115
Unasemaje yunge?
Nilimwuliza.
Umeshaniona utupu wangu, hivyo sana budi
kukupa ili ukamilishe tulipokomea jana na baada ya hapo nikuache wewe na mpenzi wako mwendelee, alisihi yunge mdogo.
Hapana, hilo hakuna, naomba unielewe, nikweli wewe ni msichana mzuri zaidi ya yunge, sasa nashangaa mbona unataka kujishusha hivyo, yaani upotayari uugawe usichana wako kwa mtu ambae hana malengo na wewe? Hapana, hilo nakataa hakuna, nilipigilia msumari.
Sawa bwana, ila ipo siku utanikumbuka, siku ambayo huyo unaemsema anakupenda mno atakapokuwa anakutenganisha kiungo kimoja baada ya kingine na kuvitafuna vibichi ndo utapata jibu, alisema.
Niliogopa kidogo japo nilijikaza ili asinistukie, niliwaza hivi kweli yunge wangu anaweza akaruhusu niliwe nyama? Hapana huyu ni mfa maji tu, nilijipa moyo na kumwuliza"
Unamaana gani kusema atanitenganisha vipande na kunila nyama, inamaana yunge ni mchawi ama vipi?
Sio mchawi tu, ni kiongozi wa wachawi wote hapa kijijini, aliongea kwa kujiamini.
Wachawi wote nawewe ukiwemo?