Trapped to a married man

Siamini kwenye limbwata mkuu. Ninachoamini kuna wanawake wengine watamu sana na pia ni warembo. Ukikuta mtoto mrembo halafu ni mtamu pia sio mchoyo kukupatia basi hilo ndio limbwata unalolisema.
Ukisha rasmisha huyo nyumba ndogo ndipo utaomba dunia ipasuke. Wanawake huwa hawaridhiki hapo anatafuta uhalali, akiupata anataka atambulike kwa ndugu zako rasmi, akifanikiwa anakuja kwa mkeo maana atataka mkeo ajue wapo wawili; kifuatacho atataka umpige kibuti ili abaki peke yake. Hivi unajua nani wataathirika zaidi? Jibu ni kuwa ni watoto wako. Kama una mabinti hao sahau. Piga nje ila usioe ndugu yangu yakakufika yetu! Nduki
 
mkuu hi comment umeitoa kwa jazba Sana .
Pole kwa kilichokukuta huo mwaka.
Nilishapoa ndugu, ila huwa kuna mambo nikiyaona huwa naghafirika sana. Ujue kujitoa kwa mtu ukiwa huna au una kidogo ila unaona wacha apate yeye kwanza angalau asijeweweseka na wenye navyo na mipango kede kede kumbe mtu huku pembeni ana mipango yake tofauti juu ya hicho mnachokipanga kila siku mkiwa wawili.

Huyu mdada kwa nini asimwambie tu huyo jomba ambaye yupo single kwamba mimi sina mpango na wewe, niko na mtu ila ukitaka kukaa kaa, usipotaka kaangalie mbele ili jomba achague mwenyewe. Kawahold wote halafu anashindwa kuamua afanye lipi
 
Olewa na huyo ambae hanamke, hiyo ndoa ya Siri baadae itakutesa Sana ..watu wanapata vichaa sababu hii, unadhani familia yake wakijua itakuaje. Kama kweli anakupenda isiwe ndoa ya Siri.

Hapo ndo utajikuta unatamani kuwa muislamu😂😂😂😂
 
Pole kwa changamoto my dear.
Nikiwa kama mume wa mwenyewe, nashauri kwa upendo tu, oana na huyo kaka bachelor, uachane na huyo mume wa mtu. Kwa sababu bottom line, one day atarejea kwa mkewe mazima na atakuacha. Lakini pia, assume wewe umeolewa, then jamaa anapata dada mwingine mzuri sana na anamuoa kisiri huku akiwa na wewe, utajisikiaje? Maoni haya ni yangu!
 
Kama ameweza kumsaliti mkewe aliyempenda kabla yako na kumuoa basi ujue siku zako za kulia na kusaga meno zinakuja, atapata chombo kipya na kukukimbia tena! Siyo mume huyo.
Ushauri wangu; chukua chako mapema (mtaji na hiyo nyumba anayokujengea) then jikate.
 
Kama ana kupenda kwa dhati kabisa, mtafunga hiyo ndoa lakini mke mkubwa atatelekezwa.
Mungu husikiliza sana kilio cha mwanamke, msala utakao upata hauta sahau...labda asiwe muombaji.
 
Hili povu vepeeeeeh? Lol
 
"Meanwhile upande wa pili kuna kaka ambae hajaoa anataka kuja kutoa mahali,well paying job we have a connection lakini hajafika level za yule mume wa mtu"

Vijana wenzangu tutafute hela tu si mmeona kinachoendelea.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka mnooh lol
 
Duuuuh poleeee San, maan umeongea kwa jazba mnooh.
 
Nipo kwenye ndoa mwaka wa 12. Usijidanganye kufanya siri eti utamuumiza mke wa jamaa.
Trust me, anafahamu uwepo wako labda tuu awe hakufaham kwa sura na jina. Inawezekana huyo mama ameshazoea tabia za mumewe kabla hata ya kukupata wewe ndio maana haoni jipya..
Niseme tuu ukweli...sisi wanawake tulioko kwenye ndoa hua tunapata mshtuko mkubwa mara ya kwanza tunapogundua mume sio mwaminifu...halaf baadae moyo unaingia ganzi tunazoea tuu...hata mume afanye nini huwezi kuguswa hata kidogo...utamtimizia mahitaji yake yooote lakini moyoni anakua hayupo...siku mume akigutuka kutoka usingizini kutaka kurepair ndoa mke anaona usanii tuu, mume anabaki analaumu mke kwa watu bila kutafakari kilichowafikisha kwenyye state hiyo...
Siwezi kukupa neno zuri la ushauri zaidi ya neno la Mungu kwa mujibu wa imani yako..hebu rejea maandiko ya imani yako yanasemaje? Naamini utafunuliwa jibu sahihi huko.
Kila la kheri
 
Nikitaka kuoa, naomba nikuweke katika list kama utakua bado single, mama mchungaji. Heaven Sent
 
😅😅😅kwaiyo vinashawishi kuoa kisirisiri.
Ndo hvo mkuu,hasa kakiwa kametoka kuoga ile usiku wakat wa kulala ngoz zenu znapogusana unajihis tofaut sana tofaut na unapokuwa na mwanamke mkubwa
 
Let me ask you uyo Jamaa mwenye mke angekua hajaoa na uyo Jamaa single boy

Ungeambiwa umchague mmoja tu (ndo option yko)
Ungemchagua Nan?
Aisee kumuacha siwezi
Bado sijapata mtu kama yeye,kwasababu hii sio mada yake ndio maana sijapata nafasi ya kumuelezea.Kama ningekuwa simpendi huu uzi usingekuwa hapa ninge jilipua na huyu jamaa mwenye mke
 
Kumsingi, wewe ndie una matatizo. Wanaosema mume au mke wa tu ni sumu huwa mnawaza swala la kukamatwa tu na kubananishwa ila mnasahau kuwa kitendo cha kuingia kimahusiano na mume au mke wa mtu sio tu ni hatari kwa afya na usalama wako lakini pia unakaribisha unnecessary complications kama kupata mtoto nae, au kupeka ujauzito na kuzaliwa watoto wa nje ya ndoa katika ndoa ya mtu, kujenga hisia na mume au mke wa mtu kiasi kwamba unaanza kumuona mwenye mke au mume kuwa anakunyima haki yako ya kuwa na mtu unae mtaka.


Wewe una matatizo sababu ulikubali from the beginning ukijua huyo ni mume wa mtu, ulitakiwa mapema sana ulipojua kuwa ni mume wa mtu, muda ule ule ungesitisha mazoea na kuachana nae.

Sasa kwanza unadanganya kuwa unapenda wanaume wawili kwa wakati m'moja, how is that even love kwanza?! How is it possible kupenda watu wawili kwa usawa ule ule....?!

So we kubali tu kuwa wewe ndie tatizo. Na kuhusu kukushauri, kwa sasa ni ngumu maana nitakushauri maamuzi magumu ya kumuacha mume wa mtu na kuwa na huyo ambae hana mtu maishani mwake. Swala ambalo najua litakuwa ni gumu sana kwako kufanya kwa wakati huu.

Mmmmmmhmn ila aisee watoto wa kike muda mwingine, mna akili za kipuuzi..... Yote hiyo ni tamaa. Sasa unaanzaje kujenga na mume wa mtu?! Na unajua mtu ana familia yake?!
 
Kama ni muislamu akuoe mke wapili


Km mkristo na anasema anakupenda kweli basi amuache mke wake akuoe wewe na hicho ndo kipimo sahihi kwamba kweli anakupenda otherwise unalishwa matango pori tu..


Ngoja nikupe siri mwanaume akipewa stress na mkewe au akinyimwa unyumba na mkewe kwa kipindi kirefu uwaga inafika kipindi anakuwa kavurugwa kabisa hajui hata kwanini kaoa huyo mwanamke sasa ukitokea unampa game za kutosha,mko nae mbali mbali hivyo haumpi stress basi anaweza kuhamia kwako lakini SI kwasababu anakupenda sana ila ni kwasababu kuna vitu unampa ambavyo mkewe hampi...

Sio love hiyo ni hiyo sex na stress free ndo vimemroga kua makini Mwanaume huyo anaweza kuacha mke kwa mchepuko, huyo ni limbukeni atakuacha wewe kwa mwanamke mwingine kipindi ambacho huwezi kumpa sex..

Mwanaume ambaye si limbukeni hawezi kumushusha mke thamani eti unamtelekeza mke sababu ya mchepuko labda km alikulupuka kuoa ila Mimi na akili zangu timamu kabisa nimchunguze mwanamke weeeeeee,nimtolee mali,nimuoe halafu atokee mwanamke mwingine eti nimpe thamani kubwa mchepuko kuliko mke.Neveeeeer haipo hiyo.

Na wewe ur self esteem is low ndo mana unategemea thamani za wanaume wanaokutongoza kujiona una thamani.Mwenyewe hapo unajiona una thamani kisa mwanaume kaacha mkewe kukufuata wewe, kisa mkaka mwenye kazi yake nzuri anakutongoza hahaahaha[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].B.
 
Wadau wanakushangaa kupenda wanaume wawili kwa mpigo usijisikie maumivu sana kwani ukiyajua ya kwao hakika utaduwaa,,

Ukiolewa na bachelor basi mume wa mtu atakuwa mchepuko na heri iwe hivi kuliko kuolewa na mume wa mtu kwa ndoa ya Siri,

Pole mkuu kama vipi achana nao wote
 
kwa wakati wako dada pitia ukurasa wa iddi makengo yuko insta, utakutana na visa vya wengine vinavyofanana na chako na wako wanaojuta. wengi wametapeliwa mali zao na kuachwa masingle mom.
 
kesho kutwa atatafuta mwingine wa kuoa baada ya wewe kulogwa na mke wake wa kwanza
Muache tu[emoji23][emoji23][emoji23] au kitamkuta kile cha yule dada wa Moshi [emoji2][emoji2]
win win situesheni[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…