True story!! Kwenye mapenzi tuwe makini kabla ya kuingia kwenye mahusiano

True story!! Kwenye mapenzi tuwe makini kabla ya kuingia kwenye mahusiano

Wakuu kwema?
Leo mida ya asubuhi nimepokea simu kutoka kwa rafiki yangu/mdg wangu jinsia ya KE. Akanielezea mkasa ambao alitaka nimshauri. Nimeona sii vibaya nikishea hapa jukwaani huenda akapata mawazo mazuri zaidi.
Huyu rafiki yangu ni kama mdogo wangu maana kaka yake amewahi kufanya kazi kwangu kipindi fulani 2022. Amekua kila akikutana na jambo linalohitaji ushauri ananishirikisha namshauri, siku zinasonga.
Kipindi hiki cha sikukuu alisafiri kwenda kwao(Moshi) kusherekea sikukuu za mwisho wa mwaka. Akiwa na mama yake mzazi alimshirikisha kua amepata mchumba ambae anaamini siku zijazo atakua mumewe. Mama yake alimpongeza, na baada ya hapo Alimuonesha picha mbalimbali walizopiga wakiwa pamoja. Kwa bahati nzuri/mbaya mama yake aliona sura ya yule kijana akahisi kumfahamu au kumfananisha na kijana anaemjua. Alimuuliza bintiye huyu kijana ni wa wapi akamjibu kwao ni Mwanza. Mama yake alivotajiwa majina ya kijana akamwambia huyu ni mtoto wa shangazi yako(akamtajia jina la shangazi).
Ghafla Mama yake akaanza kumuuliza ilikuaje mmekutana mkaanza mahusiano? Akawa mkali na kumwambia afute picha hizo na hayo mahusiano ayaache mara moja. Binti anasema anampenda lkn hajui afanyaje maana ameshaambiwa wasiendelee. Na kijana ameshaonywa tayari. Nimemuuliza ilikuaje hujui ndg zako? Akasema anajua ndg upande wa mama pekeake maana ndio alieishi nae.
Mimi nimemshauri kua yeye bado ni mdogo (26) anamuda wa kupata mtu mwingine sahihi na maisha yakasonga.

Ungekua wewe ungemshauri nini huyu dada? Ataendeleaje na mahusiano na mtu ambae ni ndugu yake?
Asiendee na uhusiano amshukuru Mungu.Ndugu wa damu kuoana mnazaa viumbe dhaifu
 
Mtoto wa shangazi au mjomba wanaoana vizuri tu na hata kisheria gaina shida.
Huo ni undugu wa mbali,angekuwa dada wa Mama mdogo au Mama mkubwa ndio kidogo utaina soo.
 
Ni kweli mkuu
Kwahyo kwa upande wako utamshaurije? Afanye maamuzi gani
yeye umeona analichukuliaje?

kuna ile aibu fulani ya kumchungulia ndugu bahati mbaya ile,

ameogopa au amechukia kuzuiwa penzi lake?
 
Hapo wewe vuta goma hilo weka ndani.!!
Km huwezi weka namba wanaume wenzio wa hapa JF wakusaidie kumshauri madhara ya kuwa na mahusiano na kaka yake.!!
 
yeye umeona analichukuliaje?

kuna ile aibu fulani ya kumchungulia ndugu bahati mbaya ile,

ameogopa au amechukia kuzuiwa penzi lake?
Anasema Bado anampenda
Anaongea kwa kilio kabisa. Yupo tayari km mzazi anabariki kuendelea nae hatomuacha
 
Hapo wewe vuta goma hilo weka ndani.!!
Km huwezi weka namba wanaume wenzio wa hapa JF wakusaidie kumshauri madhara ya kuwa na mahusiano na kaka yake.!!
Nina goma langu tayari
Alaf si unajua, sii kila ukiona kichaka unabanwa na haja. Nawaachia wadau msio nao, jimbo ilo
 
Back
Top Bottom