Treni ya Umeme yatumia dakika 114 Dar hadi Morogoro, Wananchi 600 wasafiri

Njia ya Treni na bus ni tofauti. Kwa Barabara toka Dar hadi Morogoro (Msamvu) ni Km 200(194). Kwa njia ya Treni Dar hadi Morogoro ni Km 300. Treni hukwepa sana miinuko ndio maana njia yake ni ni fupi.
YAANI WEWE HUNA HABARI HII NJIA YA SGR IMEPASUA MIINUKO???
 
Wewe punguani kweli na hii ni matokea ya ushamba na kutosafiri.

Yaani kujenga Sgr sijui madaraja ndio visio? Unajua maana ya vision kweli wewe msukule wa Mwendazake?
We chawa wa mama Jiwe alikufanyaje mbona huwa hutaki kumsikia kabisa? Ni cheti fake au ulikuwa unakula salary ya serikali wakati umehamia CWT akakufunga!
 
Safari ilianza Saa 12:01 na kufika Morogoro Saa 1:55

Hongera Rais Samia. Hongera Dr Mpango. RIP Shujaa Magufuli

========

Ilikuwa safari ya dakika 114 zenye bashasha, abiria zaidi ya 600 wakiwa kwenye mabehewa 14 ya treni ya umeme iliyoanza safari ya kwanza leo Juni 14, 2024 ikiongozwa na nahodha, Ahazi Mfupa. Treni iliondoka Dar es Salaam saa 12:01 asubuhi na kuwasili Morogoro saa 1:55 asubuhi.

Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema safari hiyo imehusisha mabehewa 14, matatu yakiwa ya daraja la juu.

"Tumekuja na abiria kama 600 hadi 700, mabehewa mengi yalikuwa yamejaa, ingawa hadi yote 14 yajae tungefika 1,000," amesema Kadogosa katika mahojiano na Mwananchi Digital.

Safari ilivyokuwa
Katika stesheni ya SGR Dar es Salaam, abiria walianza kuwasili saa 11.00 asubuhi. Kila aliyesafiri kabla ya kuingia ndani treni alikaguliwa kwa kutumia skana. Ilipofika saa 11.30 asubuhi, kulitolewa tangazo kuwataka abiria wanaosafiri waendelee kuingia ndani ya treni.

Matangazo yaliendelea hadi dakika tano kabla ya safari kuanza. Ilipofika saa 12.01 asubuhi treni ilianza safari kuelekea Morogoro. Ilipofika Kituo cha Pugu, ilisimama kwa dakika mbili na kupakia abiria wachache waliokuwa kituoni hapo. Mbali na kituo hicho, pia ilisimama kwa dakika mbili kwenye vituo vya Soga na Ngerengere kabla ya kuwasili stesheni ya Kihonda.

Tofauti na wakati wa safari ya majaribio Februari 27, 2024 iliyotumia saa 2.20, leo ikiwa ni safari ya kwanza ya abiria treni hiyo imetumia saa 1:55 kufika Morogoro.

Ukataji tiketi
Maswali ya wengi ilikuwa ni namna ya kukata tiketi. Kadogosa amesema abiria anaweza kukata kwa njia ya mtandao au dirishani kwenye ofisi za TRC. Japo kulikuwa na sintofahamu ya nauli, Kadogosa amesema Sh13,000 kwa daraja la kawaida ni nauli rafiki. "Hii ni treni ya Watanzania, zimewekwa nauli rafiki watu kuzimudu," amesema.

Baadhi ya abiria wakiwa ndani ya treni iliyoanza safari ya kwanza kutoka Jijini Dar es Salaam kwenda Morogoro.

Vyakula, vinywaji marufuku
Katika usafiri huo, hairuhusiwi kuingia na kinywaji chochote wala chakula. Mmoja wa wahudumu katika treni hiyo, Zuhura Milala amesema kila kitu kinapatikana ndani ya treni na kwenye stesheni. Japo katika safari ya leo, waliotumia vinywaji walikuwa wachache, ikielezwa huenda ni kutokana na wengi kutokuhitaji kutokana na muda waliosafiri na mabehewa mengi hakuna aliyeulizia.

Nahodha afunguka
Nahodha aliyeendesha treni hiyo, Ahazi Mfupa amesema hakuwa anafahamu kama yeye ndiye atakayekabidhiwa jukumu hilo hadi siku chache kabla ya safari. "Tuko manahodha waandamizi wengi, nilichaguliwa mimi na mwenzangu mmoja kuendesha treni hii, nashukuru Mungu safari yetu imekuwa nzuri na tumefika kwa muda tulioutarajia," amesema.

Mfupa amesema wametembea kwa mwendo wa juu wa kilomita 155 kwa saa ingawa treni hiyo uwezo wake wa juu ni kilomita 160 kwa saa.

Walichosema abiria
Wakizungumzia usafiri huo, baadhi ya abiria wamesema imekuwa na mwanzo mzuri. "Huduma tuliyoipata leo ikiwa endelevu ni usafiri mzuri, maana abiria unafika unapokewa vizuri na kila hatua ya safari mnaelezwa," amesema Noela Alphonce, mkazi wa Dar es Salaam.

Abiria mwingine, Albert John amesema aliposikia treni inaanza safari leo, aliamua kukata tiketi na kusafiri.
"Sikutaka nisimuliwe, nimeamua kutumia tu pesa yangu kuja na kurudi ili nijionee mwenyewe usafiri huu ulivyo," amesema.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile aliwahimiza Watanzania kutumia vema usafiri huo kwa usafi na ulinzi kwa kuwa ni kitu chao.
Shida muendelezo.
 
Saa 1 ingependeza zaidi!
 
Kwa nauli ya Tsh 13,000/= kwa kichwa, watu 600 inamaanisha wamepata Tsh Mil 7.8 kwa kwenda tu.
Kadogosa: Tumetumia umeme wa 336,000 kwenda na kurudi Dar - Morogoro

Kwa kusikiliza hii kauli, walitumia umeme wa Tsh Laki 3.5 kwenda na kurudi Dar to Moro. Tuweke factors zote, tu-assume watumie wa Laki 4 kwenda tu, inamaana Mil 7.4 faida.

Toa gharama zote za service, sijui itazidi Tsh ngapi ila najua kwakua chuma mpya haina matumizi makubwa kwenye service, na toa posho ya wafanyakazi.

Inamaana chuma inaingiza zaidi ya Mil 5 kwa safari.

Tusubiri waseme wanaendesha kwa hasara.
Mkuu - Ni lazima ichangie mishahara ya wafanyakazi wa TRL (Operating cost), ichangie pia ununuzi wa mabehewa, vichwa (fixed cost) na pia ichangie kwenye gharama za hiyo reli ambazo ziko kwenye deni la taifa (fixed cost). Bila kusahau - Mama anataka Gawio la uwekezaji kila Mwaka.....
 
Bora kupanda Abood, masaa 2:30 nimefika Msamvu na nauli 10k
Mmmmmh masaa 2:30 kwa basi dar moro hapana.

Mimi mara nyingi nasafiri zaidi ya masaa 3, tena
Magari yalivyomengi siku hizi na sheria za latra zilivyokuwa kali ni mpka masaa 4 unatumia tena na Dakita zake.
Hio masaa 2:30 hilo basi limetembea speed sana.
Na kwa barabara ya moro ni risk sana.
 
Safari ilianza Saa 12:01 na kufika Morogoro Saa 1:55
??
Ilikuwa safari ya dakika 114..... ikiongozwa na nahodha, Ahazi Mfupa. iliondoka Dar es Salaam saa 12:01 asubuhi na kuwasili Morogoro saa 1:55 asubuhi.
?? 12.01-1.55
"Tumekuja na abiria kama 600 hadi 700,
Hakuna anayejua abiria wangapi walisafiri!
Tofauti na wakati wa safari ya majaribio Februari 27, 2024 iliyotumia saa 2.20, leo ikiwa ni safari ya kwanza ya abiria treni hiyo imetumia saa 1:55 kufika Morogoro.
Hapo juu 114
 
Mmmmmh masaa 2:30 kwa basi dar moro hapana.

Mimi mara nyingi nasafiri zaidi ya masaa 3, tena
Magari yalivyomengi siku hizi na sheria za latra zilivyokuwa kali ni mpka masaa 4 unatumia tena na Dakita zake.
Hio masaa 2:30 hilo basi limetembea speed sana.
Na kwa barabara ya moro ni risk sana.
Vyuma vya usiku
 
Pongezi kwa mama tu.
Katoa Hela yake Mfukoni ? Mbona mnakuwa wajinga sana. Pongezi kwa wananchi ambao wanahaingaika kukatwa kodi. Anapewa pongezi mtu ambae probably hata kodi halipi.

Kwanza ni mapema kutoa pongezi zozote.

Ndani ya huo mradi pesa zimepigwa sana . Gharama zilizotumika ni kubwa as compared na ununuzi wa treni, hizo gharama tungepata train za kichwa cha ndege. Hizo train ni old version na zinatumia voltage kubwa.

Nauli sio realistic . Nauli za train huku tulipo ni dola 2 , huko , ni mambo yale Yale ya mwendokasi. WTZ wangekuwa wako smart kuna mengi ya kuhoji, mngefanya pia study kujua gjarama za nauli zina realistic gani

Unamsifia kiongozi ambae anakula takriban 400M kwa mwezi plus na wizi juu
Mambo ya hovyo
 
Kwa nauli ya Tsh 13,000/= kwa kichwa, watu 600 inamaanisha wamepata Tsh Mil 7.8 kwa kwenda tu.
Kadogosa: Tumetumia umeme wa 336,000 kwenda na kurudi Dar - Morogoro

Kwa kusikiliza hii kauli, walitumia umeme wa Tsh Laki 3.5 kwenda na kurudi Dar to Moro. Tuweke factors zote, tu-assume watumie wa Laki 4 kwenda tu, inamaana Mil 7.4 faida.

Toa gharama zote za service, sijui itazidi Tsh ngapi ila najua kwakua chuma mpya haina matumizi makubwa kwenye service, na toa posho ya wafanyakazi.

Inamaana chuma inaingiza zaidi ya Mil 5 kwa safari.

According to TRC wamesema kwa siku itakua inapiga route nne.

View attachment 3017294

Kwahiyo ni Mil 20+ faida iyo. Tumetoa matumizi.

Tusubiri waseme wanaendesha kwa hasara.
Hii uzuri sio kama kilimo cha matikiti.
 
Safari ilianza Saa 12:01 na kufika Morogoro Saa 1:55

Hongera Rais Samia. Hongera Dr Mpango. RIP Shujaa Magufuli

========

Ilikuwa safari ya dakika 114 zenye bashasha, abiria zaidi ya 600 wakiwa kwenye mabehewa 14 ya treni ya umeme iliyoanza safari ya kwanza leo Juni 14, 2024 ikiongozwa na nahodha, Ahazi Mfupa. Treni iliondoka Dar es Salaam saa 12:01 asubuhi na kuwasili Morogoro saa 1:55 asubuhi.

Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema safari hiyo imehusisha mabehewa 14, matatu yakiwa ya daraja la juu.

"Tumekuja na abiria kama 600 hadi 700, mabehewa mengi yalikuwa yamejaa, ingawa hadi yote 14 yajae tungefika 1,000," amesema Kadogosa katika mahojiano na Mwananchi Digital.

Safari ilivyokuwa
Katika stesheni ya SGR Dar es Salaam, abiria walianza kuwasili saa 11.00 asubuhi. Kila aliyesafiri kabla ya kuingia ndani treni alikaguliwa kwa kutumia skana. Ilipofika saa 11.30 asubuhi, kulitolewa tangazo kuwataka abiria wanaosafiri waendelee kuingia ndani ya treni.

Matangazo yaliendelea hadi dakika tano kabla ya safari kuanza. Ilipofika saa 12.01 asubuhi treni ilianza safari kuelekea Morogoro. Ilipofika Kituo cha Pugu, ilisimama kwa dakika mbili na kupakia abiria wachache waliokuwa kituoni hapo. Mbali na kituo hicho, pia ilisimama kwa dakika mbili kwenye vituo vya Soga na Ngerengere kabla ya kuwasili stesheni ya Kihonda.

Tofauti na wakati wa safari ya majaribio Februari 27, 2024 iliyotumia saa 2.20, leo ikiwa ni safari ya kwanza ya abiria treni hiyo imetumia saa 1:55 kufika Morogoro.

Ukataji tiketi
Maswali ya wengi ilikuwa ni namna ya kukata tiketi. Kadogosa amesema abiria anaweza kukata kwa njia ya mtandao au dirishani kwenye ofisi za TRC. Japo kulikuwa na sintofahamu ya nauli, Kadogosa amesema Sh13,000 kwa daraja la kawaida ni nauli rafiki. "Hii ni treni ya Watanzania, zimewekwa nauli rafiki watu kuzimudu," amesema.

Baadhi ya abiria wakiwa ndani ya treni iliyoanza safari ya kwanza kutoka Jijini Dar es Salaam kwenda Morogoro.

Vyakula, vinywaji marufuku
Katika usafiri huo, hairuhusiwi kuingia na kinywaji chochote wala chakula. Mmoja wa wahudumu katika treni hiyo, Zuhura Milala amesema kila kitu kinapatikana ndani ya treni na kwenye stesheni. Japo katika safari ya leo, waliotumia vinywaji walikuwa wachache, ikielezwa huenda ni kutokana na wengi kutokuhitaji kutokana na muda waliosafiri na mabehewa mengi hakuna aliyeulizia.

Nahodha afunguka
Nahodha aliyeendesha treni hiyo, Ahazi Mfupa amesema hakuwa anafahamu kama yeye ndiye atakayekabidhiwa jukumu hilo hadi siku chache kabla ya safari. "Tuko manahodha waandamizi wengi, nilichaguliwa mimi na mwenzangu mmoja kuendesha treni hii, nashukuru Mungu safari yetu imekuwa nzuri na tumefika kwa muda tulioutarajia," amesema.

Mfupa amesema wametembea kwa mwendo wa juu wa kilomita 155 kwa saa ingawa treni hiyo uwezo wake wa juu ni kilomita 160 kwa saa.

Walichosema abiria
Wakizungumzia usafiri huo, baadhi ya abiria wamesema imekuwa na mwanzo mzuri. "Huduma tuliyoipata leo ikiwa endelevu ni usafiri mzuri, maana abiria unafika unapokewa vizuri na kila hatua ya safari mnaelezwa," amesema Noela Alphonce, mkazi wa Dar es Salaam.

Abiria mwingine, Albert John amesema aliposikia treni inaanza safari leo, aliamua kukata tiketi na kusafiri.
"Sikutaka nisimuliwe, nimeamua kutumia tu pesa yangu kuja na kurudi ili nijionee mwenyewe usafiri huu ulivyo," amesema.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile aliwahimiza Watanzania kutumia vema usafiri huo kwa usafi na ulinzi kwa kuwa ni kitu chao.

Bro bila kafoto, wengine tunachelewa sana kuelewa.
 
Back
Top Bottom