TRC yatangaza kurejesha huduma za treni ya abiria kutoka Dar kwenda Moshi

Ndio nakubali, lakini nchi ambazo usafiri wa treni umeshamiri ni kule ambapo kuna treni na reli za kisasa, ambazo ni spidi na rahisi kuliko magari.
Sasa hii ya Dar kwenda Moshi inatakiwa na yenyewe iwe na spidi kubwa ili kumshawishi abiria aache gari apande treni
 
🤣
🤣🤣🤣🤣🤣 lini hiyo mbona sijawahi kuisikia mangi?
Hahaa nikatika moja ya mapokezi ya ndege zetu zile zamwanzo mwanzo sasa nazani kuna kiongozi alipiga jungu kua zile ndege hazina speed na hilo jungu likamfikia mkuu so siku hiyo aliamua kumtolea uvivu kwakusema "kama unataka yenye kasi kapande ndege za jeshi" japo hajamtaja ila mkuu alirusha tu jiwe gizani
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Mmeanza kupekenyua mtafute points za kukosoa. We kakate tiketi usafiri kama unajali muda kwea Pipa Air Tanzania
Hilo swali la muda ni muhimu. Ili tupange ratiba zetu vizuri. Hakuna suala la kukosoa hapa tunataka tujue muda ili tusijepishana na watakao kuja kutupokea, tafadhali.
 
Watanzania wengi wako bado kwenye stage ya quantity (wingi na uchache), hawajafikia level ya quality (ubora). Ni wale wanaotafuta chakula cha kushibisha tumbo tu, ni wale wanaojenga nyumba bila ramani wala mkandarasi, ni wale wanaosomesha watoto wao shule za kata, ni wale wanaokodi nyumba za mitaa ya Tandale, Buguruni, nk. Sina uhakika kama ni watanzania ambao wako tayari kulipa sh. 50,000 kufuata USB kwenye basi na kuacha treni la shi. 15,000 hadi Moshi.

Kwanza tuhangaikie quantity kisha ndio tuone namna ya kuboresha (quality). Lakini sio vibaya kama uwezo wa TRA unamudu kufanya vyote quanty and quality kwa muda uliobaki wakafanya vyote kwa pamoja.
 
Abiria wa Kanda ya Kaskazini kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka 2019, abiria wa Kaskazini watakuwa na kicheko kwao baada ya treni ya abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi kuanza Disemba.

Tayari Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa tangazo la kuanza kwa usafiri huo na kuthibitishwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Isaac Kamwele.

Waziri Kamwele amesema kama Serikali imefurahi kufikia hatua hiyo ukizingatia treni hiyo ilikuwa ianze tangu Septemba 2019.

Hata hivyo, amesema kutokana na changamoto za kunyesha mvua na kusababisha baadhi ya miundombinu ikiwemo ya reli kuharibika katika ukanda huo wa Kaskazini ndio maana kukawepo na uchelewaji wa kuanza kwake.

“Sasa ile tabia ya wafanyabiashara pale stendi ya ubungo kulangua abiria tiketi wakati watu wakienda kula sikukuu na ndugu zao itakoma, kwani hata mimi ilishanikuta na kama Serikali tulikuwa tunahangaika kutafuta njia ya kukomesha vitendo hivyo na ujio wa treni hii ya abiria utasaidia,” amesema

Kuhusu nauli, Waziri Kamwele amesema wameacha ileile iliyokuwa ikitumiwa tangu kusitishwa kwa usafiri huo na ndio maana hawakuitisha hata kikao cha wadau kuhitaji maoni ya nauli.

 
Wakati kuhusu uwezo wa kusafirisha abiria, amesema itategemea na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (Latra)


Sumatra na Latra

Naona kama kuna mamlaka inajibanza kwa nyingine bila sababu kwanini isimezwe kabisa?
 
Mchaga sio Muha, wajipange kwa kweli.hii sio reli ya kati ya kubeba wachunga ngombe
 
sisi wengine treni tunaziona tu. pengine mpango wa kupanda tunao, ndiyo tuna-weigh options. kuuliza swali kama nililouliza ni sababu nataka majibu yenye uelekeo wa uhakika, hivyo si kila kitu ni kujiongeza. mengine yanaulizwa yakitaka majibu yenye usahihi.
 
Mapumziko ya mwisho wa mwaka kwa wote wanaokwenda Tanga, Moshi na Arusha mambo yamedamshi.

Usafiri wa treni ni salama na nafuu. Awamu ya tano kazini. Umati Ubungo bye bye.

#T2020JPM

 
Inatumia siku ngap hyo treni kufika mosh, af mbna naul kubwa Sana kulinganisha na mabasi?
 
Maskini wenye kumiliki mabus. Wengi wamekopa Benki kununua Mabus na mwisho wa mwaka ndo msimu wao. Kila kitu kina mwisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…