TRC yatangaza kurejesha huduma za treni ya abiria kutoka Dar kwenda Moshi

TRC yatangaza kurejesha huduma za treni ya abiria kutoka Dar kwenda Moshi

Kaka usafiri huu utakuwepo muda wote, duniani kote kuna usafiri wa barabara, train, ndege, na majini kutokana na unafuu wa bei, usalama, uharahaka wa kufika, upatikanaji, na utashi wa mtumiaji. Hivyo hata hata hapo kwetu watakaopenda usafiri wa treni, mabasi, ndege, meli, na hata fisi na farasi wapo na watakuwepo.
Ndio nakubali, lakini nchi ambazo usafiri wa treni umeshamiri ni kule ambapo kuna treni na reli za kisasa, ambazo ni spidi na rahisi kuliko magari.
Sasa hii ya Dar kwenda Moshi inatakiwa na yenyewe iwe na spidi kubwa ili kumshawishi abiria aache gari apande treni
 
🤣
🤣🤣🤣🤣🤣 lini hiyo mbona sijawahi kuisikia mangi?
Hahaa nikatika moja ya mapokezi ya ndege zetu zile zamwanzo mwanzo sasa nazani kuna kiongozi alipiga jungu kua zile ndege hazina speed na hilo jungu likamfikia mkuu so siku hiyo aliamua kumtolea uvivu kwakusema "kama unataka yenye kasi kapande ndege za jeshi" japo hajamtaja ila mkuu alirusha tu jiwe gizani
 
Hahaa nikatika moja ya mapokezi ya ndege zetu zile zamwanzo mwanzo sasa nazani kuna kiongozi alipiga jungu kua zile ndege hazina speed na hilo jungu likamfikia mkuu so siku hiyo aliamua kumtolea uvivu kwakusema "kama unataka yenye kasi kapande ndege za jeshi" japo hajamtaja ila mkuu alirusha tu jiwe gizani
😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Mmeanza kupekenyua mtafute points za kukosoa. We kakate tiketi usafiri kama unajali muda kwea Pipa Air Tanzania
Hilo swali la muda ni muhimu. Ili tupange ratiba zetu vizuri. Hakuna suala la kukosoa hapa tunataka tujue muda ili tusijepishana na watakao kuja kutupokea, tafadhali.
 
Kwa kukusahihisha kwanza nianze na USB na sio UBS!

Swala la kuwepo ama kutokuwepo liko based kwenye ushindani zaidi.

Ukiangalia BM Coach, Marangu Coach, Dar Lux hawa ndio leading brands wenye premium trim ya mabasi kwa njia hio. Sasa unapotaka kuwahamisha watu lazma uwape sababu kwanini wahamie kwako.

Ni ngumu sana kumuhamisha mtu ati kisa umemjengea nyumba mpya ambayo kimsingi ina hadhi ya chini kuliko ile alieko nayo sasa kwa facilities na kila kitu. Kwa mfano, umtoe mtu Upanga umpeleke kwenye nyumba ya room mbili porini chanika au vikindu bila kumpa sababu za msingi au ushawishi. Lazma umshawishi na aone faida ya kuhamia Chanika against Upanga, kibiashara huwa iko hivyo. Cost ya nauli iko chini ni sawa ila je, nini faida ya ku compromise speed na comfort ya basi lenye nauli kubwa against treni yenye bei nafuu? Hio ni Logic thinking!

Ni kichaa pekee ambaye atakubali kuhama katika mazingira kama hayo, isitoshe ni biashara. Sasa hili lina uhusiano wa moja kwa moja na hao mabwana Reli.
Watanzania wengi wako bado kwenye stage ya quantity (wingi na uchache), hawajafikia level ya quality (ubora). Ni wale wanaotafuta chakula cha kushibisha tumbo tu, ni wale wanaojenga nyumba bila ramani wala mkandarasi, ni wale wanaosomesha watoto wao shule za kata, ni wale wanaokodi nyumba za mitaa ya Tandale, Buguruni, nk. Sina uhakika kama ni watanzania ambao wako tayari kulipa sh. 50,000 kufuata USB kwenye basi na kuacha treni la shi. 15,000 hadi Moshi.

Kwanza tuhangaikie quantity kisha ndio tuone namna ya kuboresha (quality). Lakini sio vibaya kama uwezo wa TRA unamudu kufanya vyote quanty and quality kwa muda uliobaki wakafanya vyote kwa pamoja.
 
Abiria wa Kanda ya Kaskazini kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka 2019, abiria wa Kaskazini watakuwa na kicheko kwao baada ya treni ya abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi kuanza Disemba.

Tayari Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa tangazo la kuanza kwa usafiri huo na kuthibitishwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Isaac Kamwele.

Waziri Kamwele amesema kama Serikali imefurahi kufikia hatua hiyo ukizingatia treni hiyo ilikuwa ianze tangu Septemba 2019.

Hata hivyo, amesema kutokana na changamoto za kunyesha mvua na kusababisha baadhi ya miundombinu ikiwemo ya reli kuharibika katika ukanda huo wa Kaskazini ndio maana kukawepo na uchelewaji wa kuanza kwake.

“Sasa ile tabia ya wafanyabiashara pale stendi ya ubungo kulangua abiria tiketi wakati watu wakienda kula sikukuu na ndugu zao itakoma, kwani hata mimi ilishanikuta na kama Serikali tulikuwa tunahangaika kutafuta njia ya kukomesha vitendo hivyo na ujio wa treni hii ya abiria utasaidia,” amesema

Kuhusu nauli, Waziri Kamwele amesema wameacha ileile iliyokuwa ikitumiwa tangu kusitishwa kwa usafiri huo na ndio maana hawakuitisha hata kikao cha wadau kuhitaji maoni ya nauli.

 
Wakati kuhusu uwezo wa kusafirisha abiria, amesema itategemea na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (Latra)


Sumatra na Latra

Naona kama kuna mamlaka inajibanza kwa nyingine bila sababu kwanini isimezwe kabisa?
 
Wasipoweka USB na A/C itakula kwao! Haiwezekani nikajipepee kwa gazeti wakati nikiongeza elfu 10 kwenye hio nauli napanda chombo full A/C na kuchaji simu yangu bila wasiwasi.

Waboreshe kwanza Cabin za mabehewa ziwe comfortable. Watu wa wiring wamejaa VETA. Wawatumie hao kufanya interior designing za infotainment systems, upholstlery n.k ili ku keep pace na mabasi ya mkoani.

Wakiendeleza uzembe wa siti ngumu kama vigoda na uchafu ndani ya cabin anguko lao halitachukua muda.
Mchaga sio Muha, wajipange kwa kweli.hii sio reli ya kati ya kubeba wachunga ngombe
 
Sio kila swali linastahili majibu ya moja kwa moja. Hii reli ya kwenda Moshi ni ile ya kizamani sana, hivyo hutegemei speed yake iwe sawa na basi. Kwa vyovyote vile basi litakwenda haraka kuliko treni ya aina hii. Piga hesabu mwenye speed ya 30-40KM/h safari itakuwa ya masaa mangapi? lazima ujiongeze mkuu. Uzuri wake nyiani haitakutana na matuta wala tochi za barabarani wala foleni za mjini.
sisi wengine treni tunaziona tu. pengine mpango wa kupanda tunao, ndiyo tuna-weigh options. kuuliza swali kama nililouliza ni sababu nataka majibu yenye uelekeo wa uhakika, hivyo si kila kitu ni kujiongeza. mengine yanaulizwa yakitaka majibu yenye usahihi.
 
Mapumziko ya mwisho wa mwaka kwa wote wanaokwenda Tanga, Moshi na Arusha mambo yamedamshi.

Usafiri wa treni ni salama na nafuu. Awamu ya tano kazini. Umati Ubungo bye bye.

#T2020JPM

IMG-20191121-WA0076.jpeg
 
Inatumia siku ngap hyo treni kufika mosh, af mbna naul kubwa Sana kulinganisha na mabasi?
 
Maskini wenye kumiliki mabus. Wengi wamekopa Benki kununua Mabus na mwisho wa mwaka ndo msimu wao. Kila kitu kina mwisho.
 
Back
Top Bottom