True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

Arudi kutoka wapi? Nipo hapahapa na si muda mrefu naanza kuziweka.

Toka Jana unasema sasa hivi unaanza bishana na watu[emoji1][emoji1]
We andika tu then watu wachangie watakacho sasa hapo hapo we muandishi, msoma comments na kubishana. Kila mwandishi angefanya hivyo kungekua na Media?
 
...76
Nilimwuliza ikiwa nae anakula nyama za watu,
Alitazama kisha akasema, utajua yote nikirudi kutoka safari yangu.
Nilikaa kimya nikiyatafakari yote yaliyotokea, kisha nikamwuliza, kwahiyo sasa hurudi tena mkutanoni?
Naomba tuyaache hayo, nataka nirudi nyumbani nikajiandae na safari ya kesho, alijibu.
Kwayaliyotokea muda mfupi uliopita, nilitamani abaki pale mpaka asubuhi, kwani nilikuwa naogopa sana.
Nikamwombia mbona bado usiku sana, ulale utaondoka asbuhi.
Alikataa huku akiniomba radhi nisichukie, aliondoka na kuniachia maswali mengi kichwani huku nikianza kuingiwa na wasiwasi juu ya ukaribu wangu mimi na yeye.
Nilijilaza bila usingizi kunipitia, nilijigeuza pale kitandani mpaka saa 11 alfajiri ndipo nipopitiwa na usingizi, nilikuja kushtuliwa na babu aliyekuwa anagonga dirishani,
Dogo unalala mpaka saa tano unaumwa au umetutoka? Alitania babu,
Hapana babu nijihisi mwili kukosa nguvu, nilimjibu huku nikitoka ndani.
Tulisalimiana huku babu akinitizama kwa jicho la mashaka kidogo.
Mbona umeharibu dawa?
 
...77
Mbona umeharibu dawa yangu? Alinitupia swali babu, nilibaki kushangaa tu, nilikumbuka yunge alivyonibana mpaka nikakubali kwamba nimechanjwa chale na kupakwa dawa.
Nilisahau kukuambia sharti moja, nikwamba hukutakiwa kukubali hata kama amejua, hatakama amekuona, ili dawa isiharibika hukutakiwa kukubali, lakini imeshatokea na hiyo dawa imekufa hivyo tuangalia namna nyingine, alisema babu na kunitaka nibaki pale muda wote kwani wao wanakwenda msibani.
Kuna msiba wapi tena babu? Nimwuliza.
Ee kuna msiba tena umetokea, baba wa yule mtoto alieliwa na fisi amefariki ghafla asubuhi ya leo wakati jana alikuwa yu mzima wa afya, alijibu babu akimaanisha yule jamaa tuliekuwanae juu ya mti usiku na kumsikia akilia mama yake kumchinja mjuku wake.
Inamaana amekufa? Nilijiuliza.
Sawa babu mie nipo hapa.
Nilimwona bibi anatoka ndani, ila tulipokutanisha macho nilimwona kashtuka kidogo, nilimuwahi kwa kumsalimia na vijiutani kidogo, sikutaka ahisi kitu kama yunge alivyopa maelezo.
Kuna viazi na uji utakula mme wangu..!
 
Toka Jana unasema sasa hivi unaanza bishana na watu[emoji1][emoji1]
We andika tu then watu wachangie watakacho sasa hapo hapo we muandishi, msoma comments na kubishana. Kila mwandishi angefanya hivyo kungekua na Media?
Kama nisingekuwa nasoma comments hata hii yakwako nisingeiona.
 
...78
Baada ya babu na bibi kuondoka nilichukua karai nikalijaza maji kisha nikaenda bafuni kwaajili ya kuoga, baada ya hapo niliingia jikoni na kukuta sufuria kubwa lililojaa viazi vilivyoiva, kulikua pia na kisufuria kidogo pembeni kichokuwa na uji mwingi wa unga wa dona, nilipakua viazi kisha nikachukua bakuli dogo na kulijaza uji, nilibeba na kuelekea nje ambapo nilianza kuvishambulia viazi na uji ule ambao ulikuwa na sukari nyingi mno, ulikuwa na maziwa pia, baada ya kula niliviondoa vyombo vile na kuviosha kisha kuvirudisha jikoni, nilirudi getoni na kujilaza ambapo nilianza kuwaza mambo mengi niliyoyaona jana.
Ulipita muda mrefu mpaka nilipostuliwa kutoka usingizini na sauti ya mtu, jamani unalala mchana hivi? Ebu njoo basi ninashida, alikuwa ni yunge mdogo akiwa pale nje.
Niltoka na kumsalimia, alionekana kuchangamka kuliko siku zote, nambie nini nikusaidie, nilimwambia,
Nimekuijia ukanisaidie kumenya karanga, nimebaki mwenyewe nyumbani, mama kaenda msibani, alisema yunge mdogo.
Leta tumenyee hapa..!
 
...77
Inamaana wewe hutembeleagi majirani jamani? Aliniuliza yunge mdogo ambapo nilikaza mpaka alikubali afate karanga aje tumenye pale kwa babu, na muda kidogo alirejea akiwa amebeba dumu lenye karanga, nilisogeza viti viwili chini ya mwembe ambapo kulikuwa na kivuli ila yunge mdogo alinitaka nimletee mkeka ili akalie, nilileta mkeka na akaukalia na mara moja tukaanza kumenya huku stori zikiendele.
Wakati tukiendelea nilimwuliza yunge mdogo, hivi mtu aliefariki alikuwa anasumbuliwa na nini?
Inasemekana usiku wa saa 8 alipiga kelele kichwa kinamuuma sana, baba yake alitaka wamkimbize kwa mganga usiku huo lakini mama yake alitaka wangoje kukuche kwanza ndo wampeleke, walisubili mpaka saa 11 alfajiri ndipo wakambeba kumpeleka kwa mganga, wakati wakiwa njiani aliomba maji ya kunywa, walifanya jitihada maji yakapatkana, alikunywa kisha akasema, mimi na mwanangu tumekuwa kitoweo cha mama, naondoka ndugu zangu ila mwambieni mama nitarudi, baada ya kusema vile alikaa kmya mpaka walipofka kwa mganga ndipo wakastuka.
 
...78
Alikua amefariki muda mfupi uliopita, alimaliza kunipa maelezo yale yunge mdogo.
Umezitoa wapi stori hizi? Nilimwuliza.
Nimesikia kisimani asubuhi, tena watu wanasema mama yake ni mchawi wa kupindukia na huenda kweli amemtoa mtoto wake na mjukuu wake kwa wachawi wenzie, alijibu yunge.
Hapo sasa niliunganisha matukio, jinsi yunge alivyokua ananiambia jana kwamba yule ameshakuwa kitoweo na kama wangenikamata na mimi pia nyama zingeongezeka na leo kungekuwa na msiba wangu pia.
Kwahio amesema analiwa nyama lakini atarudi, kivipi sasa, Niliuliza tena.
Huenda akawa amejipanga yule kijana na msiba wake ukawa kiini macho tu, alijibu yunge mdogo.
Msiba kuwa kiini macho kivipi wakati amesema analiwa nyama? Niliuliza tena.
Wenae unakichwa kigumu kuelewa, nakwambia inasemekana yule hajafa kachukiliwa na wachawi tu ila anajiamini atarudi kwa ajili ya mama yake.
Sasa kama hajafa na kila mwanakijiji anajua hivyo sasa wamekwenda msibani kufanya nini? Niliuliza tena swali lililoonekana kumkera binti huyu.
Kichwa ngumu.
 
Maswali mengi kama polithiiii[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
...79
Unakichwa kigumu sana wewe, naomba tuyaache hayo, alinikata kauli yunge mdogo.
Nami sikutaka kumsumbua zaidi nikaamua kubadili stori, hivi yule yunge mkubwa anatoka na nani kimapenzi?
Yule kiukweli sijui na wala sijawahi kusikia kabisa, yaani wewe ndo wa kwanza kuwa nae naamini hivyo, alijibu.
Mimi ni wa kwanza kuwanae nani kakwambia? Nilishangaa.
Kwani ni uongo kuwa wewe ndo umemtoa usichana wake? Aliniuliza.
Yeye ndo kakwambia ama nani? Niliuliza tena.
Hakuna siri tena kwamba wewe na yunge mkubwa ni wapenzi, tena hata wewe umetolewa uvulana wako na yunge mkubwa, aliongea kwa kebehi yunge mdogo.
Mbona watu wa kijiji hiki licha yakuwa wachawi lakini mbona pia ni waongo na wambea sana? Nilivunga kuchukia.
Sasa unamkasirikia nani? Kwani Kuna mtu alikushauli umtongoze? Si uliupenda upole na uchangamfu wake? Alikoroma yunge mdogo.
Sasa mbona unaongea kama unahasira na mimi, nmekosea kuuliza?
Hapana hujakosea na uposahihi kabisa, ila moto uliouingia ndugu yangu utakuunguza vibaya na hutatoka kamwe.
 
Ukitaka kujua humu kuna watu hawana akili hata ya kuvukia barabara siku moja njoo na story yako unayotamani kushare na jamii

Utasikia Muongo, umecopy sio wewe, chai hii dah

Mtu anakwambia nimelala na njaa wewe unamwambia "Muongo" ulikuwepo?

Kuna siku nilitamani kushare na jamii na kuwaelezea simulizi flani jinsi nilivyofanikiwa kumkamata mwizi wa mitandaoni na zile njia nilizotumia na wao wezi njia wanazotumia

Yanii mimi mwenyewe ndio nimemkamata huyo Mwizi ,
Na Rb ninayo mfukoni anatokea mtu humu hata hana anachokijua anakwambia tu chai hio Muongo, umecopy wewe

Mara nyingi tunakosa kupata taarifa mbali mabli kwa sababu ya watu wachache wenye Tabia za utoto utoto na za kijinga zinawakatisha tamaa wasimuliaji

Binafsi nikifunga hadith au simulizi humu nikiona alijanipendeza naondoka bila ya kuaga sio kucomment vimaneno vya kuwakera wengine wanaofatilia
Mkuu kwenye wengi kuna mengi. Nakumbuka nipo mdogo mzee akinambia matusi/zogo la mpita njia lisiku shughulishe ukiwa ndani mwako. Hapa kuna watu wana matatizo yao binafsi ya maisha usiweke akili nani kasema hivi na nani kasema vile. Wewe weka stori yako wapo watakao jifunza na wapo watakao idharau. Ndio maana shule kumewekwa wanao faulu na wanao feli.
 
Baelezee bana, Kama chizi baki huko huko na uchizi wako. Tiache sie tufaidi.
 
Back
Top Bottom