Trafiki ni mradi wa mapato Serikalini na wakubwa fulani

Trafiki ni mradi wa mapato Serikalini na wakubwa fulani

Ila mkiendelea kufa kwa maajali msije kuloloma humu.
Ungekuwa ni dereva uliyekamilika, na unaye safiri na gari kwenda maeneo tofauti tofauti, basi ungekubalina na hoja za wengi humu juu ya hao trafiki kuwepo barabarani kwa ajili ya rushwa tu.
 
Ungekuwa ni dereva uliyekamilika, na unaye safiri na gari kwenda maeneo tofauti tofauti, basi ungekubalina na hoja za wengi humu juu ya hao trafiki kuwepo barabarani kwa ajili ya rushwa tu.
Inaondoa hoja yangu?
 
Inaondoa hoja yangu?
Ndiyo, inaondoa! Kwa sababu dereva yeyote yule aliyekamilika, wala hahitaji uwepo wa hao wala rushwa barabarani.

Na kama ulikuwa hufahamu, ni kwamba trafiki wengi huvizia wenye magari kwenye vibao vya 50/kph!

Maeneo mengine vibao hivyo huondolewa kwa makusudi ili kuwakamata madereva kwa uonevu! Lakini maeneo hayo kuna wakati yanakuwa hayana watu au hatari yoyote ile mbele! Sasa kwa nini ulazimishwe kuendesha speed ya 50/kph?

Na wakati huo huo mabasi makubwa kwa sababu ya kufahamiana na hao wala rushwa, hupita maeneo ya 50/kph kwa speed kubwa! Na hawakamatwi! Na hata wanapokamatwa, basi humalizana kimya kimya!
 
Siku hizi hata hawa FFU nao wanasimamisha magari na pikipiki kukagua na kuchukua rushwa.
Ndo hawa wanaoitwa tigo? bila shaka bodaboda wanaijua shughuli yao........wananchi hawana uhuru wa kufanya shughuli zao za usafiri na usafirishaji kisa trafiki wametanda kila kona kusubiri kukusanya rushwa ambayo wanaita pesa ya kiwi, haya mambo yanaondoa ustaarabu wa kijamii......
 
Ndugu yangu sijui unaingea watu Gani. Hujaingia kwenye 18 zao. Ndo utawajua tu.. nilishawahi kua na vyote lkn walikula 5000. Lkn kumbuka wapo wengi sana barabarani na wanapoteza mda sana. make kila baada ya 1km umesimamishwa hasa mjini.

Chukulia unatokea buhongwa Hadi unatokea Kisesa umesimamishwa zaidi ya mara 7 Hadi 10 ndani ya 20km huoni ni kupotezeana mda

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
Huyo anaongea kishujaa tu sababu aidha yeye naye ni trafiki au ofisa mkubwa wa serikali. Mtu wa kawaida kitendo cha naomba leseni yako ukamkabidhi tu jua kinachofuata ni kubambikiwa kosa tu na aidha utachagua utoe elf 5 mmalizane au akulime 3O!
 
Hivi wakuu ukijitahidi gari yako iwe safi,kwa maana spidi ya kawaida,ukiwa umevaa mkanda,bima umelipa na tira inasoma,tairi zipo vizuri na spea yake,nenda kwa usalama umepeleka gari na imekaguliwa na wao vizuri tu.
Taa zote zipo safi,waipa na maji yapo poa,hujazidisha abiria,hujavaa sendo,fire extinguisher ipo vizuri,na unajua kuitumia.
Huhjaovateki sehem isiyoruhusiwa,kwenye zebra umepisha watu wapite,umepaki sehem sahihi,upo kwenye line yako.
Hivi hawa jamaa wanakulaje hela yako?????
Tekeleza yote, bado utashikwa kwa kuzushiwa kosa. Kumbuka mwana mbuzi aliliwa na mbwa mwitu kwa tuhuma za uchafuzi wa maji ulio fanywa na wazazi wake kabla hajazaliwa.
 
Siku hizi hata hawa FFU nao wanasimamisha magari na pikipiki kukagua na kuchukua rushwa.
Huu ugonjwa wa serikali kulitumia jeshi la polisi kukusanya mapato unaliangamiza kimaadili jeshi zima la polisi.
Kila mtu angependa kukusanya mapato ya serikali na ya kwake binafsi.
Ukicheki vizuri wengi wanaosimamisha magari /pikipiki/bajaj hawana hata vitendea kazi vya kukusanya mapato, ila mapato ya kwao wenyewe
 
Wanatumwa na wakubwa zao
Kuna hesabu lazima wawapeleke
Huo ndiyo ukweli

Ova
 
huu uzi umejaa watu wasio na magari,na hata traffic hawamo humu.

huko barabarani uhusiano wa dereva na traffic polisi hauharibiwi na rushwa,bali fine ambazo hutumika kumtunza hata huyo mwindaji haramu.

inapokuwa ni rushwa,basi si traffic wala dereva au boss anayelalamika,ila tu inapofanya kazi mashine ya malipo,hapo ndipo kelele zilipo.

tumsaidie kinana kufanya siasa kwa sasa umri unamuacha.
 
Hueleweki, maana hata abiria wewe hujui kuwa wanakereka!
 
Hivi wakuu ukijitahidi gari yako iwe safi,kwa maana spidi ya kawaida,ukiwa umevaa mkanda,bima umelipa na tira inasoma,tairi zipo vizuri na spea yake,nenda kwa usalama umepeleka gari na imekaguliwa na wao vizuri tu.
Taa zote zipo safi,waipa na maji yapo poa,hujazidisha abiria,hujavaa sendo,fire extinguisher ipo vizuri,na unajua kuitumia.
Huhjaovateki sehem isiyoruhusiwa,kwenye zebra umepisha watu wapite,umepaki sehem sahihi,upo kwenye line yako.
Hivi hawa jamaa wanakulaje hela yako?????
Hivi vyote unaweza kuvitimiza
 
Back
Top Bottom