Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema askari wawili wa Kikosi cha Usalama Barabarani walioonekana kwenye video wakifanya vitendo ambavyo ni kinyume cha maadili ya Jeshi la Polisi kwa maana ya kupokea rushwa, tayari wamekamatwa na wako mahabusu na hatua za kisheria zitafuata dhidi yao.
Pia, Soma:
Hapa ni wapi? Trafiki wadakwa kwenye video wakichukua Rushwa mara kadhaa
Rushwa imetapakaa kila Mahali katika nchi hii ya Tanzania, hakuna kitu cha ajabu hapo. Ni Askari Polisi wachache Sana kupita kiasi ambao ni wasafi, Yaani hawajihusishi na Rushwa Wala vitendo vingine viovu vya uhalifu ama uvunjaji wa Haki za watu.
Kwa uzoefu wangu, kwenye kila penye Kituo cha Polisi jirani ya hicho Kituo lazima kuna Vijiwe vya kupokea rushwa au kuna Mawakala wa kupokea rushwa ili baadaye mzigo huo wa rushwa uweze kufikishwa kwa Askari Polisi anayehusika.
Mathalani, Mawakala ambao mara nyingi Sana hutumika kupokea rushwa za Maaskari Polisi na/au Mahakimu wa Mahakama huwa ni:-
1. Wapiga brashi Viatu ambao vilinge vyao huwa vipo jirani au pembezoni mwa Vituo vya Polisi.
2. Wauza Magazeti (ambao wapo katika vijiwe, fixed location).
3. Wahudumu wa Utoaji wa huduma Stationery au kupiga photocopies waliopo jirani na Vituo vya Polisi au Mahakama.
3. Askari wa Polisi Jamii au Askari Mgambo ambao wapo katika baadhi ya Vituo vya Polisi.
Mara nyingi sana Watu hawa (Polisi Jamii au Mgambo) hutumika kupokea rushwa za Maaskari Polisi na kuwapelejea wale Askari Polisi ambao wana Vyeo vya juu kidogo,
Kwa upande wa Mahakimu, wanaotumika kupokea rushwa zao mara nyingi ni wale Warumishi wa Mahakama wa ngazi za chini au wakati mwingine huwa pia kupitia kwa Mawakili.
Taarifa hii ni kutokana na Utafiti wa kificho Sana uliofanywa kuhusiana na masuala haya.