Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Tukio linalodaiwa kutokea maeneo ya Mwenge, Dar es Salaam, ambapo askari wa usalama barabarani anadaiwa kuchomoa ufunguo wa gari la dereva baada ya kutokea mabishano, linaibua maswali muhimu ya kisheria na kiutendaji.
Je, askari wa usalama barabarani ana mamlaka ya kisheria kuchomoa ufunguo wa gari la dereva aliyekaidi maelekezo? Ikiwa mamlaka hayo yapo, yanatolewa chini ya kifungu gani cha sheria au kanuni? Na kama hayapo, je, hatua hiyo haikuwa ni kuvuka mipaka ya mamlaka ya askari?
Polisi wamesema wanamshikilia Conrad Kayoza kwa KUMSHAMBULIA ASKARI wakati akitekeleza majukumu yake.
Sasa, kwa mujibu wa Kifungu cha 243(b) cha Penal Code, Sura ya 16, mtu anayemshambulia, kumpinga au kumzuia kwa makusudi askari polisi anayetekeleza wajibu wake anaweza kutiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka mitano.
Hata hivyo, mazingira ya tukio ni muhimu kisheria. Ili kifungu hicho kitumike, lazima ithibitike kwamba askari alikuwa akitekeleza wajibu wake kihalali. Ikiwa shambulio limesababisha majeraha au limehusisha makosa mengine, mashitaka na adhabu vinaweza pia kutegemea makosa mengine yanayothibitishwa.