133
Niliingia jikoni kwa lengo la kuchota maji nikaoge.
Yunge alinitaka nibebe sabuni tu kwani maji angenisaidia yeye kupeleka bafuni, sikuwa na ubishi, nilifanya vile yunge alivyotaka.
Nilianza kuoga huku yunge akiwa amesimama nje ya bafu akiningoja.
Kesho tunaondoka wote kwenda mbugani kwetu tukasaidizane kuyavuruga yale majaruba ili tupande mme wangu, nataka tukioana maswala ya kununua mchele kwenye makopo sitaki, aliongea kwa utani yunge.
Nisawa, lakini mpaka niongee na babu nimwulize kesho kunaratiba gani asubuhi, kama hakuna, basi tutaenda huko, nilimjibu.
Kuhusu babu nishamwambia hilo muda tu nilipofika hapa, kwani nilimkuta anawasha moto ndipo nilipompa habari hii na hakuwa na shida ameruhusu twende, alijibu yunge.
Sawa, tutaenda lakini ni vizuri namie nimwombe ruhusa hata kama wewe umemwambia, nilijibu.
Sawa mie naenda ila nitakuja kulala nawe mpenzi wangu kwani nimekumisi sana na baridi hili, uegeshe tu mlango usiweke komeo sawa, aliuliza yunge nami nikamkubalia kisha akaondoka.