Pettymagambo
JF-Expert Member
- Aug 21, 2017
- 1,490
- 8,227
- Thread starter
- #721
...108
Nilishangaa yule mzee kunisema mi mchawi, nilijikaza na kumpuuza huku nikiingia ndani na kutoka na viti viwili vya mbao, niliviweka pale kivulini kisha nikafata vingine viwili, nilimkabidhi babu kiti kimoja na kingine nilikalia mwenyewe.
Ehe kijana wangu kwanza samahani kwa yote yametokea, alivunja ukimya mzee yule ambae mda si mrefu aliniita mchawi.
Sisi hapa ni wataalamu wa mambo ya jadi (waganga wa kienyeji) mimi na mwenzangu huyu, na huyo mzee mwingine ni mfiwa ambae amefiwa na mwanae wa kiume, lakini pia mke wake ni mgonjwa kitandani asiye jiweza, alisema mzee yule na kuendelea,
Kilichotufikisha hapa kwenu ni kutaka kujua ukweli, maana inaonekana kifo cha yule kijana kinatatanisha sana, na tumejaribu kufanya utaalam wetu ikaonekana kuna mchezo mchafu unachezwa ndani ya kijiji hiki.
Hatukufichi kwani unaonekana ni kijana uliepevuka sasa, hivyo hatutarajii tutakayo yaongea hapa utafungua mdomo na kumweleza mtu awae yote.
Tumepiga ramli ikaonekana mke wa huyu mzee ndo muhusika wa vifo viwili.