Trafiki wawili wakamatwa baada ya kunaswa kwenye video wakipokea Rushwa hadharani

Trafiki wawili wakamatwa baada ya kunaswa kwenye video wakipokea Rushwa hadharani

Wanakula kwa urefu wa kamba zao, hizi sio rushwa za maana, tizameni wajuu wale wabadhirifu haswaa, wale wanatokea kwenye ripoti ya CAG.

Kuna mtu aliisababishia serikali hasara ya bilioni ngapi sijui akapigwa faini ya milioni 100 🤣😂
Namkumbuka yule, alikuwa afisa wa ATCL
 
Aliyerecord na kusambaza hajafanya poa, hao jamaa wanapiga sana kazi tena kwenye mazingira magumu sana, jua,mvua zao hao..mpaka unawaonea huruma.
Na hawana sehemu ya nyongeza zaidi ya humo barabarani...watu wanapiga mabilioni kila siku na allowances za kutosha...
Wawaache bana..
Huna akili boss, hao wakati wanaajiriwa walipewa mikataba ya kazi na walisaini, sasa iweje useme mazingira magumu, kama wanaona mazingira ni magumu waache kazi wakafanye zenye mazingira malaini, msihalalishe rushwa kwa mazingira magumu ya kazi.
 

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema askari wawili wa Kikosi cha Usalama Barabarani walioonekana kwenye video wakifanya vitendo ambavyo ni kinyume cha maadili ya Jeshi la Polisi kwa maana ya kupokea rushwa, tayari wamekamatwa na wako mahabusu na hatua za kisheria zitafuata dhidi yao.
Pia, Soma: Hapa ni wapi? Trafiki wadakwa kwenye video wakichukua Rushwa mara kadhaa
 

Attachments

  • IMG-20250115-WA0008.jpg
    IMG-20250115-WA0008.jpg
    77.1 KB · Views: 5
Tanzania Kuna askari wa usalama barabarani asiyekusanya hela ? Hata kama hauna kosa ataomba hela ya maji Tena kwa kulazimisha
 
Back
Top Bottom