True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

Heading ya hii story haikunivutia kabisa,hvyo nilkuwa naipitiliza tu lakin kuna member niliona anaisifia kwenye ile story ya ujambaz wa chuga,tabora kigoma zambia ndo nikaamua niisake,nimeipenda sana

Weka weka na uongo ili iwe tamu zaidi
Wewe sawa na mimi kabisa, huku kwenyewe nimefika kwa msaada wa link aliyoweka yule jamaa na sasa hivi nipo page ya 37 nachanja mbuga tu.
 
Tuliza mshono wewe.
kasema mwenyewe muda wake wewe inakuwasha nini
Mwambie mama yako aliyefanyiwa operation ukazaliwa wewe ndio atulize mshono. Kwa kuwa wewe ni jobless na unakula kulala bure hapo kwa shem wako unafikiri kila mtu ana nafasi ya kuandika na kuchat huku kila saa ili akuridhishe wewe. Toka hapo kwa dada yako, mtaolewa wote.
 
132
Niliondoka pale uwanjani huku madogo kadhaa wakiwa wananifata kwa nyuma kwani nilikuwa napita njia inayoelekea senta hivyo bila shaka wale madogo walikuwa wanaelekea vijiweni.

Mamaaa! Ilisikika sauti ya dogo mmoja kati ya wale waliokuwa wananifata huku wakiongea kikabila, king'wana kenaka kamanile ompira, kalubhagalucha gete bhana numbhu mshikome {haka kajama kanaujua mpira, kalikuwa kanawageuza kama maviazi motoni} nilibaki kucheka kimoyomoyo huku nikiwaza kila mpenda mpira pale kijijini atanipenda tu.

Nilishtuka na kugeuka nikarudi pale alipokua yule dogo na wenzie wakiwa tayari wamemzunguka wakimwuliza kapatwa nini?
Huku akiwa kakaa na akiendelea kulia, nilimfikia na kumwuliza umepatwa na nini?
Ghafla alitoka nduki huku akicheka na kusema danganya totoo!

Upuuzi huu, nilisema huku wale madogo wengine wakicheka na kumraani mwenzao kwa kitendo alichofanya.

Nilishika njia ya kwenda nyumbani ambapo niliwakuta yunge na bibi wanapiga soga jikoni, niwasalimu na bahati nzuri moto ulishawashwa na babu.
 
133
Niliingia jikoni kwa lengo la kuchota maji nikaoge.
Yunge alinitaka nibebe sabuni tu kwani maji angenisaidia yeye kupeleka bafuni, sikuwa na ubishi, nilifanya vile yunge alivyotaka.

Nilianza kuoga huku yunge akiwa amesimama nje ya bafu akiningoja.

Kesho tunaondoka wote kwenda mbugani kwetu tukasaidizane kuyavuruga yale majaruba ili tupande mme wangu, nataka tukioana maswala ya kununua mchele kwenye makopo sitaki, aliongea kwa utani yunge.

Nisawa, lakini mpaka niongee na babu nimwulize kesho kunaratiba gani asubuhi, kama hakuna, basi tutaenda huko, nilimjibu.

Kuhusu babu nishamwambia hilo muda tu nilipofika hapa, kwani nilimkuta anawasha moto ndipo nilipompa habari hii na hakuwa na shida ameruhusu twende, alijibu yunge.

Sawa, tutaenda lakini ni vizuri namie nimwombe ruhusa hata kama wewe umemwambia, nilijibu.

Sawa mie naenda ila nitakuja kulala nawe mpenzi wangu kwani nimekumisi sana na baridi hili, uegeshe tu mlango usiweke komeo sawa, aliuliza yunge nami nikamkubalia kisha akaondoka.
 
133
Nilitoka bafuni nikaingia getoni mwangu ambamo nilibadili nguo kisha nikatoka na kwenda kuota moto ambapo babu pia alikuwa ameshafika na anafaidi.

Tulipiga soga na babu pale huku tukifurahi, babu alipenda stori za ujanani ambapo alinambia alikuwa anatembeza vichapo kwa mabinti wengi kwa posho ya maziwa tu kwani kwao palikuwa na ng'ombe wengi mno mpaka kupelekea wengine kutokukamuliwa.

Baadae bibi alileta msisi pale, tulishiriki wote na tuliposhiba bibi aliondoa vyombo na kutuaga anakwenda pumzika kwani kichwa kinamuuma mno.

Basi babu alinambia nilitakiwa kwenda na yunge mbugani kwao ili tukavuruge majaruba niliyopewa, nilimshukuru babu kwa ruhusa ile kisha niliingia ndani na kujilaza huku nikiwa nimeegesha tu mlango kwa lengo kwamba yunge akija asukume tu.

Nilijilaza kitandani pale na kufungulia kiredio changu huku nikitafuta stesheni iliyokuwa inapiga nyimbo bongo flava, muda kidogo nilisikia dirisha linagongwa, nilijua atakuwa yunge tu, hivyo nilimwambia asukume mlango kwani nimeegesha tu

Mh! Tatu?
 
Back
Top Bottom