...13
Basi tuliingia ndani ya slopu ile, nikaingia chumbani huku babu akiningoja pale sebleni, nilichukua elfu 60 ndani ya begi na kurudi nayo sebleni ambapo nilimkuta babu amengoja kwa hamu, nilimkabidhi akafurahi sana,
Kubyala kwa wiza (kuzaa kuzuri sana) alisema babu huku azificha fedha zili ndani ya puzo (bukta kubwa) alokuwa amevaa kwa ndani,
Usimwambie bibi yako kama umenipa mzigo, sawa mzee mwenzangu?
Alitahadhalisha babu, nikamwambia wala asijali, kwani bibi yeye nmempa masukari na maunga ya ngano kutoka kwa mama mkwe wake (mama yangu) hivyo simwambii chochote bibi,
Sawa pumzika kijana wangu, kesho ntakusimulia ntakayoyasikia huko kwenye tukio, alisema babu, kisha akaondoka,
Nilitoka nje kumuaga bibi kwamba nataka nipumzike, kwani nilitaka pia kuhakikisha kama babu ameondoka ili bibi naye nimpe mzgo wake,
Kweli babu alikua ameelekea senta kwenye tukio la fisi kuiba mtoto mapema tu,
Nilirudi ndani ya slop na kuchukua 50 elfu nikamkabidhi bibi na kumwambia, 30 imetoka kwa baba na 20 kwa mama.