Trafiki wawili wakamatwa baada ya kunaswa kwenye video wakipokea Rushwa hadharani

Trafiki wawili wakamatwa baada ya kunaswa kwenye video wakipokea Rushwa hadharani

Aisee hii tabia ya kurekodi watu wanapokea elf mbili mnaita rushwa ni hatari sana

Hivi mnajua Rushwa kweli?

Wanaokula rushwa hata wanaonekana kwa macho?

Eyes on small coins,

Mtasema mnaanzia hapa, lakini i can tell you hii mediocrity ni ya level ndogo sana kama taifa
 
Hakuna trafiki asiyepokea rushwa, wote wakubwa na wadogo wanapokea na kula, kuna huyu dada anayekusanya 2000 kila gari hapo China Plaza, kituo cha Sekondari ya Benjamini Mkapa katikati ya Kariakoo na Karume, karibu na kiwanda cha bia Brewaries kila jumapili, tukutane hapo jumapili tushuhudie pamoja.
 
Wanakula kwa urefu wa kamba zao, hizi sio rushwa za maana, tizameni wajuu wale wabadhirifu haswaa, wale wanatokea kwenye ripoti ya CAG.

Kuna mtu aliisababishia serikali hasara ya bilioni ngapi sijui akapigwa faini ya milioni 100 🤣😂
 
Kwamba hilo halijulikani hadi waonekane kwenye video ndio washughulikiwe?

Kama kukamatwa mbona watakamatwa wengi sana? Maana binafsi nikiamua kuwarekodi kila siku lazima niwaone kama vituo vitano hadi nilidhani ni mfumo mpya ambao ni rasmi.
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema askari wawili wa Kikosi cha Usalama Barabarani walioonekana kwenye video wakifanya vitendo ambavyo ni kinyume cha maadili ya Jeshi la Polisi kwa maana ya kupokea rushwa, tayari wamekamatwa na wako mahabusu na hatua za kisheria zitafuata dhidi yao.
Pia, Soma: Hapa ni wapi? Trafiki wadakwa kwenye video wakichukua Rushwa mara kadhaa
wawasamehe tu hiyo kazi yao ngumu sana imagine from asubh upo umesimama hadi saa mbili saa nne usiku kwa dar es salaam..
Ni ngumu sana na kama binadamu hawajakamilika pia. Wawape onyo tu.
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema askari wawili wa Kikosi cha Usalama Barabarani walioonekana kwenye video wakifanya vitendo ambavyo ni kinyume cha maadili ya Jeshi la Polisi kwa maana ya kupokea rushwa, tayari wamekamatwa na wako mahabusu na hatua za kisheria zitafuata dhidi yao.
Pia, Soma: Hapa ni wapi? Trafiki wadakwa kwenye video wakichukua Rushwa mara kadhaa
Taarifa ya msemaji wa jeshi la polisi Iko wapi?
Hao askari majina yao Yako wapi?
Lini wanapelekwa mahakamani kuhukumiwa,kwani ushahidi WA video umekamilika.
 
Back
Top Bottom