kwenye kadhia iliyowasilishwa na kampuni ya Tosh Logistics Ltd, TRA isingeweza kuthibitisha kuingizwa kwa mzigo huo nchini.

Kupitia taarifa yake aliyoitoa kwenye vyombo vya habari tumebaini kuwepo viashiria vya ukwepaji kodi kwani ni dhahiri kuwa mzigo huu uliingizwa kwa njia za magendo. TRA inamtaka mlalamikaji kuwasilisha nyaraka na uthibitisho wa kampuni yake kuingiza mzigo huo nchini mara moja ili hatua stahiki zichukuliwe.

===========
Video ya Mfanyabiashara akiituhumu TRA
1. Barua ya TRA inapingana na kutofautiana kabisa na maelezo ya huyu bwana. Huyu anaeleza hiki, TRA wanafafanua kitu kingine. Nafikiri ni ktk kutaka kupotezea tu.

2. Syndicate ya ufisadi serikalini na kwenye taasisi zake ni wa kimfumo unaohusisha watumishi wadogo kabisa huku chini hadi wale wakubwa juu wakiwemo mawaziri, Makatibu wakuu, wakuu wa taasisi na mashirika ya umma.

Katika mazingira haya, nani atamfunga mwenzake?

3. Nchi ikifikia hatua hii ya uovu kiasi cha wenye dhamana ya uongozi na utawala wa kufanya maamuzi kuwa corrupted kiasi hiki, basi wa kubadilisha hali hii hawawezi kuwa hawahawa walio ktk mfuno huu. Ni lazima force nyingine itoke nje ya wao na kusukuma uchafu wote nje
 
Hili ni bomu ambalo inatakiwa kitu cha kwanza Wazziri wa Fedha, Makamishnana, manaibu Kamishna, vyombo vya usalama vyote waliopo TRA wanaohusiana na bandarin, wote wasimamishwe kazi wawekwe wengine haraka sana, uchunguzi wa kina ufanyike.

Hawa ndiyo wanaochelewessha maendeleo.

Huyo Mfanyabiashara apewe ulinzi wa saa 24, watamfinya.

Wameshaonesha wanataka kumgeuzia kibao. Barua ya kujibiwa ndani ya muda mchache kwanini ikae miezi kujibiwa?

Tena inaonesha imejibiwa ile "ficha kombe mwanaharamu apite).

Mama aSamia, nnauhakika hili limeshafika mezani kwako.
Natamani huyo mama Samia angekuwa nao huo uwezo wa kulishughulikia.
 
Waziri wa uchukuzi ni Mzanzibar, KM wa uchukuzi ni Mzanzibar, CEO wa bandari ni mzanzibar(wote dini moja), Mwigulu anahusikaje kwenye bandari? upigaji ni mfumo ovu wa serikali nzima, kuna kuwaje na wizi na wakati hapo bandarini kuna polisi na TISS?

Kwani mzigo haujafika?
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu malalamiko ya Bw. Emmanuel Gadi kuwa, TRA imetengeneza mfumo wa kuingiza mizigo nchini nje ya mfumo halali wa Serikali kinyume na Sheria ya Forodha.

Tunapenda kuufahamisha umma na jamii kwa ujumla kuwa, Mamlaka haina mfumo wowote mwingine inaouendesha wa kuingiza mizigo nchini nje ya mfumo wa Forodha wa TANCIS ambao unatumika kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACCMA).

Bw. Emmanuel Gadi alifikisha malalamiko yake kwa njia ya barua tarehe 27 Februari, 2023 akidai kupewa uthibitisho na TRA wa kuingiza mzigo wa vifurushi 471 vya “Toner Cartridges’’ kupitia kampuni ya Tosh Logistics Ltd. TRA ilifanya uchunguzi wa kutosha na kuthibitisha kwamba, hapakuwa na mzigo wowote ulioingizwa nchini kwa jina la Wintech Tanzania Ltd wa vifurushi 471 vya “Toner Cartridges” kupitia kadhia yenye namba TZDL-22-1382193 ya tarehe 18 Agosti 2022 kama anavyodai.

Hivyo, TRA ilimjibu mhusika kupitia barua yenye kumbukumbu namba CF 8/92/01 ya tarehe 25 Julai 2023 ikimjulisha kuwa, kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa “House Bill of Lading” na kutoonekana kwa mzigo huo kwenye kadhia iliyowasilishwa na kampuni ya Tosh Logistics Ltd, TRA isingeweza kuthibitisha kuingizwa kwa mzigo huo nchini.

Kupitia taarifa yake aliyoitoa kwenye vyombo vya habari tumebaini kuwepo viashiria vya ukwepaji kodi kwani ni dhahiri kuwa mzigo huu uliingizwa kwa njia za magendo. TRA inamtaka mlalamikaji kuwasilisha nyaraka na uthibitisho wa kampuni yake kuingiza mzigo huo nchini mara moja ili hatua stahiki zichukuliwe.

===========
Video ya Mfanyabiashara akiituhumu TRA
Nashawishika kumuamini 100% ndg Emanuel na sio TRA.
 
Back
Top Bottom