Trapped to a married man

Kama hivyo ndivyo, bibie kubali kuolewa, sababu na wewe unakuwa mke halali ila unakuwa wa pili tu. Moja, na mbili zote ni namba tu ili kubainisha na kujua nani kaanza nani kafata.

Olewa bibie..... ni hayo tu.
Kuolewa sio dhambi. Ila kuolewa kisiri khaa, kwamba mkewe asijefahamu kama jamaa kaoa, ndio ndoa gani sasa!?
 
Wanawake wengi tuna penda ready made ya wanaume hatujui hustle za wake zao na maombi Hadi kufika hapo, I'm sure hata huyo dada akiolewa mwanaume ataporomoka uchumi wote.
Na kila mwanaume kwa mchepuko husifia hata visivo faa, ka ana mpenda aonyeshe talaka na amuoe hadharani sio kisiri hata hyo apartment Ni daganya Toto ya kumuingiza kingi ili ajae wafunge ndoa then ale corner, na mke hamuachi, ng'o Kuna wanawake wamejenga na nyumba kabisa.
Mume wa mtu sio wakumweka kwenye mahesabu
 
Kuolewa sio dhambi. Ila kuolewa kisiri khaa, kwamba mkewe asijefahamu kama jamaa kaoa, ndio ndoa gani sasa!?
Mnachosahau ni kuwa usiri huwa unakuwa mwanzoni, na sisi huwa tuna hekima zetu kufanya siri, siyo tunakurupuka. Hayo ni mahesabu tu ila lazima mke mkubwa aje kujua.
 

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Aisee
 
Kwani sharti la ndoa ni nini ? Kwamba mtu akiolewa kwa siri ndoa haikubaliki au ?
Haikubaliki kwetu wakristo ndoa ni moja tofauti na zenu, mtu ana Nia njema kwanini afanye Siri?
 
Mnachosahau ni kuwa usiri huwa unakuwa mwanzoni, na sisi huwa tuna hekima zetu kufanya siri, siyo tunakurupuka. Hayo ni mahesabu tu ila lazima mke mkubwa aje kujua.
Hawa ni wakristo ujue! Ingekuwa kama sisi mbona nami ningemtakia kheri aje kulia mbele ya safari
 
Umeongea kwa hisia mpaka nimejitafakari na mimi juu ya unavyotutazama wanaume.

Mimi ni mwanaume lakini nimezaliwa na Mwanamke, nina Siblings wakike sasa vipi kama mama yangu angetelekezwa na baba kisa mwanamke aliyeshindwa kucontrol tamaa kama huyu. Ama dada yangu atelekezwe leo hii kisa selfish mmoja wa namna hii. It's not fair.
 
Haikubaliki kwetu wakristo ndoa ni moja tofauti na zenu, mtu ana Nia njema kwanini afanye Siri?

Andiko gani katika Biblia linakataza mitala ?

Usiri huwa tunafanya kwa ajili ya kuusoma upepo kwa mke mkubwa, sababu tulio wengi wake zetu wakubwa huwa wakorofi sana.

Pili, ngoja nikuulize swali usiri unao ongelewa hapa unauelewa au kwako wewe usiri wa ndoa ni upi ?
 
Hawa ni wakristo ujue! Ingekuwa kama sisi mbona nami ningemtakia kheri aje kulia mbele ya safari
Ina maana Ukristo hauruhusu kabisa Mitala ?

Kama ni hivyo basi akaolewe na mdau mwingine.
 
True mwanaume si kiumbe wa kumwamini labda baba yangu na kaka yangu tu basi

Mbona tuna aminika tu vizuri cariha , lakini hii si ishu ya wanaume tu sababu huyu binti tayari alikuwa na kijana mwenzie mwingine ambaye hajaoa

Tufikiri kwamba yule kijana kule ni mwaminifu na kweli anataka kumuoa, Je si yeye ndiyo muhanga

Trust issues nafikiri ipo kote tu si kwetu wanaume peke yake

Utakuta baadaye muanzisha mada anatuita wanaume wote mbwa kumbe ni yeye alikosea kufanya maamuzi
 

Nia ya usiri ni kuto muathiri bi mkubwa
Ila ndugu wa mume mpaka mama mkwe mawifi marafiki wananijua
Nisingependa huyu mke mkubwa aumie kwasababu ya mume wake ndio maana nalitafakari hili
 
Duuh, huyo mume wa mtu atayagawa vipi majukumu yale kwa familia zote mbili...upo tayari kupewa zamu?

All in all, angalia wapi palipo pema kwako ila nadhani huyo kijana mwenzio ana future zaidi kuliko huyo married man, kama anakupenda kweli ndoa isingekua ya siri, angetaka akuweke hadharani bila kujali na sio sirini
 
Uliloandika Ni kweli Ila binti huko alifata kuhongwa vizuri yeye hajazaa ujue Bora wale huchepuka kwa starehe Ila huyu ana ndoa na watoto imagine hyo familia ikivunjika na ujue huwezi penda vitu viwili kwa usawa imagine hyo energy ya kuhonga mchepuko Ange invest kwa mkewe na familia.
 
Ina maana Ukristo hauruhusu kabisa Mitala ?

Kama ni hivyo basi akaolewe na mdau mwingine.
Hauruhusu, hivyo hiyo ndoa itakuwa ya siri milele na ataishi kama michepuko wengine tu. Na si hivyo tu, endapo lolote likimtokea huyu mumewe iwe kustaafu au kufariki basi hana haki yoyote kwa kuwa hatambuliki kama mke.

Na mume anaonekana anampenda sana mkewe ndio maana anataka ndoa ya siri.

Kingine nachokiona , mtoa uzi anadhani mahaba wanayopeana saizi yatadumu milele hivyo hivyo.

But kubwa ambalo kalirudia rudia ni hali nzuri ya kiuchumi ya mume wa mtu, kiasi anaonesha kinachomvutia si mapenzi bali uchumi wa huyo mume wa mtu.

Anasahau kuwa uchumi huwa unapanda au unaporomoka

Ila hajui kuwa wanawake tukishazaa tunaanza kutamani familia ikamilike, awepo baba, mama na mtoto/watoto waamke pamoja wafurahi pamoja. Ikifika hapa ndipo ataona kitu gani anakikosa pale mume wa mtu yupo kwa mkewe na hawezi kutoka, wakati huo yeye na mtoto/watoto wanamuhitaji pia.


Lakini watoto wataozaa watakosa haki ya kuwajua ndugu zao hadi mume atapofariki[emoji23][emoji23]watavyovamia msiba

So sad!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…