...78
Alikua amefariki muda mfupi uliopita, alimaliza kunipa maelezo yale yunge mdogo.
Umezitoa wapi stori hizi? Nilimwuliza.
Nimesikia kisimani asubuhi, tena watu wanasema mama yake ni mchawi wa kupindukia na huenda kweli amemtoa mtoto wake na mjukuu wake kwa wachawi wenzie, alijibu yunge.
Hapo sasa niliunganisha matukio, jinsi yunge alivyokua ananiambia jana kwamba yule ameshakuwa kitoweo na kama wangenikamata na mimi pia nyama zingeongezeka na leo kungekuwa na msiba wangu pia.
Kwahio amesema analiwa nyama lakini atarudi, kivipi sasa, Niliuliza tena.
Huenda akawa amejipanga yule kijana na msiba wake ukawa kiini macho tu, alijibu yunge mdogo.
Msiba kuwa kiini macho kivipi wakati amesema analiwa nyama? Niliuliza tena.
Wenae unakichwa kigumu kuelewa, nakwambia inasemekana yule hajafa kachukiliwa na wachawi tu ila anajiamini atarudi kwa ajili ya mama yake.
Sasa kama hajafa na kila mwanakijiji anajua hivyo sasa wamekwenda msibani kufanya nini? Niliuliza tena swali lililoonekana kumkera binti huyu.
Kichwa ngumu.