True Crime Thread: Updated Regularly

True Crime Thread: Updated Regularly

Castr

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
35,012
Reaction score
70,201
Ni usiku wa manane Ronnie Jr anasikia makelele baba na mama yake wanabishana. Anawafuata sebuleni anakuta damu zimesambaa sebule nzima, baba yake ameshikilia bunduki aina ya shotgun kumuelekea mama yake.

Baba, Ronnie Oneal, alipoona mwanae amefika pale akamuamrisha atembee kuzunguka sebule huku akiwa anasema 'Allah Akbar' vyanzo vinatofautiana, vingine vinasema muda huu Kenyatta alikimbilia kwenye chumba cha mwanae wa kike ambaye ni mlemavu na vyanzo vingine havisemi hili.

Ila vyote vinakubaliana kwamba muda huu ndiyo Mama, Kenyatta Barron, akapata nafasi ya kupiga namba ya dharura, 911.

60cfc1fea84cef001e5ef90c.jpeg


Kenyatta enzi za uhai wake.

Katika tape iliyosikilizishwa mahakama anasikika Kenyatta akiongea:

'Nimepigwa risasi' sauti ni ndogo kama vile ananong'ona.
'Nisaidie tafadhalia nimepigwa risasi nisaidie tafadhali'

Hakimu anasema katika kesi alizowahi kushiriki hii ni ya kikatili kuliko zote. USA kesi za risasi ni kila siku hivyo inafanya ujiulize ni nini cha ziada kwenye hii kesi ya Kenyatta Barron.

Kwenye recording anasikika Oneal akiongea kwa kelele 'Allah Akbar' kisha anasikika akisema 'Njoo hapa umuue huyu malaya haraka'

Kenyatta anasikika akimwambia Oneal:

'Ronnie basi, nisamehe' anaendelea kuongea 'Nisamehe, nisaidie umenipiga risasi mkononi'

Baada ya muda kidogo inasikika sauti ya mwanaume (Ya Oneal) ikisema:

'Hauelewi'

'Ameniua huyu'

Kisha unasikika ukunga. Hakimu anasema 'Huu ni ukunga wa mtu anayejua leo ni siku yangu ya mwisho kua hai'

Kisha Oneal akamuamrisha mwanae aje ashiriki katika kumuua mama yake. Ronnie Jr mbele ya baba ambaye ameshakua mkali na ana bunduki hakua na jinsi, akaungana na baba yake.

Baba akamwambia Ronnie Jr waishike bunduki kwa pamoja na washoot kwa pamoja. Kwenye tape kinasikika kishindo lakini inaaminiwa siyo cha risasi. Hakiwezi kua cha risasi kwa kua shotgun iliishiwa risasi.

Oneal akamuamuru mwanane akalete kisu ili waje kummalizia Kenyatta.

Ronnie Jr akaenda kufuata kisu.

Huu muda wa kusubiri kisu Kenyatta akautumia kutoroka, akatoka nje ya nyumba akafika mpaka kwenye ngazi za jirani yao na hapo ndipo alipokamatiwa na Oneal. Oneal akatumia shotgun kumpiga nayo kichwani Kenyatta, alitumia nguvu kubwa kumpiga kwa hiyo shotgun mpaka ikavunjika vipande viwili na ikapinda.

Kisha akauburuza mwili kuurudisha ndani.

Ronnie Jr akiwa anatoa utetezi wake mahakamani anasema kisha baba akarudi na shoka akamfuata mdogo wake akamlaza kifudi fudi na kumkata kwa shoka nyuma ya kichwa.

Kutokana na hitlafu ya ubongo aliyonayo Ron'veya hata hakuleta upinzani. Kaka mtu anasema akashuhudia macho ya mdogo wake yakipinduka kurudi juu. Huo ukawa mwisho wa Ron'veya.

60cfc1fea84cef001e5ef910.jpeg


Ron'veya enzi za uhai wake.

Kisha baba, Oneal, akajaribu kuwachoma Ronnie Jr na Ron'veya ila hakufanikiwa, moto haukua mkubwa kama alivyotaka. Akachukua kisu na kumchoma Ronnie Jr.

Wapelelezi na majirani wanasema walidhani Ronnie Jr hatopona. Damu mwili mzima kiasi kwamba waliamini amechanwa matumbo.

Baada ya kumchoma kisu Ronnie na kuona amelala chini Oneal akatoka nje. Siyo ili atoroke, hapana, alitoka nje ili aichome nyumba nzima huku maiti za mkewe na wanae zikiwa ndani.

So akamwagia gasoline nyumba nzima na kuiwasha moto kisha sasa akatokomea.

Ronnie Jr, kwa ujasiri akajitahidi kujivuta mpaka nje. Akakutana na jirani yao ila akapoteza fahamu na akazindukia hospitali.

Kesi ikafunguliwa na Oneal akachagua kujiwakilisha mwenyewe, hakutaka wakili, katika ufunguzi Oneal anasema 'Mnaona kama nipo peke yangu ila Mungu mkuu yupo pamoja nami'

60cfc1fea84cef001e5ef90d.jpeg


Oneal akiwa mahakamani.

Katika tukio zima aliyepona ni mwanae wa kiume na akiwa kama shahidi Oneal akawa anamhoji maswali Ronnie Jr. Katika wapelelezi wa kwanza kufika kwenye tukio mmoja amemuasilia Ronnie Jr, jina la aliyemuasili halijawekwa wazi kwaajili ya usalama wa mtoto.

Mahojiano yao yalifanywa kwa kupitia screen, Ronnie Jr anasema amekaa na mbwa ili kumtia nguvu ya kuhojiwa na baba yake.

His own father.

Baba anamuuliza 'Unayaonaje maisha siku hizi?' kisha anamuuliza 'Uliona nikimshoot mama yako?' Ronnie Jr anajibu 'Hapana' anamuuliza tena 'Uliniona nikimuua mdogo ako?' Ronnie Jr anajibu 'Hapana'

Kisha anamuuliza 'Nimewahi kukuumiza?' Ronnie Jr anajibu 'Ndiyo, ulinichoma kisu'

0_gDpIc9-f9H6xwxVP.jpeg


Ronnie Jr kulia.

Kwa kusema hapana Ronnie Jr alikua ameenda kinyume na maelezo aliyotoa polisi. Ila katika saiokolojia ni kawaida ya oppressed kubadili maneno ikatokea anaulizwa mbele ya oppresser kwakua oppressed subconsciously huamini oppresser ana mamlaka juu yake.

Mbaya zaidi tukio zima halina sababu iliyo wazi ya kupelekea Oneal kufanya alichokifanya. Baba yake Oneal anasema mwanae aliwahi kumuambia anasumbuliwa na paranoia, kama unataka mfano halisi wa paranoia ni kama Deo Kisandu anavyoamini serikali ya Tanzania inacontrol maisha yake.

Oneal anasema alimuua Kenyatta kwa kua Kenyatta alikua anataka kuwaua watoto na yeye alimuua ili kuwatetew watoto. Ni utetezi wa ajabu kidogo ukiangalia mazingira na maelezo ya tukio.

Hapa JF tuassume Kenyatta alimuua Ron'veya na Oneal akaingilia kati na kumshoot mkononi Kenyatta.

Kulikua na haja gani kumuamrisha Ronnie Jr azunguke huku akisema 'Allah Akbar'?

Kulikua na haja gani ya kumchoma kisu Ronnie Jr?

Kulikua na haja ya kujaribu kumchoma moto Ronnie Jr na Ron'veya?

Kulikua na haja ya kuichoma nyumba moto?

Haya maswali mahakama haikupoteza muda kujiuliza. Wakili wa serikali alikua amedhamiria hukumu ya kumuangukia Oneal iwe kifo. Oneal, supporter mzuri wa 'Death penalty', alikwepa kikombe hicho na amefungwa kifungo cha maisha.
 
Jina la kuzaliwa ni Karl Tanzler, akaja kujuliakana kama George Karl Tanzler, Carl Von Cosel, Carl Tanzler Von Cosel, jamaa alikuwa na majina mengi kulingana na wapi unaenda kuangalia.

Cheti cha ndoa kina jina tofauti, karatasi za kuomba uraia wa Marekani zina jina tofauti na cheti cha kifo kina jina tofauti pia.

Ila hapa tumjue kama Carl Tanzler, mjerumani ambaye alifanya kazi kama radiographer na baadaye akawa anajitambulisha kama daktari. Alitumia muda wake kusafiri huku na kule, kipindi cha vita ya kwanza ya dunia kilimkuta Carl akiwa Australia.

CARL-TANZLER_04.jpg

Carl Tanzler

Baada ya Australia kwenye miaka ya 1920 akarudi Ujerumani akaoa. Akamuoa Bi. Doris Schafer wakapata watotot wawili.

Jasiri haachi asili. Carl akaendeleza uzururaji akatoka hapo Ujerumani na safari hii akaenda mpaka Marekani, kisha akazurura mpaka Cuba. Akaenda kutulia eneo linaitwa Key West, Florida.

Na hapa ndiyo uchizi unapoanzia. Uchizi wa mapenzi to be clear.

Carl alivyokua mtoto anasema alipatwa na ndoto kutoka kwa mzimu wa bibi yake ambaye alimuambia 'Mpenzi wako wa milele atakua ni mwanamke mwenye nywele nyeusi na asiye na asili ya hapa' kisha akaonyeshwa na sura.

Bibi yake aliyempa haya maono ni Countess Anna Constantia Von Cosel kimada wa Augustus the Strong.

Akiwa hapa Florida akapata kazi kama radiographer wa hospitali ya U.S Marine.

Kisha Jumanne ya mwezi wa nne ya 1930 ikafika. Carl akiwa kazini hapo hospitali akamuona Helen de Hoyos (Elena De Hoyos), Helen aliletwa na mama yake ili kutibiwa TB, ugonjwa hatari sana kwa miaka hiyo, baada ya kumuona Carl akakumbuka maagizo ya mzimu wa bibi yake:

Nywele nyeusi.

Atakua mgeni.

Elena-de-hoyos.png

Helen (Elena) De Hoyos

Helen ana nywele nyeusi na ni mwenyeji wa Cuba. Hivyo amefit na sifa alizotajiwa.

To be fair Helen alikua ni mrembo wa eneo lile pengine kupita wote, baba yake alikua anamiliki kiwanda cha kutengeneza 'cigar'

elena_milagro_hoyos-437x640-1.jpg

Helen

Anyway, kipindi hichi ndicho Carl akasema yeye ni daktari pia hivyo aachiwe amtibu Helen.

Kilichofuatia ni Carl kutobanduka pembeni ya kitanda cha Helen. Kumpa zawadi za vito vya thamani, mikufu, pete, bangili na nguo za gharama.

Ndugu wa Helen waliona juhudi za Carl kwakua hata baada ya Helen kurudi nyumbani Carl aliendelea kwenda na kwenda na kwenda. Na huku akiwa na zawadi na vitu mbalimbali ili kumfurahisha Helen.

Pia Carl akamuambia ukweli Helen kua anampenda. Hakuna ushahidi wa kuonyesha Helen alikubali au alikataa lakini hata kama alikataa hatuwezi jua kwakua Carl alishafikia point of no return and a 'No' couldn't stop him.

But death did.

Mwaka 1931 Helen akafariki. Hatimaye something stronger came and stopped Carl.

Akagharamia mazishi.

Akagharamia ujenzi wa kaburi.

Elenas-mausoleum.jpg

Kaburi la Helen

Akajifunza nyimbo za kihispania akawa kila usiku anaenda katika kaburi la Helen na kumuimbia mpenzi wake.

Hata hivyo kifo nacho kilishindwa mzuia Carl kwa muda mrefu, jioni moja ya mwaka 1933 (Mwaka ambao alifukuzwa kazi pia) Carl akaenda kufukua kaburi akauiba mwili wa Helen. Akenda nao maabara kwake na kuanza mpango wa kumrudishia uhai mpenzi wake.

VAN-COSELS-LABORATORY.jpg

Maabara

Mwili ulishaharibika. Carl hakujali. Akaijaza mifupa ya Helen kwa nguo alizochovya kwenye nta ya mishumaa. Akatengeneza mask ya usoni kwa kutumia nta ambapo alijaribu kuirudisha sura ya Helen.

Kwa kua macho yalishatoboka akatengeneza macho ya kioo na kuyabandika kwenye mashimo ya Helen.

Kifuani na tumboni alimjaza matambara ili kumpa muonekano wa asili wa mwili wa binadamu.

Harufu ya kuoza akawa anaituliza kwa manukato makali na kumpulizia Helen na nyumba nzima.

Mwili wake ambao viungo vinameguka meguka akatumia nyaya kumuunganisha ili viungo visisambaratike.

Now Helen is perfect.

corspe-of-de-hoyos.jpg

A perfect Helen

Ila atamficha wapi? Hua hatufichi wapenzi wetu hivyo Helen alikua anaishi na Carl kama mume na mke.

Walikula pamoja, walicheza muziki pamoja na la muhimu zaidi walilala pamoja. Walilala pamoja kimaana yoyote unayoijua as in alishiriki tendo na maiti hali inayojulikana kama necrophilia na alilala naye kama mkewe hali ya wapenzi wawili wanaopendana.

Akiwa anajiona anaelekea kushindwa kumfufua mpenzi wa maisha yake kwa kutumia madawa akaamua kutengeneza ndege ambayo ataitumia kupaa akiwa na mwili wa Helen na atatumia mionzi ya jua ya nje ya atmosphere ili kumfufua Helen.

air-ship-built-by-van-cosel.jpg

Ndege

Kabla mpango wake haujafaulu tayari minong'ono ilisambaa mitaani kwamba Carl ana mpenzi mpya ila siyo binadamu wa kawaida. Ikafikia kusemwa kwamba 'Siyo binadamu wa kawaida kwakua ni mwili wa Helen'

Dada yake Helen, Florinda, akajitoa kwenda kwa Carl ili kuthibitisha, amefika mlangoni anagonga haitikiwi. Akafungua mlango na kuchungulia ndani anamkuta Carl akicheza muziki na mwili wa Helen.

So lost hata hasikii hodi.

Florinda akaita mapolisi. Carl akakamatwa. Mwili wa Helen ukawekwa kwenye public display, zaidi ya watu 6800 wakahudhuria kuuangalia mwili.

Mwili wa Helen ulikutwa umewekwa makaratasi ukeni ili kurahisisha uume kupita.

Carl akashtakiwa, mwili wa Helen ukarudishwa kwa familia yake. Wakauzika tena ila safari hii hawakuweka jiwe kuonyesha kaburi la Helen kuhofua Carl kurudia tukio.

Mahakamani Carl akaonekana hana akili za kushtakiwa hivyo akaachiwa, vyanzo vingine vinasema kuachiwa kwake kulitokana haswa na kumuonea huruma juu ya huba linalomtesa. Wakina mama walikua wakijaa mahakamani na kusema wanatamani nwanaume mwenye mapenzi kama huyu.

images (1).jpeg


Alivyoachiwa akahama na eneo akaenda Marekani, akaenda na hisia zake pia. Akajenga sanamu kubwa lenye umbo na sura ya Helen na kuendelea kuishi nalo.

Mwaka 1952 mwili wa Carl ulikutwa kwenye sakafu uchunguzi ulionyesha amefariki kwa zaidi ya wiki tatu. Hata hivyo vyanzo vinatofautiana vingine vinasema alikutwa amekufa akiwa amepakatwa na sanamu la Helen na vingine vinasema alikutwa tu sakafuni.

Pia kuna taarifa zinadai actually Carl ndiye alimuua Helen na alifanya hivyo ili kuhakikisha anabaki naye milele. Haijathibitika ila inabaki ni kitu alichokidai mwenyewe.

Cheti cha kifo kimemuandika kama Carl Tanzler
 
Niliwahi iandika sehemu naamini ina nafasi yake hapa.

Andrei Chikatilo - Rostov Ripper
images (1).jpeg


Mwalimu, muonekano wa upole, umri umeenda kidogo lakini katili aliyewalenga watoto wa kiume, wote kuanzia miaka 7 mpaka 21 na mabinti kwa uchache. Wahanga wake walikua ni vijana wa mitaani au maskini walioshinda kwenye stesheni za treni za Urusi.

Urusi ilikua na njaa. Kwa kuwahadaa kwa chakula na pesa Chikatilo alijihakikishia kua na wahanga kwa kadri alivyojisikia. Alitafuta mhanga mwanamke pale tu alipokosa wa kiume kwakua ndani mwake aliwaonea wivu watoto wa kiume akiona wanakuja kuishi na kupitia maisha ambayo yeye hakuyapitia kingono.

Chikatilo alikua hanithi.

Hata namna yake ya kuua wahanga wa kiume ilikua ni kuwakata kata sehemu za siri. Mwanzoni wahanga wake alikua akiwatoboa macho, alipoulizwa baadaye alisema anahofia mhanga wake kubaki na taswira yake machoni na kwenda nayo mbinguni, alipogundua hiyo imani siyo kweli akawa anawaachia macho yao.

Chikatilo alianza kuua mapema na ni siku hiyo ndiyo akajua wapi atapata msisimko wa kingono, sababu pekee ilimfanya ajizuie ni kazi yake ya ualimu ilikua ikimhamisha hamisha. Anasema kua alikua akipigana mieleka na mwenzake mmoja akiwa amemkaba kwa kumuweka chini alijishangaa akisimamisha mbo.o. Anadai alimuua bahati mbaya lakini yawezekana alitaka kujua mwisho wa kumkaba kama ingemsaidia tatizo lake.

Alikua mdogo hata hakuhisiwa kama angeweza kuua.

Kuanzia 1970s mpaka 1990s Chikatilo akazunguka Urusi akijiongezea idadi ya wahanga, akapachikwa jina the Rostov Ripper, kwake idadi ya visu ilitathmini kiwango chake cha kusisimuliwa kingono, hivyo haikua ajabu kukutwa maiti yenye majeraha ya visu kuanzia 40 mpaka 100.

Mhanga mmoja aliokotwa karibu na njia ya kwenda kwa jamaa ambaye ni sexual offender kwa kuhofia kuhusishwa na tukio, akajinyonga.

Maofisa wa KGB wakishirikiana na polisi wakaweka maafisa wao stesheni zote za Treni wakitumaini mhusika atajichanganya na kujilengesha kwa afisa mmoja. Mpango ulifeli, muda huo Chikatilo alikua kikazi sehemu nyingine hivyo Rostov ikatulia kwa muda ila huko alipoenda hali ikachafuka.

Akarudishwa tena Rostov akakamatwa katika mpango wa KGB kupunguza idadi ya washukiwa. Akakutwa ana kisu na kamba kwenye begi, ambacho hakua nacho ni rekodi ya uhalifu hivyo wakamuacha aende, wakasulubiwa waliobaki, wakakiri makosa ili suluba zisiendelee na wakahukumiwa kunyongwa.

Ila mauaji hayakukoma.

Wakajua kua waliingia chaka, wakarudi tena kazini. Safari hii wakafanya tena zoa zoa nyingine, na katika zoa zoa hii Chikatilo alikuemo pia, mkuu wa upelelezi machale yakamwambia huyu ndiye mtu wetu tatizo ni kwamba inabidi akubali haraka kwakua sheria imeweka ukomo wa siku unazoweza kukaa na mshukiwa ambaye hujayajua mashtaka yake.

Chikatilo alikana kila kitu na akatolea maelezo kila alichoelekezewa. Mkuu wa upelelezi akafuatwa na mwanasaikolojia ambaye aliomba amprofile na aongee na Chikatilo. Akamkatalia. Tunadeal na muuaji saikolojia yako itafaa nini?

Kisha ikabaki siku moja ili ukomo wa sheria utimie na Chikatilo aachiwe mkuu wa upelelezi akamuita yule mwanasaikolojia akamkabidhi zigo la misumari.

Mwanasaikolojia akaanza kumuelezea jinsi alivyo akasema kua "Wewe ni hanithi" kufikia hapo Chikatilo akang'aka akaanza kutoa maneno makali, askari wakajua wameipata breki waliyoitafuta kwa miaka 12. Alipoambiwa kua ulikua unawatoa macho kwakua uliogopa sura yako kubaki machoni mwao akabaki mdomo wazi.

Hunijui sikujui unawezaje kuniambia nilivyo kisirini? Chikatilo akakiri.

Akaelezea matukio, akaelezea kwanini mauaji kuna muda yalikoma Rostov. Akaelezea jinsi alivyoziingilia na kupigia punyeto maiti. Orodha ilikua ndefu, karibia watu 100 ila ripoti iliyothibitishwa ilishusha idadi.

Mahakamani Chikatilo ilibidi afungwe kweye 'Cage' ripoti nyingine zinagomea hili swala kua halikutokea ila picha zipo. Muda wote wa kesi Chikatilo alikua kama chizi, anaweza kua sawa dakika hii, dakika inayofuata atatukana kuanzia hakimu, shahidi, wakili mpaka waandishi wa habari.

images (2).jpeg

Chikatilo kwenye 'cage'

Baada ya muda hukumu ikatoka Chikatilo akahukumiwa kifo.
 
Ugonjwa wa chikatilo ulimsumbua pia mwendazake.....ila useme matukio ni tofauti..mwendazake aliwachukia vijana wadogo matajiri na wasomi na aliamini huwezi kuupata ukwasi mpaka upitie msoto majera...nyinyi ni mashahidi mnaona ni jinsi gani matajiri na wasomi walivyopata jiwe ya jiwe
 
Mwendazake anakuwasha. Haya keshaondoka msoto upo kwa gaidi je huo ni ugonjwa gani?
Ugonjwa wa chikatilo ulimsumbua pia mwendazake.....ila useme matukio ni tofauti..mwendazake aliwachukia vijana wadogo matajiri na wasomi na aliamini huwezi kuupata ukwasi mpaka upitie msoto majera...nyinyi ni mashahidi mnaona ni jinsi gani matajiri na wasomi walivyopata jiwe ya jiwe
 
Back
Top Bottom