Lumbi9
JF-Expert Member
- Oct 12, 2014
- 8,666
- 12,178
Bus gani linaenda moro kwa hela hiyo, abood nauli 1310,000
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bus gani linaenda moro kwa hela hiyo, abood nauli 1310,000
Ni karibia masaa mawili, nilitarajia itumie dakika 60 tu
Yes treni yetu mkuu inauwezo wa kufika hapo lakini wameona kwa ajili ya usalama wa miundo mbinu iwekwe hiyo 160
Hatutaki wauaji.Vision ya Magufuli kweli tunahitaji rais mwingine mwenye vision ya Hali ya juu kuhusu Nchi.
Sijaelewa, inapokwepa inakuwa inazunguka, sasa inakuwaje fupi?Njia ya Treni na bus ni tofauti. Kwa Barabara toka Dar hadi Morogoro (Msamvu) ni Km 200(194). Kwa njia ya Treni Dar hadi Morogoro ni Km 300. Treni hukwepa sana miinuko ndio maana njia yake ni ni fupi.
Hongera watanzania kwa kulipa kodi 😳🤠Safari ilianza Saa 12:01 na kufika Morogoro Saa 1:55
Hongera Rais Samia. Hongera Dr Mpango. RIP Shujaa Magufuli
========
Ilikuwa safari ya dakika 114 zenye bashasha, abiria zaidi ya 600 wakiwa kwenye mabehewa 14 ya treni ya umeme iliyoanza safari ya kwanza leo Juni 14, 2024 ikiongozwa na nahodha, Ahazi Mfupa. Treni iliondoka Dar es Salaam saa 12:01 asubuhi na kuwasili Morogoro saa 1:55 asubuhi.
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema safari hiyo imehusisha mabehewa 14, matatu yakiwa ya daraja la juu.
"Tumekuja na abiria kama 600 hadi 700, mabehewa mengi yalikuwa yamejaa, ingawa hadi yote 14 yajae tungefika 1,000," amesema Kadogosa katika mahojiano na Mwananchi Digital.
Safari ilivyokuwa
Katika stesheni ya SGR Dar es Salaam, abiria walianza kuwasili saa 11.00 asubuhi. Kila aliyesafiri kabla ya kuingia ndani treni alikaguliwa kwa kutumia skana. Ilipofika saa 11.30 asubuhi, kulitolewa tangazo kuwataka abiria wanaosafiri waendelee kuingia ndani ya treni.
Matangazo yaliendelea hadi dakika tano kabla ya safari kuanza. Ilipofika saa 12.01 asubuhi treni ilianza safari kuelekea Morogoro. Ilipofika Kituo cha Pugu, ilisimama kwa dakika mbili na kupakia abiria wachache waliokuwa kituoni hapo. Mbali na kituo hicho, pia ilisimama kwa dakika mbili kwenye vituo vya Soga na Ngerengere kabla ya kuwasili stesheni ya Kihonda.
Tofauti na wakati wa safari ya majaribio Februari 27, 2024 iliyotumia saa 2.20, leo ikiwa ni safari ya kwanza ya abiria treni hiyo imetumia saa 1:55 kufika Morogoro.
Ukataji tiketi
Maswali ya wengi ilikuwa ni namna ya kukata tiketi. Kadogosa amesema abiria anaweza kukata kwa njia ya mtandao au dirishani kwenye ofisi za TRC. Japo kulikuwa na sintofahamu ya nauli, Kadogosa amesema Sh13,000 kwa daraja la kawaida ni nauli rafiki. "Hii ni treni ya Watanzania, zimewekwa nauli rafiki watu kuzimudu," amesema.
Baadhi ya abiria wakiwa ndani ya treni iliyoanza safari ya kwanza kutoka Jijini Dar es Salaam kwenda Morogoro.
Vyakula, vinywaji marufuku
Katika usafiri huo, hairuhusiwi kuingia na kinywaji chochote wala chakula. Mmoja wa wahudumu katika treni hiyo, Zuhura Milala amesema kila kitu kinapatikana ndani ya treni na kwenye stesheni. Japo katika safari ya leo, waliotumia vinywaji walikuwa wachache, ikielezwa huenda ni kutokana na wengi kutokuhitaji kutokana na muda waliosafiri na mabehewa mengi hakuna aliyeulizia.
Nahodha afunguka
Nahodha aliyeendesha treni hiyo, Ahazi Mfupa amesema hakuwa anafahamu kama yeye ndiye atakayekabidhiwa jukumu hilo hadi siku chache kabla ya safari. "Tuko manahodha waandamizi wengi, nilichaguliwa mimi na mwenzangu mmoja kuendesha treni hii, nashukuru Mungu safari yetu imekuwa nzuri na tumefika kwa muda tulioutarajia," amesema.
Mfupa amesema wametembea kwa mwendo wa juu wa kilomita 155 kwa saa ingawa treni hiyo uwezo wake wa juu ni kilomita 160 kwa saa.
Walichosema abiria
Wakizungumzia usafiri huo, baadhi ya abiria wamesema imekuwa na mwanzo mzuri. "Huduma tuliyoipata leo ikiwa endelevu ni usafiri mzuri, maana abiria unafika unapokewa vizuri na kila hatua ya safari mnaelezwa," amesema Noela Alphonce, mkazi wa Dar es Salaam.
Abiria mwingine, Albert John amesema aliposikia treni inaanza safari leo, aliamua kukata tiketi na kusafiri.
"Sikutaka nisimuliwe, nimeamua kutumia tu pesa yangu kuja na kurudi ili nijionee mwenyewe usafiri huu ulivyo," amesema.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile aliwahimiza Watanzania kutumia vema usafiri huo kwa usafi na ulinzi kwa kuwa ni kitu chao.
Ni mwendo wa Gari tu.Masaa 2 hayo 😂😂
Hata kama unamchukia mtu sio kwa kiasi hicho kill uongozi utasifiwa kwa mazuri yake na utakosolewa kwa mabaya yake Acha ROHO YA WIVUWewe punguani kweli na hii ni matokea ya ushamba na kutosafiri.
Yaani kujenga Sgr sijui madaraja ndio visio? Unajua maana ya vision kweli wewe msukule wa Mwendazake?
Jibu swali, kujenga Sgr ndio visio?Hata kama unamchukia mtu sio kwa kiasi hicho kill uongozi utasifiwa kwa mazuri yake na utakosolewa kwa mabaya yake Acha ROHO YA WIVU
AMetumia mshahara wake kujenga?Pongezi kwa mama tu.
zuna uhakika alisema? au unawaza kwa kutumia utumbo mpana?Hapa alizingua jamaa yetu Lissu ila nna uhakika lissu anatakiwa kuangaliwa kiwango chake cha Akili kama bado kiko sawa baada ya lile shambulio la Risasi.
Mwakani tutawaleteeni ripoti mtaona hasara yake.[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]Kwa nauli ya Tsh 13,000/= kwa kichwa, watu 600 inamaanisha wamepata Tsh Mil 7.8 kwa kwenda tu.
Kadogosa: Tumetumia umeme wa 336,000 kwenda na kurudi Dar - Morogoro
Kwa kusikiliza hii kauli, walitumia umeme wa Tsh Laki 3.5 kwenda na kurudi Dar to Moro. Tuweke factors zote, tu-assume watumie wa Laki 4 kwenda tu, inamaana Mil 7.4 faida.
Toa gharama zote za service, sijui itazidi Tsh ngapi ila najua kwakua chuma mpya haina matumizi makubwa kwenye service, na toa posho ya wafanyakazi.
Inamaana chuma inaingiza zaidi ya Mil 5 kwa safari.
According to TRC wamesema kwa siku itakua inapiga route nne.
View attachment 3017294
Kwahiyo ni Mil 20+ faida iyo. Tumetoa matumizi.
Tusubiri waseme wanaendesha kwa hasara.