TRC yatangaza kurejesha huduma za treni ya abiria kutoka Dar kwenda Moshi

TRC yatangaza kurejesha huduma za treni ya abiria kutoka Dar kwenda Moshi

Train hapo zamani zilikua zinandoka saa kumi jion pale Stesheni na huingia moshi asubuh ya saa mbili na nusu kama dereva ni mzuri...kipind hicho kulikua na dereva mtata sana wakuitwa Yona alikua anarifuluusha train acha tu moshi mnaingia asubuhi mapema kabisa....zile bata za buffet acha tu
 
Ufipa watagoma watawaambia watu wao wapande mabasi[emoji1][emoji1]
Mawazo yako ni ya kipumbavu. Ni mawazo yasiyojua kuwa haya mambo hufanyika kwa kodi za wananchi kwa hiyo hayapaswi kuwa SIASA kila yanapozungumzwa.

Hakuna mtu timamu wa akili mwenye kuyakataa maendeleo. Lakini haimaanishi kwa kuwa unajenga njia ya reli basi ukidhulumu fidia ya mali za watu unazozibomoa kwa ajili ya ujenzi unapata uhalali kwa kuwa reli ni maendeleo. Tufikie sehemu tuwe tunatumia akili zetu kabla ya kuropokaropoka na kubwatuka kama wehu.
 
Hapo kwenye kulala sijaelewa ....
kwa hivyo unaweza kununua kiji room kabisa!?
Behewa moja huwa na vyumba vitatu. Kila chumba kina vitanda 6 vyembamba kama vile vya hospitali za serikali. Kama una novel yako, unanyoosha tu mgongo unakula novo huku chombo kinakata mwitu.

Treni ni tamu sana kwa wanaopenda starehe.
 
Hii treni itakuwa poa sana ila changamoto itakuwa kwenye booking na ticketing...TRC wawekeze kwenye mfumo ambao utakuwa unamruhusu mtu kukata ticket mtandaoni, kwa mfano mfumo wa shabiby na Darlux, mtu unachagua seat, unabook na kulipia kwa simu na system inakutumia ticket yako kwenye email instantly...wakazi wa hiyo mikoa hustle za kwenda mpaka stesheni kukata ticket zitawashinda.

Mfumo huu unaweza kutoa hata ajira kwa agents kuwakatia ticket wale wasioelewa namna ya kufanya mambo mtandaoni
Kweli kaka, itabidi ticket zianze kuuzwa sasa ili kila mhitaji na hata TRC wajuwe mapema ni lini nani atasafiri. Hii itasaidia abiria kujitambua mapema kama amekosa au amepata nafasi ya kusafiri lini kwakutumia treni. Hii itamsaidia abiria kutafuta mapema njia nyingine za kusafiri kwenda anakokwenda.

TRC ni rahisi kusema ticket za tarehe fulani zipo au zimekwisha.
 
JPM akijikita kwenye usafiri wa treni, hakika nchi itapiga hatua kubwa sana kimaendeleo. Treni ni usafiri bora na nafuu sana kote duniani, nchi nyingi zilizoendelea zina mtandao mkubwa wa njia za treni. Katika hili kafanya Jambo jema sana, wale tunaoitwa "walalahoi" tunaangukia kwenye kundi hili sasa, wa juu yetu wataendelea kutumia "dreamliners"!!
 
Umesahau kuwaambia hao wachagga kuwa wasijakufanyiwa majaribio kwenye hizo treni waanzie kubeba mizigo kwanza baadae tutafikiria kama huo usafiri ni salama kwa afya zao mm nikienda kwa wakwe zangu ni bora basi bado familia inanihitaji mno
Wameweka mabehewa ya aina gani?
Je safari itatumia masaa mangapi?
HAWA JAMAA ZETU HUWA WANAJALI SANA UBORA,SIO SAWA NA WALE WANAOSAFIRI NA MAJIKO YAO NA KUANZA KUPIKIA HUMO HUMO.
 
Kwa hiyo mkuu hii ni kwa ajili ya msimu wa Disemba tu?

Maana kipindi kingine mabasi yanayoenda huko sio ya shida, na mtu atapendelea usafiri wa basi kuliko wa treni kutokana na spidi na ubora
Na wala sio gharama pia nikilinganisha na bei za hiyo treni

Anyway ngoja tusubiri tuone itakuaje, zinaeza kuwa za viwango kuliko tunavyowaza
Kaka usafiri huu utakuwepo muda wote, duniani kote kuna usafiri wa barabara, train, ndege, na majini kutokana na unafuu wa bei, usalama, uharahaka wa kufika, upatikanaji, na utashi wa mtumiaji. Hivyo hata hata hapo kwetu watakaopenda usafiri wa treni, mabasi, ndege, meli, na hata fisi na farasi wapo na watakuwepo.
 
Daraja la 2 kukaa. Nadhani Daraja la 1 litakuwa kusimama au kuchuchumaa maana la 3 ni kulala.



Shirika la Reli Tanzania, TRC linawatangazia watu wote kuwa safari za treni la biria kutoka Dar kuelekea Moshi zitarejea rasmi mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka 2019

Nauli Dar - Moshi inategemewa kuwa ifuatavyo:
- Daraja la tatu Tsh. 16,500
- Daraja la pili kukaa Tsh. 23,500
- Daraja la pili kulala Tsh. 39,100

================================

Dar es Salaam. Ikiwa tunaelekea sikukuu za mwisho wa mwaka 2019, abiria wa Kanda ya Kaskazini watakuwa na kicheko kwao baada ya treni ya abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi itaanza Desemba.

Tayari Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa tangazo la kuanza kwa usafiri huo na kuthibitishwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Isaac Kamwele.

Waziri Kamwele amesema kama Serikali imefurahi kufikia hatua hiyo ukizingatia treni hiyo ilikuwa ianze tangu Septemba 2019.

Hata hivyo, amesema kutokana na changamoto za kunyesha mvua na kusababisha baadhi ya miundombinu ikiwemo ya reli kuharibika katika ukanda huo wa Kaskazini ndio maana kukawepo na uchelewaji wa kuanza kwake.

“Sasa ile tabia ya wafanyabiashara pale stendi ya ubungo kulangua abiria tiketi wakati watu wakienda kula sikukuu na ndugu zao itakoma, kwani hata mimi ilishanikuta na kama Serikali tulikuwa tunahangaika kutafuta njia ya kukomesha vitendo hivyo na ujio wa treni hii ya abiria utasaidia,” amesema

Kuhusu nauli, Waziri Kamwele amesema wameacha ileile iliyokuwa ikitumiwa tangu kusitishwa kwa usafiri huo na ndio maana hawakuitisha hata kikao cha wadau kuhitaji maoni ya nauli.

Wakati kuhusu uwezo wa kusafirisha abiria, amesema itategemea na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (Latra) itakavyowapangia japokuwa uwezo wa behewa moja ni kubeba abiria 80 huku kichwa kimoja cha treni kikiwa na uwezo wa kubeba mabehewa 20.

“Katika idadi ya abiria tutakaobeba tutasubiri Latra watuambie kwa kuwa wenyewe ndiyo wataalam wa usafiri lakini uwezo wetu kwa behewa moja ni kubeba abiria 80 huku kichwa kikiwa na nguvu ya kubeba mabehewa 20,”amesema.

Treni hiyo itakayopita Korogwe mkoani Tanga, TRC imetangaza nauli zake ambapo Dar es Salaam hadi Korogwe daraja la tatu itakuwa Sh10,700, daraja la pili kukaa Sh15,300 na daraja la pili kulala Sh25,400.

Wakati kwa abiria watakaotoka Dar es Salaam kwenda Moshi daraja la tatu itakuwa Sh16,500, daraja la pili kukaa Sh23,500 na daraja la pili kulala Sh39,100.
View attachment 1267371
 
Umesahau kuwaambia hao wachagga kuwa wasijakufanyiwa majaribio kwenye hizo treni waanzie kubeba mizigo kwanza baadae tutafikiria kama huo usafiri ni salama kwa afya zao mm nikienda kwa wakwe zangu ni bora basi bado familia inanihitaji mno
sema "nita...." sio "tuta...." maana kuna watu walioteseka sana kwa muda mrefu na usafiri wa mabasi ambao hawezi kuendelea kusubiri kama unavyotaka iwe hapa. Hivi barabara ikishatengenezwa na kupitishwa na engineers wa ujenzi yanaruhusiwa malori tu kwanza yapite kabla ya mabasi. Watanzania tumejaa vituko.
 
Back
Top Bottom