TRC mnazua taharuki na madaraja yenu! Kwa hili mmetukosea sana wananchi

Uzio huo hauna miaka 2 ngoja waturuki waondoke utakatwa wote.
Wao wangeweka matobo ya kupita watu chini ya reli ingesaidia kudumisha huo uzio
 
Nchi nzima hata mijini na wilayani ipitayo reli kilio the same wamezuia watu kuvuka bila kuwawekea matobo chini ya reli
 
Ni ngumu kutoa uzio kwenye hii reli, mtazoea tuu kupanda na kushuka vivuko, ni safe zaidi kuliko kuiacha wazi
Wataingia gharama sana kurejeshea uzio kila mara pindi watu wakikata.
Mfano gongo la mboto wananchi walikata uzio wapite
 
Umbali wa vivuko sio rafiki kwa wakazi wa eneo husika
 
Wa kulaumiwa hapa ni mainjia wetu wao wanakaa masaki osterbay hawajui hadha wapatao wakazi wa huko.
Sijui walisomea wapi hivi unaziba vipi mji kwa wavu pande mbili bila kuweka vivuko vya miguu ili maisha ya wengine yaendelee.
Wanataka wapewe sifa na viongozi
 
Ana kitambi afu kalewa, dah sio poa.
Ukilewa hutoboi, maana Kwanza Kuna ka ngazi ka mchongo kushukia huko chini, halafu Kuna madimbwi pale lazima ukanyage mawe kadhaa kufika sehem kavu, then ubend kuelekea langoni, πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ daah
 
Huo uzio walioweka TRC umepunguza mapato ya treni la mwakyembe ng'ambo ya pili wanashindwa kupanda tren kwa sababu ya fence ili apande treni anahitaji kupita vituo vitatu vya daladala ili akapate sehemu ya kupanda mwakyembe.
So kama TRC walimudu kubeba abiria elf 25 kwa siku Leo hata elf kumi hawafiki sababu ya fence hii imeathiri mapato yao kwa siku wapatayo toka kwa nauli ya mwakyembe.
Wanaweza kuwarudisha abiria hao 15 elf waliopotea kwa kuweka vipito salama yaani matobo au vipenyo chini ya reli kwenye mapitio asili ya watu.
Pale Ukonga wananchi wamezuiliwa haki ya msingi kumudu kupata hudumq za kijamii mfano nyumba za Ibada makanisa na misikiti ipo upande wa pili wa uzio.
 
Asante kwa kuliona Hilo na una maoni mazur san
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…