Trump aifuta wizara ya elimu.Kisa walimu wengi wanakiunga mkono chama cha Democratic.Mfumo anaoutaka ni K-12

Lazima atashindwa tu, atapingwa kwa nguvu zote.

Marekani Rais hana mamlaka ya kifalme.
 
Asante mkuu kwa udadavuzi wa kina juu ya hili swala,lakini huko mitandaoni wanalalamika baada ya kuvunjwa hii DOE elimu haitakuwa na usawa tena hususani kwa yale majimbo maskini hasa hasa kwenye utoaji wa elimu kwa watu wenye mahitaji maalumu??Kwa maana kuwa hii department of education ilikuwa inasimamia ile principle ya quality and equal education for all.
 
𝐇𝐢𝐥𝐢 𝐧𝐚𝐥𝐨 𝐧𝐞𝐧𝐨 𝐌𝐤𝐮𝐮📌
 
Hahaa.

Hivi unadhani watu wa kulalamika watakosekana?

Chochote afanyacho Trump, au hata Rais mwingine yeyote yule, watu wataolalamika watakuwepo tu.

Kwani unadhani hiyo wizara tokea ianzishwe mwaka 1979 hakukuwepo watu ambao waliilalamikia?

Chini ya hiyo wizara, viwango vya elimu Marekani vimeshuka sana na ndo maana kuna watu wengi tu ambao hawaitaki.

Na kuifuta hiyo wizara ilikuwa ni moja ya ahadi za Trump wakati was kampeni.

Siku ya uchaguzi ilipofika, watu wakamchagua Trump kwa zaidi ya kura milioni 77.

Watu walimpigia kura huku wakiwa nazijua ahadi alizozitoa kipindi cha kampeni.

Kwa vile yeye ndiye aliyeshinda urais, basi aliweza kuwashawishi watu wengi zaidi kumpigia kura yeye.

Hiyo wizara ingekuwa ni ya muhimu sana na kulingana na ahadi aliyoitoa, naamini watu wasingempigia kura nyingi kiasi hicho.

Sasa hivi kuna usawa gani katika elimu chini ya hiyo wizara? Manake viwango vya elimu viko chini sana ukilinganisha na nchi zingine zilizoendelea.

Anachofanya Trump ni sahihi. Huduma muhimu zirudishwe karibu na wananchi.
 
Mwisho huyu Trump ataifuta nchi yote ya Marekani
 

Shida ni kwamba democrats wanalazimisha ushoga kwenye mfumo wa Elimu. So Trump amewaachia waamue wenyewe majimboni kama wanataka ushoga mashuleni au la. Maana kila Maamuzi ya Trump wanayapinga mahakamani hata ya kulinda jinsia ya kike.
 
Kuna Taifa flani hapa Afrca waalimu ni mapoyoyo wa chama Dola! Wakati wa uchaguzi huwasadia chama dola kuiba kura, baada ya hapo hutupwa kama kondom iliokwisha tumika! na wao kuanza kulia lia NJAA! Na wao siku wakimpata Trump wao aifute wizara ya Elimu?
 
Si kweli amefuta kwa sababu hiyo. Uwe unasoma kwa undani na usikilize kile kilisemwa.
Usipotoshe.
 
Asante kwa ufafanuzi mkuu humu watu walijua anafuta shule zote za usa
 
Baraza la madiwani la huko limeridhia huo uamuzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…