Treni ya Umeme yatumia dakika 114 Dar hadi Morogoro, Wananchi 600 wasafiri

Safari ilianza Saa 12:01 na kufika Morogoro Saa 1:55

Hongera Rais Samia. Hongera Dr Mpango. RIP Shujaa Magufuli

========

Ilikuwa safari ya dakika 114 zenye bashasha, abiria zaidi ya 600 wakiwa kwenye mabehewa 14 ya treni ya umeme iliyoanza safari ya kwanza leo Juni 14, 2024 ikiongozwa na nahodha, Ahazi Mfupa. Treni iliondoka Dar es Salaam saa 12:01 asubuhi na kuwasili Morogoro saa 1:55 asubuhi.

Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema safari hiyo imehusisha mabehewa 14, matatu yakiwa ya daraja la juu.

"Tumekuja na abiria kama 600 hadi 700, mabehewa mengi yalikuwa yamejaa, ingawa hadi yote 14 yajae tungefika 1,000," amesema Kadogosa katika mahojiano na Mwananchi Digital.

Safari ilivyokuwa
Katika stesheni ya SGR Dar es Salaam, abiria walianza kuwasili saa 11.00 asubuhi. Kila aliyesafiri kabla ya kuingia ndani treni alikaguliwa kwa kutumia skana. Ilipofika saa 11.30 asubuhi, kulitolewa tangazo kuwataka abiria wanaosafiri waendelee kuingia ndani ya treni.

Matangazo yaliendelea hadi dakika tano kabla ya safari kuanza. Ilipofika saa 12.01 asubuhi treni ilianza safari kuelekea Morogoro. Ilipofika Kituo cha Pugu, ilisimama kwa dakika mbili na kupakia abiria wachache waliokuwa kituoni hapo. Mbali na kituo hicho, pia ilisimama kwa dakika mbili kwenye vituo vya Soga na Ngerengere kabla ya kuwasili stesheni ya Kihonda.

Tofauti na wakati wa safari ya majaribio Februari 27, 2024 iliyotumia saa 2.20, leo ikiwa ni safari ya kwanza ya abiria treni hiyo imetumia saa 1:55 kufika Morogoro.

Ukataji tiketi
Maswali ya wengi ilikuwa ni namna ya kukata tiketi. Kadogosa amesema abiria anaweza kukata kwa njia ya mtandao au dirishani kwenye ofisi za TRC. Japo kulikuwa na sintofahamu ya nauli, Kadogosa amesema Sh13,000 kwa daraja la kawaida ni nauli rafiki. "Hii ni treni ya Watanzania, zimewekwa nauli rafiki watu kuzimudu," amesema.

Baadhi ya abiria wakiwa ndani ya treni iliyoanza safari ya kwanza kutoka Jijini Dar es Salaam kwenda Morogoro.

Vyakula, vinywaji marufuku
Katika usafiri huo, hairuhusiwi kuingia na kinywaji chochote wala chakula. Mmoja wa wahudumu katika treni hiyo, Zuhura Milala amesema kila kitu kinapatikana ndani ya treni na kwenye stesheni. Japo katika safari ya leo, waliotumia vinywaji walikuwa wachache, ikielezwa huenda ni kutokana na wengi kutokuhitaji kutokana na muda waliosafiri na mabehewa mengi hakuna aliyeulizia.

Nahodha afunguka
Nahodha aliyeendesha treni hiyo, Ahazi Mfupa amesema hakuwa anafahamu kama yeye ndiye atakayekabidhiwa jukumu hilo hadi siku chache kabla ya safari. "Tuko manahodha waandamizi wengi, nilichaguliwa mimi na mwenzangu mmoja kuendesha treni hii, nashukuru Mungu safari yetu imekuwa nzuri na tumefika kwa muda tulioutarajia," amesema.

Mfupa amesema wametembea kwa mwendo wa juu wa kilomita 155 kwa saa ingawa treni hiyo uwezo wake wa juu ni kilomita 160 kwa saa.

Walichosema abiria
Wakizungumzia usafiri huo, baadhi ya abiria wamesema imekuwa na mwanzo mzuri. "Huduma tuliyoipata leo ikiwa endelevu ni usafiri mzuri, maana abiria unafika unapokewa vizuri na kila hatua ya safari mnaelezwa," amesema Noela Alphonce, mkazi wa Dar es Salaam.

Abiria mwingine, Albert John amesema aliposikia treni inaanza safari leo, aliamua kukata tiketi na kusafiri.
"Sikutaka nisimuliwe, nimeamua kutumia tu pesa yangu kuja na kurudi ili nijionee mwenyewe usafiri huu ulivyo," amesema.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile aliwahimiza Watanzania kutumia vema usafiri huo kwa usafi na ulinzi kwa kuwa ni kitu chao.
ii ndiyo Tanzania yetu siku zijazo uenda tukaifulaia nchi yetu
 
Kwa nauli ya Tsh 13,000/= kwa kichwa, watu 600 inamaanisha wamepata Tsh Mil 7.8 kwa kwenda tu.
Kadogosa: Tumetumia umeme wa 336,000 kwenda na kurudi Dar - Morogoro

Kwa kusikiliza hii kauli, walitumia umeme wa Tsh Laki 3.5 kwenda na kurudi Dar to Moro. Tuweke factors zote, tu-assume watumie wa Laki 4 kwenda tu, inamaana Mil 7.4 faida.

Toa gharama zote za service, sijui itazidi Tsh ngapi ila najua kwakua chuma mpya haina matumizi makubwa kwenye service, na toa posho ya wafanyakazi.

Inamaana chuma inaingiza zaidi ya Mil 5 kwa safari.

According to TRC wamesema kwa siku itakua inapiga route nne.

View attachment 3017294

Kwahiyo ni Mil 20+ faida iyo. Tumetoa matumizi.

Tusubiri waseme wanaendesha kwa hasara.
Bado gharama za mizigo
 
Mbona ratiba imekaa kiduwanzi hivyo tuliambiwa tutakuwa tunaishi Dodoma na kufanya kazi Dodoma au Kuishi Dar kufanya kazi Dodoma Siasa ni ushatani
 
Pongezi kwa mama tu.
Ajabu gani hii? Huu uchawa wa nchi hii utatuweka pabaya. Anayestahili pongezi ni dereva wa hii treni ya umeme ambaye ameweka rekodi yake ya kwanza kwa kuendesha treni ya umeme kwa kasi ya kilometer 155 kwa saa, siamini kuwa hiyo treni imeendeshwa na samia siku ya leo. 🤔
 
Weka na gharama za manunuzi mpaka ilipofikia kuanza safari.

Haupigi hesabu ya mradi kwa gharama za kuuendesha safai moja tu.

Weka na hesabu ya Watanzaniawajinga walichoharibu na kuvunja katika hiyo safari.
Enh ushazeeka na meno huna eti
 
Safari ilianza Saa 12:01 na kufika Morogoro Saa 1:55

Hongera Rais Samia. Hongera Dr Mpango. RIP Shujaa Magufuli

========

Ilikuwa safari ya dakika 114 zenye bashasha, abiria zaidi ya 600 wakiwa kwenye mabehewa 14 ya treni ya umeme iliyoanza safari ya kwanza leo Juni 14, 2024 ikiongozwa na nahodha, Ahazi Mfupa. Treni iliondoka Dar es Salaam saa 12:01 asubuhi na kuwasili Morogoro saa 1:55 asubuhi.

Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema safari hiyo imehusisha mabehewa 14, matatu yakiwa ya daraja la juu.

"Tumekuja na abiria kama 600 hadi 700, mabehewa mengi yalikuwa yamejaa, ingawa hadi yote 14 yajae tungefika 1,000," amesema Kadogosa katika mahojiano na Mwananchi Digital.

Safari ilivyokuwa
Katika stesheni ya SGR Dar es Salaam, abiria walianza kuwasili saa 11.00 asubuhi. Kila aliyesafiri kabla ya kuingia ndani treni alikaguliwa kwa kutumia skana. Ilipofika saa 11.30 asubuhi, kulitolewa tangazo kuwataka abiria wanaosafiri waendelee kuingia ndani ya treni.

Matangazo yaliendelea hadi dakika tano kabla ya safari kuanza. Ilipofika saa 12.01 asubuhi treni ilianza safari kuelekea Morogoro. Ilipofika Kituo cha Pugu, ilisimama kwa dakika mbili na kupakia abiria wachache waliokuwa kituoni hapo. Mbali na kituo hicho, pia ilisimama kwa dakika mbili kwenye vituo vya Soga na Ngerengere kabla ya kuwasili stesheni ya Kihonda.

Tofauti na wakati wa safari ya majaribio Februari 27, 2024 iliyotumia saa 2.20, leo ikiwa ni safari ya kwanza ya abiria treni hiyo imetumia saa 1:55 kufika Morogoro.

Ukataji tiketi
Maswali ya wengi ilikuwa ni namna ya kukata tiketi. Kadogosa amesema abiria anaweza kukata kwa njia ya mtandao au dirishani kwenye ofisi za TRC. Japo kulikuwa na sintofahamu ya nauli, Kadogosa amesema Sh13,000 kwa daraja la kawaida ni nauli rafiki. "Hii ni treni ya Watanzania, zimewekwa nauli rafiki watu kuzimudu," amesema.

Baadhi ya abiria wakiwa ndani ya treni iliyoanza safari ya kwanza kutoka Jijini Dar es Salaam kwenda Morogoro.

Vyakula, vinywaji marufuku
Katika usafiri huo, hairuhusiwi kuingia na kinywaji chochote wala chakula. Mmoja wa wahudumu katika treni hiyo, Zuhura Milala amesema kila kitu kinapatikana ndani ya treni na kwenye stesheni. Japo katika safari ya leo, waliotumia vinywaji walikuwa wachache, ikielezwa huenda ni kutokana na wengi kutokuhitaji kutokana na muda waliosafiri na mabehewa mengi hakuna aliyeulizia.

Nahodha afunguka
Nahodha aliyeendesha treni hiyo, Ahazi Mfupa amesema hakuwa anafahamu kama yeye ndiye atakayekabidhiwa jukumu hilo hadi siku chache kabla ya safari. "Tuko manahodha waandamizi wengi, nilichaguliwa mimi na mwenzangu mmoja kuendesha treni hii, nashukuru Mungu safari yetu imekuwa nzuri na tumefika kwa muda tulioutarajia," amesema.

Mfupa amesema wametembea kwa mwendo wa juu wa kilomita 155 kwa saa ingawa treni hiyo uwezo wake wa juu ni kilomita 160 kwa saa.

Walichosema abiria
Wakizungumzia usafiri huo, baadhi ya abiria wamesema imekuwa na mwanzo mzuri. "Huduma tuliyoipata leo ikiwa endelevu ni usafiri mzuri, maana abiria unafika unapokewa vizuri na kila hatua ya safari mnaelezwa," amesema Noela Alphonce, mkazi wa Dar es Salaam.

Abiria mwingine, Albert John amesema aliposikia treni inaanza safari leo, aliamua kukata tiketi na kusafiri.
"Sikutaka nisimuliwe, nimeamua kutumia tu pesa yangu kuja na kurudi ili nijionee mwenyewe usafiri huu ulivyo," amesema.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile aliwahimiza Watanzania kutumia vema usafiri huo kwa usafi na ulinzi kwa kuwa ni kitu chao.

Treni imetumie pesa nyingi . Serikali msipoteze muda kila siku kupandisha watu wa PR na machawa kwenye treni hii ni biashara na wekezaji tayari ni mkubwa
 
Duh.. wajukuu wa Taqiyya hawa... hata ukitumia bodaboda hutumii masaa mengi kihivyo
We jamaa mbona unapendaga ubishani wa kitoto!?
Dar to Moro 194kms.
Gari inaruhusiwa kutembea speed ya 60km/hr hujajumlisha foleni pia hujajumlisha kusimama vituo vidogo kama Mlandizi,Chalinze,Kingolwira,Mikese.
Una ubishani wa kipumbavu sana.
Kwa bas Dar mpaka Moro ni masaa 5 ama 6 kasoro.
 
tulihitaji treni ya 300km/hr, hapo ndipo tungelikuwa tumefanya jambo la maana sana, ila always upeo wetu ni mdogo sana
 
Abiria 600 sawa na basi 10..utawala wa wale waarabu wa pale Morogoro unaenda kwisha..na ndio maana huu mradi ulikuwa unapigwa sana vita

Mkuu Hao waarabu wana hela za kutosha hawendi kuyamba kabisa, hivi sasa tayari wameshabuni miradi mengie ya ku replace huyi biashara
 
kwenda zako mama ana vision gani? hii ni vision za magufuli na aliyekua waziri wake wa fedha ndio huyo sasa makamu wa rais . Mtu mwenye akili kuruhusu watendaji wa umma wale kwa refu wa kamba zao nini cha umma anaweza kufanikisha zaidi ya kupeleka mablioni ya umma mikoani yakaliwe na watendaji fisadi.

Huyo unaemwita mwenye akili alikuwa anajilia yeye tu na genge lake
 
Kwa hili la hii reli ya SGR hakika Serikali inahitaji PONGEZI, cha msingi sasa iwepo MANAGEMENT iliyo bora na thabiti ili MRADI huu ulete TIJA iliyokusudiwa..naamini wapo Watanzania wanaoweza kusimamia MRADI huu vizuri kabisa ILA ikishindikana sio vibaya tukaangalia hata nje

Ngoja sasa mwisho wa Mwezi huu, niwahi Ruvu chap, nikapate hata ekari 20, najua SOGA nimeshachelewa
 
Back
Top Bottom