Treni ya Umeme yatumia dakika 114 Dar hadi Morogoro, Wananchi 600 wasafiri

Treni ya Umeme yatumia dakika 114 Dar hadi Morogoro, Wananchi 600 wasafiri

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Safari ilianza Saa 12:01 na kufika Morogoro Saa 1:55

Hongera Rais Samia. Hongera Dr Mpango. RIP Shujaa Magufuli

========

Ilikuwa safari ya dakika 114 zenye bashasha, abiria zaidi ya 600 wakiwa kwenye mabehewa 14 ya treni ya umeme iliyoanza safari ya kwanza leo Juni 14, 2024 ikiongozwa na nahodha, Ahazi Mfupa. Treni iliondoka Dar es Salaam saa 12:01 asubuhi na kuwasili Morogoro saa 1:55 asubuhi.

Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema safari hiyo imehusisha mabehewa 14, matatu yakiwa ya daraja la juu.

"Tumekuja na abiria kama 600 hadi 700, mabehewa mengi yalikuwa yamejaa, ingawa hadi yote 14 yajae tungefika 1,000," amesema Kadogosa katika mahojiano na Mwananchi Digital.

Safari ilivyokuwa
Katika stesheni ya SGR Dar es Salaam, abiria walianza kuwasili saa 11.00 asubuhi. Kila aliyesafiri kabla ya kuingia ndani treni alikaguliwa kwa kutumia skana. Ilipofika saa 11.30 asubuhi, kulitolewa tangazo kuwataka abiria wanaosafiri waendelee kuingia ndani ya treni.

Matangazo yaliendelea hadi dakika tano kabla ya safari kuanza. Ilipofika saa 12.01 asubuhi treni ilianza safari kuelekea Morogoro. Ilipofika Kituo cha Pugu, ilisimama kwa dakika mbili na kupakia abiria wachache waliokuwa kituoni hapo. Mbali na kituo hicho, pia ilisimama kwa dakika mbili kwenye vituo vya Soga na Ngerengere kabla ya kuwasili stesheni ya Kihonda.

Tofauti na wakati wa safari ya majaribio Februari 27, 2024 iliyotumia saa 2.20, leo ikiwa ni safari ya kwanza ya abiria treni hiyo imetumia saa 1:55 kufika Morogoro.

Ukataji tiketi
Maswali ya wengi ilikuwa ni namna ya kukata tiketi. Kadogosa amesema abiria anaweza kukata kwa njia ya mtandao au dirishani kwenye ofisi za TRC. Japo kulikuwa na sintofahamu ya nauli, Kadogosa amesema Sh13,000 kwa daraja la kawaida ni nauli rafiki. "Hii ni treni ya Watanzania, zimewekwa nauli rafiki watu kuzimudu," amesema.

Baadhi ya abiria wakiwa ndani ya treni iliyoanza safari ya kwanza kutoka Jijini Dar es Salaam kwenda Morogoro.

Vyakula, vinywaji marufuku
Katika usafiri huo, hairuhusiwi kuingia na kinywaji chochote wala chakula. Mmoja wa wahudumu katika treni hiyo, Zuhura Milala amesema kila kitu kinapatikana ndani ya treni na kwenye stesheni. Japo katika safari ya leo, waliotumia vinywaji walikuwa wachache, ikielezwa huenda ni kutokana na wengi kutokuhitaji kutokana na muda waliosafiri na mabehewa mengi hakuna aliyeulizia.

Nahodha afunguka
Nahodha aliyeendesha treni hiyo, Ahazi Mfupa amesema hakuwa anafahamu kama yeye ndiye atakayekabidhiwa jukumu hilo hadi siku chache kabla ya safari. "Tuko manahodha waandamizi wengi, nilichaguliwa mimi na mwenzangu mmoja kuendesha treni hii, nashukuru Mungu safari yetu imekuwa nzuri na tumefika kwa muda tulioutarajia," amesema.

Mfupa amesema wametembea kwa mwendo wa juu wa kilomita 155 kwa saa ingawa treni hiyo uwezo wake wa juu ni kilomita 160 kwa saa.

Walichosema abiria
Wakizungumzia usafiri huo, baadhi ya abiria wamesema imekuwa na mwanzo mzuri. "Huduma tuliyoipata leo ikiwa endelevu ni usafiri mzuri, maana abiria unafika unapokewa vizuri na kila hatua ya safari mnaelezwa," amesema Noela Alphonce, mkazi wa Dar es Salaam.

Abiria mwingine, Albert John amesema aliposikia treni inaanza safari leo, aliamua kukata tiketi na kusafiri.
"Sikutaka nisimuliwe, nimeamua kutumia tu pesa yangu kuja na kurudi ili nijionee mwenyewe usafiri huu ulivyo," amesema.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile aliwahimiza Watanzania kutumia vema usafiri huo kwa usafi na ulinzi kwa kuwa ni kitu chao.
 
Kwa nauli ya Tsh 13,000/= kwa kichwa, watu 600 inamaanisha wamepata Tsh Mil 7.8 kwa kwenda tu.
Kadogosa: Tumetumia umeme wa 336,000 kwenda na kurudi Dar - Morogoro

Kwa kusikiliza hii kauli, walitumia umeme wa Tsh Laki 3.5 kwenda na kurudi Dar to Moro. Tuweke factors zote, tu-assume watumie wa Laki 4 kwenda tu, inamaana Mil 7.4 faida.

Toa gharama zote za service, sijui itazidi Tsh ngapi ila najua kwakua chuma mpya haina matumizi makubwa kwenye service, na toa posho ya wafanyakazi.

Inamaana chuma inaingiza zaidi ya Mil 5 kwa safari.

According to TRC wamesema kwa siku itakua inapiga route nne.

trc.png


Kwahiyo ni Mil 20+ faida iyo. Tumetoa matumizi.

Tusubiri waseme wanaendesha kwa hasara.
 
Safari ilianza Saa 12:01 na kufika Morogoro Saa 1:55

Hongera Rais Samia

Hongera Dr Mpango

RIP Shujaa Magufuli

Credit; Mwananchi
Hakuna cha kuwapongeza, tuliwaajili wafanye hayo. chawa mkubwa we 😀 😀 😀 😀
Pili, masaa mawili km 192 km ni muda mwingi sana. Ulaya ni 300km/hr. Ilibidi iwe less tha an hour. Bado waliiba hela wakaleta mikweche.,
 
Hakuna cha kuwapongeza, tuliwaajili wafanye hayo. chawa mkubwa we 😀 😀 😀 😀
Pili, masaa mawili km 192 km ni muda mwingi sana. Ulaya ni 300km/hr. Ilibidi iwe less tha an hour. Bado waliiba hela wakaleta mikweche.,
Kuna treni za umeme aina nyingi. Ukitaka ya km 200/hr zipo, ukitaka km 300/hr zipo. Sisi ni Km 150/hr hadi 180km/hr. Sababu ni aina ya treni tulizo oda ni za KM chini ya 200, pia dizaini ya Miundombinu kwenye reli ni ya Km 200 tu. Tukitaka km 200 hadi 300 inawezekana kwa kuoda bullet treni kutoka Ulaya, China au Japan, pia kubadili Vitu vichache kwenye miundimbinu ya reli.
 
Pongezi kwa mama tu.
Weee unainamishwa sio bure! Unajua JPM pressure na vikwazo vya ndani na nje alivyopambana navyo katika miradi mikuu mitatu? SGR, Nyerere Hydro, na kuhamisha serikali Dodoma? Mama anachofanya ni kupiga hela tu hawa wakandarasi wanabadilisha terms of reference na kusema mradi ulikuwa wa kiasi cha juu mara 2 ya kile cha JPM alafu Mama anaidhinisha na Abdul mwanae kuweka kibindoni 10%
 
Mimi shukrani zangu za kipekee nazipeleka kwa Watanzania wote walipa kodi.

Watumishi wa umma nadhani wanakumbuka sana kipindi hicho waliponyimwa baadhi ya stahiki zao za msingi ili tu hiyo reli iweze kujengwa, ndege ziweze kununuliwa, na piwa bwawa la umeme liweze kujengwa.
 
Hakuna cha kuwapongeza, tuliwaajili wafanye hayo. chawa mkubwa we 😀 😀 😀 😀
Pili, masaa mawili km 192 km ni muda mwingi sana. Ulaya ni 300km/hr. Ilibidi iwe less tha an hour. Bado waliiba hela wakaleta mikweche.,
Hizo za 300km/hr hazipiti maporini kwenye mbunga. Zinapita kwenye mega cities kuunganisha hubs, na zina miundombinu ya bei mbaya. Kwanza ni ama ziwe kwa ndani au zijengewe reli ya daraja. Sasa imagine ujenge reli ya juu kuanzia City Center mpaka Dodoma. Kwa bajeti ipi
 
Back
Top Bottom