True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

Success never come to people who listens to too many whistles.

My friend JF is a jungle with too many animals, braves to fools

Dont base to fools dear fella, those are dogs in the Cage, that make you lose direction, infact they can not bite
Unamjaza sifa tu na wew ili aandike story yake Mara ,Mara saa tatu maraa saa nne kwa kifupi huyu Hana Content ya kuandika
 
162
Nilishangaa kuona mikia miwili ya mijusi ikiwa inagaagaa kwenye mko wangu sehemu ambapo yunge mkubwa, nilitikisa mkono kwa hofu ili ile mikia idondoke, lakini nilipotazama tena nakaiona ile mikia ikiwa imetulizana na kunata mkononi mwangu ikijishikiza isidondoke, ndipo babu alipeleka taratibu mkono wake kwa lengo la kutaka kuibandua ile mikia mkononi mwangu.

Babu alionekana kuchanganyikiwa kwani muda ulivyokuwa unasogea mbele basi ile mikia ya mijusi ilikuwa inazama taratibu ndani ya mwili wangu kupitia mkononi na taratibu nilianza kuyahisi maumivu.

Babu alishindwa kujizuia, sifahamu ale mikia ilimpa ishara gani mbaya maana alivyoonekana ni kama mtu atoavyo jicho kwa hofu pale anapomwona ampendae anataka kukata roho, ndivyo babu alivyoonekana.

Mama fai ebu njoo mara moja, aliita babu akimtaka bibi aje aone jambo lile, huku maumivu yakiongezeka kwa kasi nilianza kuugulia.

Bibi alifika pale na kunitazama mkononi ambapo wale mikia bado kidogo tu waishie mwilini mwangu, bibi alitimua mbio kuingia ndani.
 
Utake usitake utashusha tu [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
163
Bibi alirudi nduki kutoka ndani na alikuja tulipokuwa tumesimama na babu, aliushika mkono wangu na kunivuta tukausogelea moto, bibi alikisogeza kiganja cha mkono wake karibu kabisa na moto kwa muda kama wa sekunde 10 kitendo kilichonishangaza na kujiuliza inamaana haungui?

Alinishika mkono wangu kwa mkono wake wa kulia huku nikiwa nimeanza kulia kutokana na maumivu ya ile mikia, haraka bibi aliutoa mkono kwenye moto kwa haraka na kunichapa kofi pale ilipokua inazama ile mikia, nilipiga kelele za maumivu lakini babu alikuwa amenikamata vizuri na tayari bibi alisharudisha mkono wake karibu na moto kama mwanzo, nilianza kuhisi ile mikia imezama yote mwilini mwangu na ilianza kujiviringisha kitendo kilichonipa maumivu makali mno, nilipigwa tena kofi kali na la moto kwelikweli na bibi kama mwanzo, maumivu makali niliyasikia na nilitoa sauti ya maumivu, sauti ile nadhani ilifika kwa majirani.

Mh! Tumechelewa, aliongea bibi kwa kukata tamaa huku akianza kumtupia lawama yunge mkubwa kwa kitendo alichonifanyia.
 
INTERESTING...
 
164
Tunafanyaje sasa? Aliuliza babu huku akionekana kuzidiwa ujanja na yunge mkubwa kwani aliona mjukuu wake ninavyotabika kwa maumivu makali, nililia huku sauti ya kilio ikiongezeka na kupelekea majirani waanze kumiminika pale nyumbani mida hii ya saa 2 usiku, waliuliza tatizo nini, lakini hakuna aliyekuwa tayari kuweka bayana chanzo cha ugonjwa wangu, zaidi babu aliwaambia nilianza kuumwa ghafla tu.

Huyu msichana anataka kunivua nguo, nilishaapa kuachana na mambo haya lakini huyu mtoto anataka kunirudisha kwenye ulimwengu wangu pendwa, aliongea babu kwa sauti ya chini akimwambia bibi mara baada ya majirani kuondoka.

Ile mikia ilipotelea mwilini yote na kwenye mkono wangu vilibaki vialama viwili vyekundu vilivyojichora kama ile mikia iliyozama, maumivu yaliendelea mpaka babu alivyoinuka na kuingia ndani mwake akisema "nadime ntumba gwalushilo" {sasa nakamata kombora la kiama}

Alitoka ndani na kunitaka nimfuate, nilimfata mpaka nyuma ya nyumba niliyokuwa nalala mimi, kisha anitaka nifumbe macho nisifumbue.
 
Duuh, tunasubiri mkuu... Songa mbele usijibizane na mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…