True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

157
Nilikimbia na kuzunguka nyuma ya nyumba niliyokuwa nalala kwani ndiko nilitakiwa kuogea.

Babu alinipa maelekezo namna ya kuoga huku akinisimamia mpaka nikamaliza.
Alinitaka niliache pale karai angelibeba yeye na akanitaka niizunguke upande wa pili wa nyumba tofauti na nilikopitia wakati naenda kuoga, nilipita upande ule na nilipotokeza kwa mbele ya nyumba nilimwona yunge mdogo anawasha moto pale nje ambapo huwa tunaota na babu.

Nilipita kwa haraka mpaka chumbani ambako nilishangazwa na hali niliyoikuta, chumba kilikuwa tofauti na asubuhi nilipoamka na kufata maji, yaani kulikuwa na vitu vingi vya ajabu ajabu, upembe mdogo ulioonekana kama wa kondo kutokana na kujipindapinda, vibuyu vitatu ambavyo vilivekwa hirizi kuvizunguka shingoni, mkia mfupi mweusi ambapo nilijua utakuwa mkia wang'ombe ukiwa umechomekwa vihirizi kwenye manyoya yake.

Nilishangaa vitu vile kuwa juu ya kitanda ambapo hapakuwa na godoro bali ngozi kubwa ya kakhi yenye mabaka meusi, {ilikuwa ngozi ya chui}
Nilibaki nakodoa macho tu.
 
158
Jifunge hii, alisema babu akinikabidhi nguo nyeusi ama kaniki, nilipokea na kujifunga kwa kuipitisha kwapani na kuizungusha nyuma ya shingo.

Sasa mwanangu nakukabidhi vitu hivi vikusaidie kukulinda mpaka atakaporudi mzee mapengo atupe utaratibu wa kufanya, alisema babu akinionesha ule upembe na mkia, kesho ukiamka vizuri nitakuelezea kila kitu kilchotokea na kwasasa twende nje mwenzio anakungoja akujulie hali, alisema babu kisha akatoka nje.

Niliziangalia zile zana pale kitandani nikajua mambo yamekwiva sasa, hizi siyo siraha za maangamizi kweli? Upembe wenye kuzungukwa mahirizi, vibuyu lundo vyenye mahirizi shingoni, mkia{usinga}wenye hirizi kadhaa na ngozi ya mnyama hatari sana, vyote vilikuwa eti mali yangu nisijue namna ya kuvitumia, ngoja tuone, nilijisemea na kuelekea nje ambako yunge mdogo alikuwa amekaa kuningoja.

Pole kwa majanga yaliyokukuta mchumba, alisema yunge mdogo huku akiniangalia machoni ambapo nilinamisha uso chini nisijibu.
Afadhali moyo umeanya kutulia kukuona katika hali hii.
 
159
Sikuelewa ananipa pole ya nini wakati asubuhi nilikuwa mzima wa afya.

Kwani nimepatwa na nini? Mie sielewi kabisa kilichotokea mara baada ya kukorofishana na tatu asubuhi bombani, nashangaa najiona kuwa tofauti na hali niliyokuwanayo asubuhi, ebu nambie nmefanya nini? Nilimwuliza yunge mdogo ambae hakutaka kufungua kabisa na nilihisi atakuwa amezuiliwa kuniambia.

Nitakusimulia usiku tukiwa tumelala, alisema yunge mdogo.
Nilishangaa kwa kauli yake ile ya kunisimulia tukiwa tumelala, yaani utafikiri tulikuwa na mazoea ya kulala wote ama tumeoana.

Wakati nikiyatafari hayo yunge mkubwa alifika pale nyumbani na kutusalimia mimi na yunge mdogo huku akiniuliza vipi hali yangu, hapa nikajua kabisa kulikuwa na jambo kubwa lilokuwa limenitokea.

Mie mbona nipo kawaida tu? Sina tatizo lolote, nilimjibu.
Nzehe naomba uegeshe mlango usibane, nakuja nikulinde mchumba sawa? Aliongea yunge mdogo akinyanyuka huku akingoja jibu langu aondoke.
Sawa, nilijibu huku nikimwangalia yunge mkubwa ambae lionekana kuchukia sana.
 
160
Aliondoka yunge mdogo akaingia jikoni alimokuwa bibi anapika, nilimsikia akiaga kwa sauti ya juu huku akimwambia bibi angerudi kuja kuniangalia usiku mzima, nilimsikia bibi akimruhusu ambapo alisogea kwenye dirisha la nyumba kubwa akawa anagonga na kumuaga babu pia na kama alivyofanya kwa bibi, alimwambia pia babu kwamba angerudi baadae kuja kuniangalia usiku wote.

Tulibaki pale na yunge mkubwa ambae hakuwa amekaa bado, alionekana kuwaza sana, huenda aliwaza juu ya maneno aliyoongea yunge mdogo ama la! Sikupata jibu japo niliamini ni hayo tu.

Alienda jikoni alimokuwa bibi, alimsalimia na akaelekea dirishani pale alipoenda yunge mdogo na kumuaga babu, alibisha hodi yunge mkubwa na kumsalimia babu kisha akarejea na kukaa kwenye kiti kilichokuwa karibu yangu.

Umeanza lini kulala na yule mchawi? Aliniuliza yunge mkubwa kwa sauti ya chini lakini iliyoonekana kuwa na wivu waziwazi.

Nilikaa kimya nisimjibu.
Nzehe si nakuuliza, mmeanza lini kulalanae mpaka mnaitana mme na mke? Aliuliza tena yunge mkubwa....!
 
161
Nilijikuta naanza kuchukizwa na maswali yake sasa, nilimuona anataka kunicontroo, nilikaa kimya nisimjibu.

Kwahio umekua mtu wa tamaa kiasi hiki mpaka kupelekea kila msichana unaeonana naye umtake kimapenzi sio? Naanza kuamini maneno ya tatu sasa, aliongea yunge mkubwa huku akinyoosha mkono wake na kunifinya kwa nguvu mkononi mwangu, ajabu aliniachia haraka sana utafikiri mtu alieshika mkaa wa moto.

Alisimama na kuniangalia kwa macho ya chuki, aliondoka kwa unyonge tena bila kuaga akisema, sitokubali kuchezewa akili hata kidogo, nitawakomesha lazima, aliongea akiishilizia nyuma ya nyumba kubwa ya babu mahali ilipokuwepo njia ya kwenda makwao.

Umemsikia alivyosema? Aliuliza babu akiwa kasimama mlangoni.

Hawa wanataka kutuchezea hawa, tumewalea sana hawa, muda umefika tuwanyooshe sasa, alisema babu huku akiwa tayari amenifikia na kuutwaa mkono wangu akiniangalia nilipofinywa na yunge mkubwa.

Mhh? Inamaana babu kaona yote? Niliwaza huku nikitupa jicho pale nilipofinywa, niliona mikia miwili ya..!
 
Duuh kweli hako ka Yunge kanataka kakupande kichwa bhaghoshaaa
 
Hatakama ungekua wewe lazima uchukie tu, kwawakati ule nilihisi kama hakuwa na hakai ya kuniganda vile, ila kwa sasa, naelewa mapenzi yanavyoweza kumfanya mtu akatenda mambo ya ajabu.
Daaah! Huko kijijini hapafai hata kwenda kwa kweli!
 
Back
Top Bottom