Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema askari wawili wa Kikosi cha Usalama Barabarani walioonekana kwenye video wakifanya vitendo ambavyo ni kinyume cha maadili ya Jeshi la Polisi kwa maana ya kupokea rushwa, tayari wamekamatwa na wako mahabusu na hatua za kisheria zitafuata dhidi yao.