True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

147
Nilishtuliwa usiku sana na kelele za mafisi, yalikuwa yanatoa sauti mbaya mno, baadae niligundua kumbe yalikuwa mbali na pale nyumbani hivyo hofu ilipungua, nilipitiwa usingizi tena mpaka asubuhi.

Hodi, ilikuwa sauti ya yunge akigonga dirishani.
Nakuja, nilimjibu huku nikinyanyuka kitandani, nilivaa nguo na kwenda kufungua mlango, nilimwona yunge akiwa na jembe moja kuashiria alikuwa tayari kwenda mbugani.

Oooh! Bibi umempitia mchumba wako kwenda majarubani? Samahani sana mwenzio hayupo sawa, nitakujulisha akipona sawa mwanangu? alisema babu hata kabla hatujaongea neno lolote na yunge.

Sawa babu, shkamoo, alikubali yunge na kusalimia.
Marahaba, hatakiwi kutoka nje baridi kali hili, hivyo mwache alale, alikomalia yunge ambae alinisalimia na kuniuliza kwa sauti ya chini, umepatwa nini jamani?
Tutaongea tukipata muda, niache nipumzike kwani nahisi baridi kali sana, nilimdanganya akanipa pole na kuaga yeye anakwenda mbugani kuvuruga na mchana angepita kunijulia hali.

Tule haraka tunakazi nzto ya kufanya.
 
148
Tulimaliza kula msosi wa asubuhi maarufu shipolo kwa kisukuma, ila nyie waswahili mnaita sijui break nini huko.

Tuliondoka kuelekea kule mbugani huku tukipita karibu na bomba la maji ambapo kulikuwa na wasichana kadhaa.

Usiwasalimie, alinambia babu kwa sauti ya chini.
Hamjambo wake zangu? Alisalimia babu ambapo wote waliitikia.

Tuliwapita huku nimeinamisha kichwa.
Tulifika mbugani tukawakuta wale vibarua wanapiga job kama kawaida.

Baada ya kuwasalimia tulielekea kwenye kijumba kile kidogo ambapo babu alinitaka nichukue mkaa nikoke moto pale nje, nilifanya kama alivyonambia huku yeye akielekea lamboni na muda kidogo alirudi na samaki wawili wakubwa na watatu wa wastani, tulimbanika mmoja aliyekuwa mkubwa kushinda wengine kisha tukamshambulia mpaka akaisha.

Jana uliniuliza kwanini ile siku tulikufanyia utundu mimi na bibi yako na wakati huohuo nisijue kama anajihusisha na mambo ya ulozi.
Kwanza ile siku nilikuwa nakufanyia viini macho tu, yaani macho yako yanahama na na taswira ya mtu
 
149
Macho yanahama na taswira ya mtu 1 kwenda nayo kwa mwengine, nimchezo rahisi mno ila kwa asiejua ataona maajabu, alisema babu.

Kumfahamu mtu kama ni mchawi hatakama ni mkeo ama mme ni ngumu mno labda muwe washirika, alisema babu.

Nawewe je, ni mganga au? Maana watu wengi wanakusema vibaya sana, eti wewe ni mchawi, nililopoka.

Unajua watu wengi hawanipendi kwakuwa mipango yao yote mibaya juu yangu huwaga inagonga mwamba na kufeli vibaya mno, watu hawajishugulishi kutunza mazao yao shambani ili wavune kilicho bora badala yake wanapita kwenye mashamba ya wenzao kukagua nani anamazao mazuri ili wamwekee chuma ulete, hilo kwangu nilishalidhibiti na hiyo ni moja ya sababu inayowafanya wanisemee maneno mabaya.

Zamani ilikuwa mtu akija kufanya michezo michafu shambani mwangu hatoki salama, lazima ubongo uyumbe na kupelekea hata kifo kabisa huku akitaja tamaa yake ya kuingia shambani mwa buhabhi imemponza.

Baadae niliona dawa nibadili kutokana na maneno kuwa mengi sana na kupelekea niogopwe sana, niliogopwa.!
 
Back
Top Bottom