Pettymagambo
JF-Expert Member
- Aug 21, 2017
- 1,490
- 8,227
- Thread starter
- #461
...80
Moto niliouingia? Unamaanisha nini.
Tuyaache hayo utajionea mwenyewe siku ikifika, alinikatisha.
Kiukweli mimi yule simpendi kamwe, na sijui ilikuwaje tu mpaka nikajikuta nipo nae, nilisema.
Basi sawa, asante kwa msaada wako, ngoja niwahi nikaanue maharage yasinyeshewe mvua, alisema baada ya kuwa tumemaliza kumenya karanga na sasa wingu zito lilitanda kuashiria huenda muda si mrefu ingenyesha mvua.
Nilimwomba akimaliza kuanua maharage arudi pale kwani kuna jambo la muhimu nilitaka kumwambia.
Twende unisaidie kuanua kisha turudi wote, aliniomba nami kwakuwa nilikuwa na langu moyoni nilimkubalia na kumtaka anipe ile ndoo iliyokuwa na karanga, alinipatia kisha tukaanza kuondoka, sikufunga mlango wa nyumba niliyokuwa nalala kwani nilijua hatutokawia kurudi.
Tulipiga hatua kuelekea kwao yunge mdogo, lakini mara tulipofika tu kwenye mpaka wa kiwanja cha babu na chakina yunge mdogo nilisikia mlango wa nyumba niliyokuwa nalala umejibamiza kwa nguvu paa!
Niligeuka haraka lakini kwa mshangao mlango ulikuwa wazi.!