True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

umeona eeehhh..... jamaa anadhani anasimulia watoto wenzie. mara babu yake alimtuma kisimani mara anaenda bombani anajichanganya tu. na uandishi wake dogo anaweka maneno ya kitoto tu hajui hata kusimulia.
We unajua kusimulia?? Acheni kujikuta
 
Ukitaka kujua humu kuna watu hawana akili hata ya kuvukia barabara siku moja njoo na story yako unayotamani kushare na jamii

Utasikia Muongo, umecopy sio wewe, chai hii dah

Mtu anakwambia nimelala na njaa wewe unamwambia "Muongo" ulikuwepo?

Kuna siku nilitamani kushare na jamii na kuwaelezea simulizi flani jinsi nilivyofanikiwa kumkamata mwizi wa mitandaoni na zile njia nilizotumia na wao wezi njia wanazotumia

Yanii mimi mwenyewe ndio nimemkamata huyo Mwizi ,
Na Rb ninayo mfukoni anatokea mtu humu hata hana anachokijua anakwambia tu chai hio Muongo, umecopy wewe

Mara nyingi tunakosa kupata taarifa mbali mabli kwa sababu ya watu wachache wenye Tabia za utoto utoto na za kijinga zinawakatisha tamaa wasimuliaji


Binafsi nikifunga hadith au simulizi humu nikiona alijanipendeza naondoka bila ya kuaga sio kucomment vimaneno vya kuwakera wengine wanaofatilia
Umenena vyema
 
...77
Mbona umeharibu dawa yangu? Alinitupia swali babu, nilibaki kushangaa tu, nilikumbuka yunge alivyonibana mpaka nikakubali kwamba nimechanjwa chale na kupakwa dawa.
Nilisahau kukuambia sharti moja, nikwamba hukutakiwa kukubali hata kama amejua, hatakama amekuona, ili dawa isiharibika hukutakiwa kukubali, lakini imeshatokea na hiyo dawa imekufa hivyo tuangalia namna nyingine, alisema babu na kunitaka nibaki pale muda wote kwani wao wanakwenda msibani.
Kuna msiba wapi tena babu? Nimwuliza.
Ee kuna msiba tena umetokea, baba wa yule mtoto alieliwa na fisi amefariki ghafla asubuhi ya leo wakati jana alikuwa yu mzima wa afya, alijibu babu akimaanisha yule jamaa tuliekuwanae juu ya mti usiku na kumsikia akilia mama yake kumchinja mjuku wake.
Inamaana amekufa? Nilijiuliza.
Sawa babu mie nipo hapa.
Nilimwona bibi anatoka ndani, ila tulipokutanisha macho nilimwona kashtuka kidogo, nilimuwahi kwa kumsalimia na vijiutani kidogo, sikutaka ahisi kitu kama yunge alivyopa maelezo.
Kuna viazi na uji utakula mme wangu..!
Ngoja nisome nitacomment badae
 
Mahali nilipo siyo rafiki, naona kufikia saa 12 jioni nitakuwa nimefika sehemu yangu huru na nitaanza kuziweka kwa wingi.
Kwani hizi story huwa mnaandika na kuzificha mahali , mnakuwa mnadokoa tuepisode tumoja tumoja ama huwa mnaandika na kupost,??? Nawaza tu vile niko mvivu kutype siku nikileta story yangu nitakavyoshambuliwa na mitusi
 
Zipo mbili mkuu ila zina arosto ya kufa mtu

Nakwenda kuzicheki, bila shaka arosto mtakuwa nayo nyie ambao mlianza kuisoma mapema.

Sasa nikushangaze hii title ya uzi ulionipa link hua naiona several times ila hua naikwepa wala sijawahi kuifungua.

Asante kwa ushirikiano mkuu.
 
158
Jifunge hii, alisema babu akinikabidhi nguo nyeusi ama kaniki, nilipokea na kujifunga kwa kuipitisha kwapani na kuizungusha nyuma ya shingo.

Sasa mwanangu nakukabidhi vitu hivi vikusaidie kukulinda mpaka atakaporudi mzee mapengo atupe utaratibu wa kufanya, alisema babu akinionesha ule upembe na mkia, kesho ukiamka vizuri nitakuelezea kila kitu kilchotokea na kwasasa twende nje mwenzio anakungoja akujulie hali, alisema babu kisha akatoka nje.

Niliziangalia zile zana pale kitandani nikajua mambo yamekwiva sasa, hizi siyo siraha za maangamizi kweli? Upembe wenye kuzungukwa mahirizi, vibuyu lundo vyenye mahirizi shingoni, mkia{usinga}wenye hirizi kadhaa na ngozi ya mnyama hatari sana, vyote vilikuwa eti mali yangu nisijue namna ya kuvitumia, ngoja tuone, nilijisemea na kuelekea nje ambako yunge mdogo alikuwa amekaa kuningoja.

Pole kwa majanga yaliyokukuta mchumba, alisema yunge mdogo huku akiniangalia machoni ambapo nilinamisha uso chini nisijibu.
Afadhali moyo umeanya kutulia kukuona katika hali hii.
Kuna kurudi nyumbani kweli au ndio tushazamia kwa babu kizaa baba
 
Back
Top Bottom