True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Punguza Kamba basi Mwamba
 
170
Ndio babu nilifumbua macho uliponipiga na kitu mkononi, kwani nilimsikia yunge analia kwa maumivu akisema eti bhuhabhi mmeamua kumwua mtoto wenu? Ndo nikafumbua nimwone huyo mtoto, nilijitetea.

Kweli ulisikia sauti ya yunge? Aliuliza babu ambae nilimhakikishia ilikuwa sauti ya yunge mkubwa.

Basi tupumzike ila leo nauna mwisho wangu, aliongea babu kwa masikitiko na kukata tamaa.
Hapana babu, hakuna wa kukugusa upo na mimi, nilimtia moyo babu huku nikiwa sijui nini kilinipa jeuri ya kusema vile.

Nini kinakufanya ujiamini hivyo mjukuu wangu? Aliniuliza babu huku akijitaidi kutabasamu ilihali akiwa na maumivu.

Swali lile lilinifikrisha kidogo, nikawa najiuliza mimi mwenyewe, eti kweli, ni nini kinachonipa jeuri ya kutunisha kifua na kumwaminisha babu kwamba alikuwa katika mikono salama kwa uwepo wangu mimi ikizingatiwa nilikuwa nalia kama mtoto mdogo muda mfupi uliopita.

Huku babu akinitazama na kungoja nitampa jibu gani,
Ghafla nilikumbuka kitu, niliangaza chumbani nisione nichokitafta, vimeenda wapi?
 
Doh, Bibi yako keshafanya yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…