True story: Nimeamua kumkataa mtoto rasmi

True story: Nimeamua kumkataa mtoto rasmi

Kwa hiyo mleta uzi unapata amani kwa kuwa wana JF wamekuelewa, kana kwamba wao wanaishi maisha yako!

Mimi ni mwanamme, ila ningekuwa mwanamke halafu nimezaa na mtu asiye na utayari kulea mtoto, sidhani kama ningembembeleza.
 
Kwa hiyo mleta uzi unapata amani kwa kuwa wana JF wamekuelewa, kana kwamba wao wanaishi maisha yako!
Mimi ni mwanamme, ila ningekuwa mwanamke halafu nimezaa na mtu asiye na utayari kulea mtoto, sidhani kama ningembembeleza.
Najua wamenielewa au kuna kitu wameelewa/jifunza
 
SEHEMU YA PILI:

Kabla ya picha picha kuanza wakati nikiwa nae nyumbani haraka tukafunga ndoa ya bomani ili anapokwenda kuripoti kazini asajili cheti cha ndoa kusudi aanze haraka kufanya michakato ya kuhamia mahali alipo maisha yaendelee, akaenda zake.

Baada ya muda mfupi akaja kunitembelea nikafurahi sana kwamba bado anakumbuka kuna mtu amemuacha huku anayemhitaji na sasa maisha ya ajira yakawa yameanza kumkubali akanawiri akapendeza zaidi lakini kuna kitu kikanitia mashaka, hakuwa na pete ya ndoa[emoji848][emoji848][emoji848] nikamuuliza akajibu inambana nimnunulie nyingine, sasa hivi ndio najiuliza pengine aliposema inambana hakumaanisha nilivyoelewa, inawezekana alimaanisha inamzuia kufanya mambo yake...hilo nikamezea.

Akaondoka ndio hapo sasa ilipofika mwisho wa mwaka huo, kiufupi ni miezi isiyozidi minne tu tangu tule yamini pale bomani akaniambia ana ujauzito [emoji2307][emoji2307]kwa maana kwamba ni ujauzito alioupata alipokuja kunitembelea

Lakini uwasilishaji wake haukuwa wa furaha kabisa, wajua mimi nina uwezo wa kuhisi sana mambo, hata nikiongea na mtu tu kwa njia ya simu nahisi zile hisia zake halafu naunga dots haraka. Kwanza akawa jeuri jeuri hivi, baadae ndio akanijulisha juu ya ujauzito huo.

Mimi nikafurahi sana maana kwa umri huo wa katikati mwa 20's nilikuwa na moto hasa wa kupata mtoto, na sio mtoto tu bali mtoto na BM, Haraka nikamuuliza ana hakika ili niwajulishe nyumbani? Akajibu niwajulishe tu, basi sawa mimi nikawaambia home.

Tukaendelea na maisha lakini mimi nikawa na wasiwasi sana, wasiwasi nisioelewa ni wa nini, lakini kwa upande wake hakuwa sawa kuna vitu sikuviona sawa kabisa hasa kwa mtu uliyemzoea.

Mawasiliano yakawa hafifu kidogo plus majibu makavu makavu hivi baada ya mwezi au miezi miwili nilipokuwa najibebisha nikamuuliza kijacho wangu hajambo? Akanijibu kijacho gani?

Nikamwambia wewe si ndio ulisema una ujauzito mpaka home nimewajulisha?
Akanijibu nani ana mimba?

Nikiri wazi katika maisha yangu kuna kipindi nilipitia kudata kwa hali ya juu na kipindi chenyewe kilikuwa hicho.

Kumbe ule wasiwasi wangu Usio na sababu ulikuwa unani-alert na jambo fulani lijalo.

Baada ya majibu hayo makavu nikakaa chini nikajiuliza sasa nyumbani ntawaambia nini tena? Na nikiwaambia wataelewa nina mwanamke wa aina gani? Hii si aibu?
Yaani katika suala zima mimi kilichoniumiza ni aibu tu..sipendi aibu kuliko chochote.
Kuna kitu kimoja tu nilichoamini wakati huo kwamba huyu Mimba alikuwa nayo, sasa;
Inawezekana ni yangu lakini kwa sasa hanihitaji ndio maana siku za karibuni alipata mabadiliko ya tabia kwahiyo akatoa mimba JAMBO AMBALO NI BAYA NA LA AIBU mke kutoa mimba yako, Au inawezekana mimba haikuwa yangu akaona akiiacha atafanyaje na anaishi kwenye ndoa? Akaona bora anipe mimi lakini baadae akaona bora atoe tu JAMBO AMBALO NALO NI BAYA NA LA AIBU mke kupata mimba nje ya ndoa yake.

Kwa haya yaliyoanza kuizonga akili yangu taratibu nikaanza kubadilika/kuvurugika
Watu wangu wa karibu walishtukia tu nimeshakuwa mlevi wa kupindukia lakini siri hii mpaka kesho ninayo mimi tu juu ya nini kilinivuruga, nashukuru Mungu nilikipita kile kipindi kigumu baada ya miaka kama miwili ya kupitishwa katika tanuru la moto halafu nikaibuka kuwa imara ajabu.

Basi bwana, hilo suala nikiwaza kukaa kimya haiwezekani, nikifikiria kuwajulisha nyumbani kichwa kinapata moto[emoji27][emoji27][emoji27]hali inaniacha dilemma, nachanganyikiwa, nadhoofu, nawaza, nazidi kuwa mlevi tu[emoji24][emoji24]

Mpaka hapo mimi nilishaanza kujua BM wangu ameshaanza kuzuzuka baada ya kuanza kupendeza na ajira, ndio kilichoanza kuzunguka akilini mwangu, basi siku moja nikajivisha mabomu nikamwambia mama kwamba ujauzito wa mkwe wao umeharibika

Sikutumwa kusema hivi, yaani kwa jinsi nilivyompenda nikapanga kumlinda wasijekuniambia niachane nae, ni jambo ambalo sikutaka kusikia hivyo nikadanganya imeharibika

Lakini mama ni mtu mzima aliguna tu, hili likapita kidogo pakatulia.
Baadae kidogo kuna binti nilikuwa nafahamiana nae alipata kutembelea mkoa anaofanya kazi BM, akaniambia nimekutana na mkeo ila huu mkoa haumpendi ni kama amepungua kidogo

Mimi nikaunga matukio, alipokuja kwangu alinawiri, na sasa naambiwa kapungua, huyu katoa mimba, iwe yangu au ya mwingine yote ni mabaya. Dah!!

Baada ya miezi kama mitatu tukiwa tumeshavuka mwaka, yaani ni mwezi wa tatu wa mwaka uliofuata dada yake aliyekuwa mkoa niliopo (Ambaye ndiye alimtafutia kile chuo) aliugua ikabidi BM aje kumtazama, huyo dada yake anafanya kazi vijijini ni mtandaji huko. Basi BM akaniita twende wote kwa dada yake niliyemheshimu kama mkwe, nikafurahi sana, wajua ukipenda halafu ukaona penzi linapotea unaumia sana halafu umpendaye akionyesha kitu kama cha kuonyesha uzito wa penzi bado upo unaona kama amekutua mzigo fulani moyoni mwako.

Tukaenda kwa dada yake, tulikaa huko siku tatu mimi nikaondoka kurudi kazini maana niliomba ruhusa ndogo tu, cha ajabu wakati tunaagana akawa anaaga kana kwamba akitoka hapo anarudi kazini kwake mkoani kwake mbali kabisa, yaani hatujaonana muda mrefu, tumekutana juu kwa juu anarudia huko huko[emoji15][emoji15][emoji15] nikamsema akaona aibu ndio baada ya siku mbili akaja kwangu, ieleweke kwamba mimi na dada yake tunaishi mkoa mmoja wilaya tofauti
Kwahiyo akaja kama kawaida pete hanaga tena, akakaa siku moja akaondoka

Alipofika kazini kwake baada ya mwezi akaniambia ana ujauzito, akimaanisha alipokuja alipata ujauzito dah, sifahamu mahesabu ya siku za hedhi lakini nakumbuka tukiwa kwa dada yake alienda kwenye siku zake sijui zilikata lini, baada ya siku kama mbili au tatu akaja kwangu wajuzi wataniambia siku za hatari ni ngapi baada ya kukata hedhi.

Kwahiyo tumefikia hapo nilipoambiwa ana ujauzito, mimi kama kawaida nikafurahi na nikawajuza nyumbani....


Will Be Back...
Uko na age gani??how come mtu anapata mimba unaambia nyumbani..? Kama huishi nae hawapaswi jua wala kumwambia yoyote utaaibika...mwanamke anatoa hadi mimba ya miezi mitatu wewe ki mimba cha week ushatangazia umma..jifunze kubeba aibu zako mwenyewe
 
Uko na age gani??how come mtu anapata mimba unaambia nyumbani..? Kama huishi nae hawapaswi jua wala kumwambia yoyote utaaibika...mwanamke anatoa hadi mimba ya miezi mitatu wewe ki mimba cha week ushatangazia umma..jifunze kubeba aibu zako mwenyewe
Nilikuwa mdogo hata hivyo, shobo za kishamba na kutokujua mambo tu

Nilishajifunza mama
 
Boss.
Kwanza pole sanaaaa, mimi nilikua na mapenzi kama yakoooo hayooo ila nilipoumwa na nyoka nilisitisha uwendawazimu

Huyo si mtoto wako kabisaaa, huyo ni daraja la kupigia helaaa.

Kama unabisha, tumia nguvu kumchukua nakuhakikishia humalizi wiki 2 baba yake atajulikana.

Achana na hiyo Ngiri msee.
 
Boss.
Kwanza pole sanaaaa, mimi nilikua na mapenzi kama yakoooo hayooo ila nilipoumwa na nyoka nilisitisha uwendawazimu

Huyo si mtoto wako kabisaaa, huyo ni daraja la kupigia helaaa.

Kama unabisha, tumia nguvu kumchukua nakuhakikishia humalizi wiki 2 baba yake atajulikana.

Achana na hiyo Ngiri msee.
Dah kuna jambo umezungumza zito sana
Nimepata kitu

Shukrani sana mkuu
 
Wanazinguaa Mastory ya kikudaa tuu...Mara iendele mbelee maraa irudi nyumaa kama time travellers..!! Mtu una mkasa na ulipitia kweli unaweza kusummarize na ikawa bonge la story sio huu Utopo wa kucopy mastory huko unakuja kuleta mainshaa marefuu kama msafara wa wangoni.

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
Hebu andika na ww story yako ndefu tuone.
 
Achana nae, mtoto kama ni wako atakutafuta

Nasema nyamaza kimyaaa tena utulie
 
  • Thanks
Reactions: T11
Back
Top Bottom