True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

Uongo yaani hata maji anakuchotea kwa uchawi na wengine wapo? Na yeye ulimkuta kwenye foleni? Wy hakujichotea?
 
Uongo yaani hata maji anakuchotea kwa uchawi na wengine wapo? Na yeye ulimkuta kwenye foleni? Wy hakujichotea?
Kuna watu wachawi dunia hii balaa, aafu kuhusu kufanya viini macho mchana kweupe tena mbele za watu, mwanzo hata mimi ilikua inanishangaza, lakini baadae nilikuja gundua karibia madem wote pale kijijini ni hatari kwa ulozi.
WEndouseme uwongo sasa.
 
Kuna watu wachawi dunia hii balaa, aafu kuhusu kufanya viini macho mchana kweupe tena mbele za watu, mwanzo hata mimi ilikua inanishangaza, lakini baadae nilikuja gundua karibia madem wote pale kijijini ni hatari kwa ulozi.
WEndouseme uwongo sasa.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 We jamaa kwa fix daaah ...
 
Nilichojifunza story hii na ya umughaka kanda ya ziwa kuna uchawi sana tena wa waz waz kabisa
 
Stori nzuri sana, ulifaidi sana maisha ya kijijini Hongera [emoji2] [emoji2]

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
...99
Jana ulinifurahisha ulivyokuwa unapaa huku umenikumbatia, alisema yunge mdogo tukiwa tumefika mahali pa kugawanyika kila mmoja ashike njia ya kwenda makwao.
Nilishtuka kusikia anasema jana nilikuwa napaa na sio ndoto kumbe! Nilitua madumu yangu ya maji pale na kumtaka asimame ili anieleze vizuri.
Hapana, peleka maji kisha tukutane hapa nikusimulie nilivyokuwa najisikia vizuri wakati tukiwa angani, alizidi kunitia hamu ya kutaka kujua kama kweli ile haikuwa ndoto bali uhalisia?
Haraka niliyabebelea madumu nikazipiga hatua zenye ujazo kuelekea nyumbani ili nimimine maji na kurudi nimgonje pale yunge mdogo anape kisa chote ambacho mimi niliamini ni ndoto tena mbaya mno, nilikumbuka jinsi alivyopasuliwa na jiwe lenye ncha kali na mwonekano mbaya na wakuchukiza kisha nikashtuka nikiwa kitandani na asubuhi hii kumwona akiwa hai, tena mwenye urembo uleule pasi na mchubuko wowote, iweje aniambie nilikuwa napaa live?
Nilifika pale nyumbani na kuingia haraka jikoni, nilimimina maji mtungini nikatoka nje haraka.
 
...100
Nilitoka jikoni haraka ili kumuwahi yunge mdogo asinipite pale njiapanda, lakini kabla sijafika mbali bibi aliniita na kunitaka nimfatie chumvi senta mara moja kisha ntafata maji baadae, nilishtuka kidogo huku moyoni nikimlaumu bibi kwanini asingoje nafate maji kwanza?
Niliyaweka madumu pale na kumrudia bibi ili anipatie pesa haraka nifate chumvi kisha nimuwahi yule msichana anipe stori nzima, alitumia kama dakika mbili nzima ndipo akatoka ndani na shiringi 1000 akinitaka nikanunue kilo 1 ya chumvi.
Nilitoka nduki kama kiberenge, muda kidogo nikawa nimefika pale senta, nilitafta kibanda ili ninue chumvi haraka kisha nirudi lakini vibanda vyote vilifungwa, muda kidogo nilimwona juma (captain) akiwa na jamaa wengine wawili, nilimsalimia kisha nikamwuliza mbona vibanda vyote wamefunga?
Kuna msiba ulitokea jana, hivyo watu hawawezi kufungua ilihali kuna msiba, alinijulisha juma na kunitaka nimngoje kidogo aniitie mhusika wa moja ya kibanda kilichokua pale, nilingoja na muda kidogo alirejea akiwa mwanamke.
 
...101
Alizunguka nyuma ya kibanda yule mwanamke na kufungua kisha akanipatia chumvi, nilimlipa na akanirudishia chenchi kisha nikatoka pale kibandani.
Kwahio dogo kesho utakuja zoezi, maana mechi inakaribia hivyo, alisema juma.
Kesho nitahudhuria wala usijali, nilimwambia.
Aaf habari ya mzee maduhu ya kupata ajali uliipata? Aliniuliza juma.
Mzee maduhu Yupi? Niliuliza.
Yule mzee kiongozi wa timu yetu, alielewesha juma.
Nilimkumbuka mzee yule, nilimkumbuka namna alivyoshindwa kunikamata dakika za mwisho kabisa kabla sijautupa upembe mbele yangu na kuuruka kisha nikasikia sauti za maumivu wakilia pamoja na yule mwanamke mnene.
Ahaa! Kumbe yule mzee mchangamfu sana alipata ajali? Nilivunga kama sijui jambo lolote.
Ndio alipata ajali ya moto pale kwake usiku wa kuamkia jana, kwani alikuwa amejificha kwenye kijumba kidogo cha nyasi akimngoja paka anaekamata kuku kila mara pale kwake, ndipo alipopitiwa usingizi na alikuja kushtuka nyumba inateketea moto, aliungua sehemu kubwa ya mwili na tumetoka kumsalimia hvyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…