Trafiki wawili wakamatwa baada ya kunaswa kwenye video wakipokea Rushwa hadharani

Trafiki wawili wakamatwa baada ya kunaswa kwenye video wakipokea Rushwa hadharani

Traffic wa Dar kiboko,wanabeba hadi mikoba!😁.

BTW: Hivi huu ni ushahidi usiotia shaka unaoweza kumtia hatiani mtu kuwa alikuwa anapokea rushwa kunako mahakamani?

Yasiwe yaleyale ya DC Bomboko na kesi ya makahaba Ubungo,mashahidi wa Jamhuri wakaishia kung'ata kucha tu.
 
Hawa wamekamatwa Kwa sababu wameonekana lakini hii ipo majiji yote na Huwa inafanyika Kila siku.Mimi nimeiona sana hapa Dar lakini unaamua kupotezea tu.kila daladala 2000, muda mwingine Hadi 5000.
Ni uzalendo ukiwapiga picha au kuchukua video,kuliko kukaa kimya,ulinzi wa raia na nchi,si wa askari tu,unaanza na wewe mwananchi.
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema askari wawili wa Kikosi cha Usalama Barabarani walioonekana kwenye video wakifanya vitendo ambavyo ni kinyume cha maadili ya Jeshi la Polisi kwa maana ya kupokea rushwa, tayari wamekamatwa na wako mahabusu na hatua za kisheria zitafuata dhidi yao.
Pia, Soma: Hapa ni wapi? Trafiki wadakwa kwenye video wakichukua Rushwa mara kadhaa
Mambo ya aibu kabisa. Ila hawa mahakamani watatoboa, nani ana uhakika/ushahidi kuwa walichokuwa wanapewa ni pesa!? Japo sote tunajua wamepokea pesa ila kisheria wanaweza kukwepa huo mtego.
 
Ni taarifa za maigizo au taarifa za kutengenezwa kama kawaida yao.

Hao Askari Polisi anaodai kwamba wamekamatwa na wako mahabusu, Je, kwa nini hajataja Majina yao?? Why?
Watuhumiwa wengine huwa wanatajwa majina na kuanikwa hadharani ila hao watumishi wao majina hayatajwi na hatuwaoni!
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema askari wawili wa Kikosi cha Usalama Barabarani walioonekana kwenye video wakifanya vitendo ambavyo ni kinyume cha maadili ya Jeshi la Polisi kwa maana ya kupokea rushwa, tayari wamekamatwa na wako mahabusu na hatua za kisheria zitafuata dhidi yao.
Pia, Soma: Hapa ni wapi? Trafiki wadakwa kwenye video wakichukua Rushwa mara kadhaa
Nimewaonea huruma tu masikini ya mungu, hawa ni watoto wa maskini tu wamepata ajali kazini , ni wa kuwaonea huruma maana ajira zenyewe hakuna wakifukuzwa ndio tumewapoteza
 
Kama kweli wanataka kupunguza rushwa kwa hawa traffic basi iwe ni lazima mazingumzo ya kondakta na askari yawe mlangoni mwa daladala na abiria wakiona na kusikia mazungumzo. Siyo gari inakwenda kusimama mbele halafu konda anarudi nyuma kwa askari kumshikisha kitu kidogo.
Nusu ya hiyo pesa inarudi kituoni kilasiku wanaenda kugawana na wakubwa wao
 
dah sio sawa umewaanika wenzio ona sasa. kwan si ni madaladala hayo nayo yana makosa meng .
mchkua picha hukupaswa kuchkua video sio poa u akua kama hujaenda depo bwana
 
Kama kweli wanazuia na kupambana na rushwa wakawakamate na wanaokula mabilioni kwenye ripoti ya CAG
[/QUOTE
Umeongea real man uku padogo wanajifanya kweli kukamia uko kwenye billions of money kimya, kutekana kimya, GOD bless Tanzania citizens
 
Aliyerecord na kusambaza hajafanya poa, hao jamaa wanapiga sana kazi tena kwenye mazingira magumu sana, jua,mvua zao hao..mpaka unawaonea huruma.
Na hawana sehemu ya nyongeza zaidi ya humo barabarani...watu wanapiga mabilioni kila siku na allowances za kutosha...
Wawaache bana..
twajibiii
 
Back
Top Bottom