Trafiki wawili wakamatwa baada ya kunaswa kwenye video wakipokea Rushwa hadharani

Trafiki wawili wakamatwa baada ya kunaswa kwenye video wakipokea Rushwa hadharani

Kuna jamaa yangu alinambia akiwa anasafiri umbali mrefu anatenga elfu tano tano hataki kupoteza mda barabarani
Waache wale kwa urefu wa kamba zao
 
Kuna siku nilimkosakosa kumgonga traffic na pkpk barabaran....hzi mambo za Rushwa kutupiwa vikaratasi vilivyofungwashwa pesa barabarani aisee hasa haya mabus ya mkoani ndo tabia zao
 
sema hawa ni wapuuzi 💩
Kuna wengine wanapokeaga rushwa wanavizia magari yanayopita service road pale buguruni... huwa nawaangalia najisemea hawa wajinga siku yako inakuja... bad enough kazi yenyewe kufukuzwa ni rahisi kama kumfukuza dada wa kazi, boss akijisikia anytime unaachia gwanda
 
sema hawa ni wapuuzi 💩
Kuna wengine wanapokeaga rushwa wanavizia magari yanayopita service road pale buguruni... huwa nawaangalia najisemea hawa wajinga siku yako inakuja... bad enough kazi yenyewe kufukuzwa ni rahisi kama kumfukuza dada wa kazi, boss akijisikia anytime unaachia gwanda
Wazoefu hawapokei wao wenyewe wanakuambia hela
Peleka pale kwa Fulani

Ova
 
Ukweli ukisemwa Rushwa ni mfumo rasmi nchini mwetu. Tunakwenda kupata huduma huku tunajipanga kutoa rushwa. Hata kama huduma ni haki yetu.
Wakubwa zao ndiyo wanawatuma
Na wao wana mgawo wao hapo
Difenda zenyewe za polisi zikirudi
Wanaambiwa wawe na hesabu

Ova
 
Hizo video wakipata wakili mzuri kwenye mahakama za, kiraia wanashinda kesi,, sijui kwenye mahakama zao za, kijeshi
 

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema askari wawili wa Kikosi cha Usalama Barabarani walioonekana kwenye video wakifanya vitendo ambavyo ni kinyume cha maadili ya Jeshi la Polisi kwa maana ya kupokea rushwa, tayari wamekamatwa na wako mahabusu na hatua za kisheria zitafuata dhidi yao.
Pia, Soma: Hapa ni wapi? Trafiki wadakwa kwenye video wakichukua Rushwa mara kadhaa
Wanawaonea, hao traffic wamepata nafasi ya traffic kwa kuhonga, na waliye mhonga awateuwe kuwa trafiki naye alihonnga kuwa kwenye kitengo cha kupandisha vyeo. Halafu unataka wasifanye kitu kilicho wapa kazi! Kama unataka kukomesha Rushwa Anzia jjuu huko kwa Waziri wa Mambo ya ndani kuja mpaka kwa IGP ukisha safisha mpaka hapo hao wadogo wala hawana shida watanyoka tu.
 
Back
Top Bottom