TRC: Picha zinazosambaa ni za Mabehewa ya safari ndefu, mengine yatafika Juni 2023

Wewe Bado mdogo ukikua utajua

Kuna siku nilimpeleka rafiki yangu hospital kumuona baba yake tulipofika tukaambiwa Mzee amefariki tulipotoka nje tukakutana na mama yake pamoja na dada zake kama kama 4 hivi na rafiki zao wote ni wa kike

Yule rafiki yangu akamwambia mama yake na wale dada zake kuwa baba alizidiwa amepelekwa icu doctor amesema hatuwezi kumuona Leo Hadi kesho asubuhi nendeni nyumbani mi nipo hapa kuweka mambo mengine sawa

Walipotoka nje wanaondoka tukaa sehemu tukaagiza maji tukawa tunakunywa huku jamaa anatafakari baada ya mda akawauliza kama wameshafika nyumbani wakamjibu ndio akawambia baba amefariki

Angekuwa poyoyo kama wewe ungewambia pale pale alafu ingekupata kazi ya kulinda usalama wao na kuwafikisha nyumbani

We changia tu kuhusu mabehewa hayo mengine akili yako ikikomaa utayajua
 
Kama ndio hivyo,kwanini asingesema ni mgonjwa?
 
Kwa hiyo yakiwa ya safari ndefu, ndio yanakuwa tofauti na picha walizotoa wenyewe?
Safari ndefu ni kutoka wapi hadi wapi? Na reli ya safari ndefu imekamilika, hadi mabehewa yake yanaanza kuletwa, Ila ya safari fupi haijakamilika ndio maana mabehewa yake hajaletwa?!!!
 
Yaani yametangulia mabehewa ya safari ndefu wakati reli haijafika hata hapo Dom.

Halafu safari fupi ya Moro inayoanza Feb 2023 behewa zake zitakuja Juni 2023.
Mauzauza hoyee!!!
 
Yaani yametangulia mabehewa ya safari ndefu wakati reli haijafika hata hapo Dom.

Halafu safari fupi ya Moro inayoanza Feb 2023 behewa zake zitakuja Juni 2023.
Imeisha hiyo... mtapanda haya haya yaliyokuja🤣🤣
 
Hawana jipya hawa tayari pumzi imekata, wameona waishie hapo.

Magufuli alikua anatumia uchawi gani kufanya mambo? Mungu amrehemu yule mzee aisee.
Uchawi na Mungu, wapi na wapi?
 
Yaani yametangulia mabehewa ya safari ndefu wakati reli haijafika hata hapo Dom.

Halafu safari fupi ya Moro inayoanza Feb 2023 behewa zake zitakuja Juni 2023.
Tatizo la hawa watu, ni kujiona wana akili nyingi kuliko wananchi wanao waongoza! Kumbe kinyume chake, ndiyo ukweli wenyewe.
 
Yaani yametangulia mabehewa ya safari ndefu wakati reli haijafika hata hapo Dom.

Halafu safari fupi ya Moro inayoanza Feb 2023 behewa zake zitakuja Juni 2023.
Viongozi wa hii nchi wapinwe afya ya akili walah🤣🤣🤣
 
Sasa sgr haifiki hata Dom halafu leo unaleta mabehewa ya Tabora? Na kama mabehewa yako hivi vichwa vitakuwa vinachekesha zaidi
 
Mmi nilijua zimetangulia power bank kumbe ndio mabehewa yenyewe! Dah
 
Sasa yakiwa ya safari ndefu ndio yawe ya kizamani? Hayo mabehewa ni ya enzi za mkoloni.

Ebu acheni ujinga ,rudisheni hizo takataka mlipotoa ,ndio maana wakenya wanatudharau sana.

Hiyo mitakataka si kama ile ya zamani? Hivi utatofautishaje hayo mabehewa na treni ya mwakyembe?
 
Ni kwamba hela hakuna au kiwanda kinaruhusiwa kuzalisha behewa 13 tu kwa mwaka,,,,huu ujinga wa kuchelewesha mipango ndio ulifanya yule mzee akatishe posho za vikao na hatimae seminar zikagawanywa pipi na azam embe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…