True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

Heading ya hii story haikunivutia kabisa,hvyo nilkuwa naipitiliza tu lakin kuna member niliona anaisifia kwenye ile story ya ujambaz wa chuga,tabora kigoma zambia ndo nikaamua niisake,nimeipenda sana

Weka weka na uongo ili iwe tamu zaidi
 
Heading ya hii story haikunivutia kabisa,hvyo nilkuwa naipitiliza tu lakin kuna member niliona anaisifia kwenye ile story ya ujambaz wa chuga,tabora kigoma zambia ndo nikaamua niisake,nimeipenda sana

Weka weka na uongo ili iwe tamu zaidi
nitag mkuukwenye hiyo story
 
114
Alilalamika sana msichana yule kwa kitendo cha kumwambia live kwamba nilikuwa nmezama kihisia kwa msichana mwingine.

Kama kosa langu ni kutovumilia maumivu jana naomba unisamehe na nipo tayari kukupa usichana wangu ikiwa hicho ndo kimesababisha utake kuniacha, alijitetea yunge mdogo.

Hapana yunge, kwanza nakupongeza kwaulicho kifanya jana, kitendo cha kujitoa mikononi mwangu na kusababisha
Tusishiriki tendo lile kilikua cha kishujaa sana, tamaa za kimwili zilitaka kuniponza na ningesababisha ugomvi kati yenu, hivyo basi naomba tuheshimiane tu kama majirani, nilimwambia pasipo masihara.

Nilishtuka kuona machozi yanamtoka binti huyu.

Basi sawa, alijibu kwa unyonge kisha akageuka na kuanza kuondoka huku akijifuta machozi kwa khanga kuukuu aliyokuwa amejifunga.

Niliingiwa na huruma kumwona msichana huyu akinililia, nilijikaza kiume kwani nilitaka kumwaminisha yunge mkubwa kwamba aliyonitendea nilipaswa kuyalipa kwa upendo wa kipekee kabisa.

Basi nakuomba unitoe tu usichana wangu kisha uniache.

Duh!
 
115
Unasemaje yunge?
Nilimwuliza.
Umeshaniona utupu wangu, hivyo sana budi
kukupa ili ukamilishe tulipokomea jana na baada ya hapo nikuache wewe na mpenzi wako mwendelee, alisihi yunge mdogo.

Hapana, hilo hakuna, naomba unielewe, nikweli wewe ni msichana mzuri zaidi ya yunge, sasa nashangaa mbona unataka kujishusha hivyo, yaani upotayari uugawe usichana wako kwa mtu ambae hana malengo na wewe? Hapana, hilo nakataa hakuna, nilipigilia msumari.

Sawa bwana, ila ipo siku utanikumbuka, siku ambayo huyo unaemsema anakupenda mno atakapokuwa anakutenganisha kiungo kimoja baada ya kingine na kuvitafuna vibichi ndo utapata jibu, alisema.

Niliogopa kidogo japo nilijikaza ili asinistukie, niliwaza hivi kweli yunge wangu anaweza akaruhusu niliwe nyama? Hapana huyu ni mfa maji tu, nilijipa moyo na kumwuliza"

Unamaana gani kusema atanitenganisha vipande na kunila nyama, inamaana yunge ni mchawi ama vipi?

Sio mchawi tu, ni kiongozi wa wachawi wote hapa kijijini, aliongea kwa kujiamini.

Wachawi wote nawewe ukiwemo?
 
116
Mimi sio mchawi, alijibu.
Basi umejuaje kama ni kiongozi wa wachawi? Nilimwuliza huku nikitambua fika kabisa aliyokuwa ananiambia ilikuwa ukweli mtupu, nami sikutaka kuoneka nayajua hayo hivyo nilivunga ili nipate kuyajua mengi.

Ebu niache nisije kukueleza nawe ukaja mwambia kisa umenogewa penzi mwenzio nikaenda kulimishwa usiku, alisema yunge mdogo.

Aliondoka huku nikimwona kabisa akiwa na uhitaji wa kuendelea kubaki pale tupige stori, nami kutokana na njaa kuniuma nilimwacha aende ili nitinge jikoni kujipakulia ubwabwa ule mtamu na kuanza kuushambulia, kweli nilifanya vile mpaka nikatosheka, nilinawa kisha nikaenda getoni mwangu na kujipumzisha kitandani.

Jioni babu na bibi walirudi na kunikuta nimeshakoka moto tayari.

Bibi aliingia jikoni na babu alikaa pale kuota moto, alinisimulia yote yaliyojiri kule juu ya wale waganga kung'ang'ana kwamba mimi nilihusika na kuwapa pigo wale wachawi wawili.

Na inasemekana sio hao tu, pia kunawengine watano nao walikutana na pigo lako takatifu,
Ehe nielezee a-z
 
Heading ya hii story haikunivutia kabisa,hvyo nilkuwa naipitiliza tu lakin kuna member niliona anaisifia kwenye ile story ya ujambaz wa chuga,tabora kigoma zambia ndo nikaamua niisake,nimeipenda sana

Weka weka na uongo ili iwe tamu zaidi
Uzi wake unaitwaje?? Toa link kama inawezekana
 
Back
Top Bottom