True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

Twidegeleke lolo bhadugu bhane

Pettymagambo anakuja
 
...68
Tusikilizane ndugu zangu, ambae alikuwa anasubiriwa amesha wasili tayari hivyo shughuli zote kama kawaida yetu iendelee, naomba masufuria yote yajazwe nyama haraka na utaratibu wake ufanyike kama kawaid, aliagiza binti huyu ambae nilitambua kabisa ni mkuu wao pale.
Watu waligawana masufuria na wengine kuwasha mioto pembeni kwa ajili ya kupika nyama ambazo sikuwa nimeziona mpaka muda huu. Muda kidogo walitokea wanaume kama 20 hivi wakiwa wamegawanyika wawili wawili ambapo begani walibeba mzegamzega nyama iliyoonekana kama ya ng'ombe, nilistaajabu ndani ya dakika 5 masufuria yale yalikuwa yanatokota nyama huku mioto ikiwaka vikali.
Tusikilizane tenaa! Alisikika yunge ambae sasa nilianza kumwogopa, leo ng'wana jong'hela ametuletea deni letu jamani, tunamshukuru kwa kutimiza ahadi hii, hivyo nimkaribishe hapa mbele atukabidhi mali yetu, aliamuru yunge.
Basi alitokeza yule mwanamke mnene aliyekuwa amefika muda si mrefu akiwa na yule mtoto kamning'iniza kwa mkono mmoja huku akitembea kwa majigambo,
 
Back
Top Bottom