Treni ya SGR yazimika tena Morogoro!
View attachment 3059049
Rais Samia akiwasalimia wananchi katika uzinduzi wa treni Agosti 1, 2024

Rais Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi amezindua rasmi huduma za usafiri wa reli ya kisasa (SGR), treni iliyokuwa imebeba wageni walioshiriki uzinduzi huo wakiwamo mabalozi na viongozi mbalimbali wa kiserikali kutokea mkoani Dodoma, imepata tena hitilafu karibu na Stesheni ya Morogoro kwa zaidi saa moja sasa.

Pia soma: Morogoro: Treni ya SGR (Dar-Dodoma) yakwama Kidete Kilosa kwa zaidi ya saa 4, sababu Hitilafu ya Umeme

Mmoja wa abiria aliyemo kwenye treni hiyo amesema:"Tumetoka vizuri tu Dodoma lakini tulipofika katikati ya Mkata na Moro stesheni ikiwa kama saa 4:33 usiku ikasimama ghafla hadi na kuzima kabisa, hadi sasa saa 5:33 usiku bado tupo hapa."

Mmoja wa wahariri, Peter Nyanje katika ukurasa wake wa Instagram ameandika:"Ni saa tano usiku tulitoka Dodoma kwenye uzinduzi wa SGR. Wakati tunakaribia station ya Morogoro treni imesimama ghafla njiani, air conditions zimezima, milango haifunguki. Tumekwama hapa sasa ni zaidi ya nusu saa. Tupo takribani watu 1,000 humu ndani."

Hata hivyo, ilipofika saa 5:35 usiku, treni hiyo ilianza safari.

Juhudi za kuupata uongozi wa Shikika la Reli Tanzania (TRC) zinaendelea.

Hayo yanajiri ikiwa zimepita siku mbili baada shirika hilo kuomba radhi kwa treni yake iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili kati ya stesheni ya Kilosa na Kidete mkoani Morogoro juzi tarehe 30 Julai 2024.

Pia soma: TRC yatolea ufanunuzi kuzimika kwa treni ya SGR Julai 30, 2024 katikati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete

“Taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system),” amesema.

Mwananchi
View attachment 3059048
Mtabaki mnawasingizia nyani tu bure. Kwa hizo treni zinatumia umeme tu hazina option b kwa imejensi kama hizo? Hawajui kuwa wanaharibu vyakula vya watu kwahiyo hujuma kwasasa ni nje nje?
 
kitu chochote kipya takes time to be perfect, hii ni train ya kwanza Africa mashariki na kati ya umeme yenye urefu huu; so its not an easy task mpaka ikaja kukaa sawa
kitu ukitolee hela alafu useme kipewe muda hizi kweli akili za bara la giza mpka hapo hujajua kwamba sgr imepigwa imetafunwa lini akili zitawakaa sawa...... toka tunaubuni mradi walitakowa wajue changamoto za mapema ni ni nini ipa kwakua tunavilaza kwenye uongozi na utendaji hawakusoma gap. leo mwananchi unakuja kutetea eti ya kwanza afrika mashariki na kati.

aliesema tz ni maiti hakukosea kabisa
 
Sasa jamani leo wa Tanzania tumekuwa tunajali muda, saa moja tumefanya big deal. Mbona kwenye ma bus tunasimama kila sehemu mara kwenye miti kujisaidia, chakula na mifoleni kikubwa tunafika salama. Lakini ukweli lazima tutoe muda unajuwa japo train imeanza rasmi lakini kwangu mimi tuko kwenye pre-commissioning kwa kuwa hatukufanya test muda wa kutosha kama standard kwa hiyo inafanyika lakini pia inahudumu. Hata hapo Airport delays zinatokea nyingi tu lakini safety first.
 
View attachment 3059049
Rais Samia akiwasalimia wananchi katika uzinduzi wa treni Agosti 1, 2024

Rais Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi amezindua rasmi huduma za usafiri wa reli ya kisasa (SGR), treni iliyokuwa imebeba wageni walioshiriki uzinduzi huo wakiwamo mabalozi na viongozi mbalimbali wa kiserikali kutokea mkoani Dodoma, imepata tena hitilafu karibu na Stesheni ya Morogoro kwa zaidi saa moja sasa.

Pia soma: Morogoro: Treni ya SGR (Dar-Dodoma) yakwama Kidete Kilosa kwa zaidi ya saa 4, sababu Hitilafu ya Umeme

Mmoja wa abiria aliyemo kwenye treni hiyo amesema:"Tumetoka vizuri tu Dodoma lakini tulipofika katikati ya Mkata na Moro stesheni ikiwa kama saa 4:33 usiku ikasimama ghafla hadi na kuzima kabisa, hadi sasa saa 5:33 usiku bado tupo hapa."

Mmoja wa wahariri, Peter Nyanje katika ukurasa wake wa Instagram ameandika:"Ni saa tano usiku tulitoka Dodoma kwenye uzinduzi wa SGR. Wakati tunakaribia station ya Morogoro treni imesimama ghafla njiani, air conditions zimezima, milango haifunguki. Tumekwama hapa sasa ni zaidi ya nusu saa. Tupo takribani watu 1,000 humu ndani."

Hata hivyo, ilipofika saa 5:35 usiku, treni hiyo ilianza safari.

Juhudi za kuupata uongozi wa Shikika la Reli Tanzania (TRC) zinaendelea.

Hayo yanajiri ikiwa zimepita siku mbili baada shirika hilo kuomba radhi kwa treni yake iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili kati ya stesheni ya Kilosa na Kidete mkoani Morogoro juzi tarehe 30 Julai 2024.

Pia soma: TRC yatolea ufanunuzi kuzimika kwa treni ya SGR Julai 30, 2024 katikati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete

“Taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system),” amesema.

Mwananchi
View attachment 3059048
Mwenye picha ikionesha waya zilizotandikwa juu ya reli naomba aiweje hapa, huku Dar waya zinaonekana zipo juu kwenye nguzo.
Hivi ni sayansi ya wapi ndege au mtu akining'inia kwenye waya mmoja bila kuugusa mwingine atasababisha umeme ukatike!
Huko nyuma tuliambiwa hata umeme ukikatika treni itaendelea kwenda kwa umeme mbadala, ni hatari kama milango haiwezi kufunguka huku viyoyozi vimezima.
 
Kuna taarifa sisizo rasmi kuwa

Treni ya umeme Dom-Dar yadaiwa kupata hitilafu, yakwama kwa muda.​

Je, ni bundi na Ngedere imesababisha hiyo hitilafu Tena?​

***
Treni ya reli ya umeme (SGR) kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam imedaiwa kukwama kwa muda mkoani Morogoro usiku wa Alhamisi Agosti 1, 2024.

Treni hiyo iliyokuwa imebeba abiria na wageni mbalimbali waliotoka kwenye uzinduzi wa huduma za SGR zilizofanyika mkoani Dodoma jana.

Mmoja wa abiria aliyekuwa katika chombo hicho ameiambia Mwananchi Digital kuwa safari ilianza bila changamoto mishale ya saa 2 usiku.

"Tumetoka vizuri tu Dodoma," anaeleza. "Lakini tulipofika katikati ya Stesheni ya Mkata na Moro ikiwa kama saa 4:33 usiku ikasimama ghafla na kuzima kabisa, hadi sasa saa 5:33 usiku bado tupo hapa."

Abiria Peter Nyanje, ambaye ni mhariri aliyeshiriki uzinduzi Dodoma, ameripoti changamoto hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, akiandika:

"Ni saa tano usiku tulitoka Dodoma kwenye uzinduzi wa SGR. Wakati tunakaribia station ya Morogoro treni imesimama ghafla njiani, air conditions zimezima, milango haifunguki. Tumekwama hapa sasa ni zaidi ya nusu saa. Tupo takribani watu 1,000 humu ndani."

Mwananchi haijathibitisha chanzo cha changamoto hiyo, wala idadi ya abiria waliokuwa kwenye treni kutoka kwa mamlaka husika.

Tunaendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuutafuta uongozi ama msemaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) ili kupata undani zaidi wa kilichojiri.
Hata hivyo, taarifa kutoka kwa abiria zinaonesha saa 5:35 usiku, treni hiyo ilifanikiwa kuendelea na safari yake mpaka Morogoro, kabla ya kuendelea kuelekea Dar es Salaam.

Hii haikuwa treni pekee iliyorejea Dar es Salaam jana ikiwa na wageni kutoka katika uzinduzi Dodoma.

Treni nyingine ya awali iliyoondoka Dodoma saa 1 usiku ikiwa na viongozi, wasanii na wadau mbalimbali, ilifanikiwa kufika Dar es Salaam bila changamoto.

"Tulitoka Dodoma saa 1 usiku tukasimama kushusha watu kwenye stesheni za Kilosa, Morogoro, Ngerengere na Pugu, tukaingia Dar es Salaam saa 5.32 usiku," anaeleza abiria aliyekuwa kwenye treni hiyo.

Anaeleza, "hakukuwa na changamoto zozote. Tulisubiri tu kwa dakika 25 hivi hapo Pugu ili kuipisha treni ya Dar-Dodoma."

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Samahanini niko Nje ya mada kidogo ndugu zangu naombeni miwape hii fursa pia mana inaweza kutusaidia sana

KAMA UNATUMIA TIGO NIBORA UTOE 40K ILA UOKOE HELA UNAZONUNUA DATA&DK KWA MIAKA MIWILI (GB48 KILA MWEZ+DK 2000)📌

Watumiaji wa t!go njoo nikuunge huduma hii uwe unapewa gb 48 na dk 2000 kila mwezi kwa miaka miwili, huduma hii sahivi unaungwa pekeyako na sio kikundi (pia kuna Gb35 kwa sh. 30000 na gb 30 kwa sh.25000)

Uhakika na usalama wapesa yako ni 100% mana hela unailipa direct T!go kama unavyojiunga na vifurushi vingine, mm nakupa maelekezo tu ya kujiunga, (ukijiunga nalipwa na t!go).

kama ukitaka kujiridhisha nikishakupa maelekezo unaweza kupiga 100 uulizie ujiridhishe kabla ya kulipia.

HUNITUMII HELA YOYOTE HATA MIA!

Karibu hata mitandao ya halotel voda na Airtel uniulizie tu nikupe maelekezo bure!

0717700921
Ngoja nitakuseach hewani soon.........ngoja niteremke kwenye gari🚌
 
I told you guys, Nchi maskini ku opt expensive project using high technology tena za kusubiria mfundishwe na Wazungu haya ndio madhara yake.

Kama tungekuwa tumejenga Barabara km 6,000 Sasa hivi tungekuwa tumevuna Uchumi mkubwa sana ambao ungewezesha kusomesha watu Wetu na kujenga Sgr bila pressure yeyote kuanzia mwaka 2030 huko.

Hela zimepotea na ki sgr chenu kitaendelea kusumbua Hadi mkome

View: https://twitter.com/Mwanahalisitz/status/1819110185480474692?t=_qVsO48V6sF8D4m2t00mgA&s=19
 
1722564494610.png
 
Ni wakati sahihi ngedere na bundi kukamatwa ili wasaidie uchunguzi.

NB; Uongozi wa TRC watoe taarifa ya ukweli kuhusu yanayojiri na kuzimika kwa injini za treni. Wasisahau kuja na suluhu ya muda mrefu. Kuja na vistori vya kitoto na uongo havitawasaidia.
 
Back
Top Bottom