Trafiki ni mradi wa mapato Serikalini na wakubwa fulani

Sawasawa
 
Kama wanauliza mpaka mikwaruzo ya rangi, wewe ni nani uendeshe gari jipya kila siku
 

Ninakazia:

Kwa rushwa ilivyotamalaki, PCCB na wengine wa hivyo wana umuhimu gani kuendelea kuwapo?
 
Hapa Trafiki waboreshewe maslahi, wapewe training za mara kwa mara,wapewe vitendea kazi bora na waongezwe barabarani.
Training gani?
Walipewaje kazi kama hawako trained?
Vitendea kazi gani kama wanapiga vita matumizi ya ICT? Mfano mdogo tu polisi wa cyber crime wanakamata simu za wizi kisha wanajimilikisha wao
 
Hawa jamaa ni Taasis ya kuzuia na kupambana na rushwa ila hiyo kazi ya kuzuia sidhani kama walishawahi ifanya maisha yao yote.

Labda kupambana tena ni mpaka wapewe maelekezo na wakubwa nendeni mkacchumguze ndio unakuta watu wanakamatwa.
 
Unaowaongelea kwa bashasha ni hawa?



Labda kama u mmoja wao?

Wana tija wapi hawa?
 
Traffic wanahesabu kama dereva wa daladala au uber, anapangiwa apeleke kiadi fulani kila siku, so kazi ni kwake, ahakikishe anapata pesa(hesabu) ya bosi, anapata poshoo yake na pesa ya serikali(vyeti/faini)
 
Ni wao, nimefanya utafiti, tangu Kinana amemwaga sumu ukipita barabarani utaona wameinamia simu zao wako busy kujibu mapigo humu na hawalali
Kazi ya Traffic ni kusimamia sheria za Barabarani ili kudumisha usalama kwa watumiaji wote wa barabara.

Anaposimamisha gari ni sehemu ya kazi kuifanyia ukaguzi wa gari lenyewe, dereva na hata abiria waliomo kwenye gari.

Fanya kosa uone kama hawata kusimamisha.
 
Trafik wa siku hizi hawakagui matatizo ya gari.Wakikusimamisha wanakimbilia kukuomba leseni yako ukishampa ndo shida inapoanzia.ili akurudishie lazima wewe ndo uwe mpole,Ukijitetea kwamba huna kosa wanakua wakali kua unaleta ujeuri na mikwara yakutosha.Sasa hili kuepusha kelele na kuokoa muda wako wakati mwingine mtu unaona uwe mpole tu ili ukafanye mishe zako.
 

Wewe hujui kuwa kazi halali zikiwamo hizi za hawa ndugu zimekuwa zikitumika kama kichaka cha kijipatia rushwa?
 
Hajasema traffic police waondolewe barabarani, ila idadi na kusimamishwa kwa magari ndiyo kero.
Kazi ya askari wa usalama barabarani ni kuongeza ufanisi kwa dereva na siyo kupunguza.
Askari wasaidie wakati wa breakdown, wafuatilie wanaoendesha vibaya, taarifa za wahalifu wanaokimbia na yanayofanana na hayo. Siyo kusimamisha magari kwa sababu ya kitu kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…